Elections 2010 Chadema tunaachiana vijiti

Elections 2010 Chadema tunaachiana vijiti

AMARIDONG

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2010
Posts
2,501
Reaction score
185
ALIYEKOSA nafasi ya kuwania ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rachel Mashishanga, ametangaza kumuunga mkono Fred Mpendazoe anayewania ubunge kupitia chama hicho.

Rachel ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga, alitangaza uamuzi huo hivi karibuni katika kongamano maalumu la kukamilisha maandalizi ya kampeni lililoitishwa na Mpendazoe, jimbo hilo jijini Dar es Salaam.

"Baadhi yenu mlitarajia mimi niwe mgombea lakini sikupita maana Kamati Kuu iliamua kaka yangu Fred (Mpendazoe) kuwa mgombea wetu. Bahati nzuri mimi ni mtiifu, nimekubali maamuzi ya juu ya chama.

Niliumia sana lakini sasa niko tayari, ninamuunga mkono mgombea wetu," alisema Mashishanga na kuamsha shangwe kwa wana CHADEMA waliohudhuria kongamano hilo. Mashishanga aliliambia kongamano hilo lililohudhuriwa na viongozi na wanachama wa CHADEMA kutoka katika kata zote nane za jimbo hilo, kwamba atafanya kampeni za nyumba kwa nyumba na mikutano ya hadhara katika kata zote ili kuhakikisha Mpendazoe na wagombea wote wa udiwani wanaibuka na ushindi.
 
Hongeraeni sana kwa kuanza kuwa wakomavu kisiasa, hata kabla ya kushika hatamu.
Hii ndiyo inatakiwa. Si kuachiana vijiti tu, bali tumpeleke bungeni hata mtu mwenye uzoefu na ameondoka kutokea CCM akalete changamoto kama anazo. Naamini aliona kuna mapungufu na atayatoa vizuri
Good, Big up Mashishanga
 
Tumekomaa siku nyingi sema tunaonyesha njia sasa
 
Wote hamjui kinachoendelea... Amekubali kumuunga mkono mpendazote baada ya kuwekwa nambari moja katika orodha ya viti maalum!!!!!!!... Hii ina maana kuwa tayari kajihakikishia kuwa mbunge kupitia viti vya mteremko kuliko kbahatisha kwa kugombea!!.. Anachoomba mngu ni anagalau chadema wapate viti vichache kwani hata wakiambulia kiti kimoja cha viti maalum, basi ni yeye!!!!!!!!!

Hii ndiyo sababu kura za viti maalum zikafutwa na ikaamuliwa kuwa mwaka huu wataeuliwa kwa utaratibu tofauti na baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu..... Hakuna ukomavu hapo bali kuna "mahesabu makali" sana yamefanyika... Hahah... Ndiyo bongo hii, mwenye akili kali zaidi ndiye hula zaidi....
 
akili miguuni hata hujui unaongea nini na unaandika nini,angekuwa anajua kuwa amechaguliwa viti maaalumuangegombea kwa ajili gani/Masishanga amechaguliwa viti maalumu baada ya kumsaport braza sio kabla alaaaaaaaaaaa
 
Hii ni CHADEMA ina watu waliokomaa na wanaolitakia Taifa letu mema.
 
akili miguuni hata hujui unaongea nini na unaandika nini,angekuwa anajua kuwa amechaguliwa viti maaalumuangegombea kwa ajili gani/Masishanga amechaguliwa viti maalumu baada ya kumsaport braza sio kabla alaaaaaaaaaaa

kwa hiyo amehakikishiwa kweli nafasi ya viti maalum?

hongera zake .............ajitayarishe kufanya kazi ya kutumikia wananchi mjengoni.
 
Back
Top Bottom