Elections 2015 CHADEMA/ UKAWA wakitaka kuichapa CCM wamchague Tundu Antiphas Lissu kupeperusha bendera ya Urais

Elections 2015 CHADEMA/ UKAWA wakitaka kuichapa CCM wamchague Tundu Antiphas Lissu kupeperusha bendera ya Urais

Hapana lisu awe mbunge na uwaziri wa mambo ya sheria utaona raha yake....
Pia slaa akikosa kusimama urais basi arudi karatu akagombee ubunge
 
Ukawa mkitaka kuichukua nchi hii msimamisheni kijana Tundu lisu.

Siwakubali ukawa hasa kwa ngazi ya uraisi lakn kama atasimama huyu jamaa Tz watafarakana..

Acheni ubaguzi mtu kama slaa miaka yote tunaliona lenyew tuu na halina ya maana ya kuongea zaidi ya njaa tu.

Ukija lipumba ndip tupa kule tangu 95 anabuluzwa tuu. Tumechoka kuwaona sura zenu na mawazo yenu chakavu
 
CHADEMA (UKAWA) wakitaka CCM wachanganyikiwe mwaka huu, na kubadilisha mchezo mzima wa kunyang'anyana kiti cha urais, Oktoba, 2015, wamchague Tundu Antiphas Lissu kupeperusha bendera ya UKAWA/CHADEMA. Kwa mjibu wa utafiti wangu, watu wanamwona Lissu kama "GameChanger".

Vitu vitakavyowavuta wananchi na kuamua kumpa T. A. Lissu kura zaidi ya asilimia 90 ni hivi hapa:

1. Uzalendo wake wa kuipigania nchi kwa dhati. Tumeona jinsi anavyosimamia ukweli bungeni na kuwavua nguo mafisadi (akiwemo John Pombe) bila woga wala kuogopa mtu yeyote. Jina lake na rekodi alizoziweka bungeni mpaka kesho zinarindima kwenye vichwa na masikio ya wananchi.

2. Ni msomi "pragmatic" mwenye weledi wa hali ya juu wa kujenga hoja "consistently", "logically" na kuzisimamia mwanzo mwisho.

3. Ana akili timamu, sio za kukopa wala za kuchanganya, ana uwezo mkubwa wa "kutrigger mental faculties" na "kureact" "contingently" kwa kuangalia hali halisi. Kwa hali hiyo ataweza kukabiliana na maswali ya aina yoyote na kuyajibu kwa unyoofu bila kusuasua wakati wa kampeni za kuwania urais.


4. Ni Kijana mwenye nguvu, "very energetic" na "mechanical", Magufuli hakaribii hata 1/4. Kwa hali hii atakimbiza kwenye mchakamchaka wa kampeni mwanzo mwisho.

5. Ana "data" mpaka "anaboa" ambazo atazitumia kuwashtaki maCCM kwa wananchi. Ana uwezo wa kufanya "derivations" zinazohusu ufisadi na udhalimu wa CCM mpaka watu "wablow"!

Badala ya kukariri data za urefu wa barabara na idadi ya dagaa ziwa Victoria kama afanyavyo Magufuli, zisizokuwa na mantiki yoyote kwa mustakabali wa nchi, yeye uwezo wake upo kwenye "kuerupt detailed logical data" na kuzitumia "kuvalidate" jambo analolisismamia.

6. Ana uwezo wa kuongea kwa sauti kubwa na inayosikika vizuri ukilinganisha na Magufuli ambaye kiswahili tu ni shida, zaidi ya kuimba nyimbo za ajabuajabu kwa kiswasukuma kama vile "mselema mselema mselema" na kauli ya "sitawaangusha wanaCCM wenzangu".

7. Kikwete mwenyewe atatetemeka sana atakaposikia Lissu anagombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA maana anamwogopa Lissu kuliko mtu mwingine yeyote hapa duniani, kama unabisha kamwuulize yeye mwenyewe. Hofu na kihoro atakachokipata Mh. Kikwete kitaambukiza wanaCCM wengine, na CHADEMA/UKAWA itakuwa imeshinda vita kabla ya kupigana. Tundu Lissu kwa Kikwete ni "Devastating". J. M. Kikwete anamwona Tundu Lissu kama jinamizi linalokaba na kutoa roho ya mtu!

8. Mtaani ninapoishi, sehemu ninapofanyia kazi zangu za kila siku, na wapenda mabadiliko wote kutoka CCM na CHADEMA/UKAWA, hata wasiokuwa na vyama wanasema Tundu Antiphas Lissu ni zaidi "SEAL Team Six" kwa CCM.
Naunga mkono hoja! Hiyo namba moja hata 2020 iko valid. Actually all of them!
 
Back
Top Bottom