econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,522
- 40,795
Habari wakuu. Leo tarehe 24/7/2026 Makamu wa Rais Dr Emmanuel Nchimbi ametoa kauli za kisiasa ambazo kwangu ni kama mtego kwa CHADEMA. Kabla CHADEMA haijaanza kufurahia kauli hiyo ijiulize maswali yafuatayo.
1. Kwanza, Kama Nchimbi anahimiza watanzania waipiganie katiba mpya, kwanini wanachama wa CHADEMA wanakamatwa nchi nzima kwa kosa la ugaidi kisa kudai reforms? Kama kudai reforms ndogo ni ugaidi je kudai katiba mpya itakuwaje? Hawa waliokamatwa watatumika kama sababu ya kushusha mapambano ya kudai kudai katiba mpya.
2. Pili, kama Nchimbi anahimiza vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA kupigania katiba mpya, je watumie njia gani kupigania katiba mpya?. Maana wakiitisha maandamano jeshi lote linahamia mitaani na vitisho kama vyote. Na hiyo mikutano ya hadhara inafanyika kwa mapenzi ya Waziri na Wala sio Sheria. Atuambie Njia ya kutumika kupigania katiba mpya.
3. Tatu, Nchimbi anahimiza watanzania ya kwamba tuandike katiba mpya kwa ajili ya vizazi vijavyo. Cha kushangaza huyo Nchimbi amesahau ya kwamba Tume ya Jaji Warioba ilikuja na rasimu nzuri sana ila wao akina Nchimbi na CCM yake wakaja na rasimu yao inayojali maslahi yao mchakato ukaishia hewani. Leo nani anamwamini Nchimbi kwenye matamshi ya kuandika katiba itakayotumika vizazi na vizazi?. Kama walishaharibu mchakato wa kwanza?
Mwisho, naomba niwashauri CHADEMA msifate maneno ya Nchimbi bali angalieni matendo ya serikali. CCM sio ya kuiamini kabisa. Tujifunze kwa Mbowe na maridhiano na Samiah, mpaka kupewa tuzo. Ila mwisho wa siku mambo yakageuka mpaka Leo. CCM ni Ile Ile haiwezi kubadilika kamwe.