AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,501
- 185
ALIYEKOSA nafasi ya kuwania ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rachel Mashishanga, ametangaza kumuunga mkono Fred Mpendazoe anayewania ubunge kupitia chama hicho.
Rachel ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga, alitangaza uamuzi huo hivi karibuni katika kongamano maalumu la kukamilisha maandalizi ya kampeni lililoitishwa na Mpendazoe, jimbo hilo jijini Dar es Salaam.
"Baadhi yenu mlitarajia mimi niwe mgombea lakini sikupita maana Kamati Kuu iliamua kaka yangu Fred (Mpendazoe) kuwa mgombea wetu. Bahati nzuri mimi ni mtiifu, nimekubali maamuzi ya juu ya chama.
Niliumia sana lakini sasa niko tayari, ninamuunga mkono mgombea wetu," alisema Mashishanga na kuamsha shangwe kwa wana CHADEMA waliohudhuria kongamano hilo. Mashishanga aliliambia kongamano hilo lililohudhuriwa na viongozi na wanachama wa CHADEMA kutoka katika kata zote nane za jimbo hilo, kwamba atafanya kampeni za nyumba kwa nyumba na mikutano ya hadhara katika kata zote ili kuhakikisha Mpendazoe na wagombea wote wa udiwani wanaibuka na ushindi.