Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Wakili Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema kuwa wanakusudia kitafungua kesi ya kudai fidia ya shilingi bilioni 100 dhidi ya Said Issa Mohammed na wenzake pamoja kuwafikisha kwenye kamati ya maadili Mawakili wao.
"Said Issa Mohamed na wenzake wameisababishia Chadema hasara ya zaidi ya bilioni 100 na mawakili wao wameshiriki kusababisha hiyo hasara. Tutawasaidia waweze kulipa kwa namna inayostahiki." Mhe. Rugemeleza Nshala,Mwanasheria Mkuu wa ChademaHayo yamesemwa leo Juni 23, 2026 nje ya Mahakama baada ya kuahirishwa kwa kesi mpya ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Zanzibar.
Wakili Nshala amesema hatua hiyo inatokana na hasara ambayo CHADEMA imeipata kufuatiamchakato uliosababisha changamoto ya kesi ya awali ya mgawanyo wa mali ambayo ilifutwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.
Katika kesi ya leo imeahirishwa hadi Julai 7, 2026.