CHADEMA VS ZITTO, Ufafanuzi wa Kisheria Tafadhali!

JATELO1

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,230
Reaction score
301
Wana-JF,
Naomba ufafanuzi au tafsiri wa kisheria kuhusiana na na hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu kuhusu kesi ya uanachama wa Zitto Chadema.

Mahakama imetoa amri ya pingamizi

Kamati kuu ya chadema haitajadili uanachama wake au chombo chochote hadi kesi ya msingi isikilizwe
.

Naomba ufafanuzi hasa kuhusu hiyo kesi ya msingi.

Mods, tafadhali hii post iachwe isimame bila kuunganishwa na zingine kwani maudhui yake ni tofauti. Imelenga zaidi katika kupata tafsiri za kisheria kutokana na hukumu ya leo na si mwenendo wa kesi.

Ahsanteni.
 
Zitto amekata rufaa baraza kuu la chama,kwa hiyo hadi rufaa yake itakapojadiliwa na baraza kuu... kwa hiyo chadema itaitisha mkutano wa baraza kuu la chama then rufaa yake itasikilizwa... baraza litaamua kama aendelee na vyeo vyake ama laa na pia kama aendelee kuwa mwanachama ama laa... not that much kisheria though! watakuja wenyewe ... just a chip in... nko tayari kuelimishwa.
 
Hata iweje hawezi kuendelea kuwa na vyeo vyake wale uanachama!!! Watamtema kwa aibu kubwa sana. Hafai.
 
Zitto amekata rufaa baraza kuu la chama,kwa hiyo hadi rufaa yake itakapojadiliwa na baraza kuu... kwa hiyo chadema itaitisha mkutano wa baraza kuu la chama then rufaa yake itasikilizwa... baraza litaamua kama aendelee na vyeo vyake ama laa na pia kama aendelee kuwa mwanachama ama laa... not that much kisheria though! watakuja wenyewe ... just a chip in... nko tayari kuelimishwa.

Ahsante kwa ufafanuzi. Tuchukulie kwamba uko sahihi, sasa kama Kamati kuu ndiyo ina mamlaka ya kuitisha kikao cha Baraza kuu, na Mahakama tayari imezuia suala la Zitto kuongelewa na Kamati kuu, Je Baraza Kuu itapata wapi mambo ya kujadili wakati Kamati Kuu imepokoknywa mamlaka hayo na Mahakam hivi leo?
 
Mkuu aante lakn mbona kuna taarifa humu kuwa anataka Mahakama imuamuru Katibu Mkuu ampe mwenendo wa kukao kulichomvua uongozi ili akate rufaa baraza kuu imekaaje hii sasa
 
Ahsante kwa ufafanuzi. Tuchukulie kwamba uko sahihi, sasa kama Kamati kuu ndiyo ina mamlaka ya kuitisha kikao cha Baraza kuu, na Mahakama tayari imezuia suala la Zitto kuongelewa na Kamati kuu, Je Baraza Kuu itapata wapi mambo ya kujadili wakati Kamati Kuu imepokoknywa mamlaka hayo na Mahakam hivi leo?
Kuweka jambo kwenye agenda list sio kulijadili ... katibu mkuu wa chama ataitisha kikao cha baraza kuu,agenda mojawapo ikiwa ni hiyo ila mjadala utafanyika kwenye baraza kuu... labda swali hapa ni kuwa ni lini kikao hicho kitaitishwa? na Je kuna shuruti yeyote toka huko mahakaman kuwa kikao hicho kiitishwe ? Naona yale mambo ya Rage na Simba yamehamia kwenye siasa ...
 
Ahsante Mkuu kwa ufafanuzi. Hakika ni kizungumkuti. Chezea mshahara wa Mbunge kwa kipindi cha miaka 2 na posho za PAC?
 
Chezea uenyekiti wa PAC nin! Kazi bado ipo kwa zitto, kadi yake ya uanachama imelindwa na mahakama! Ngoma bado mbichi hii..
 
Mambo sasa na huku
.7 NGAZI YA TAIFA
7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
7.7.7 Ngazi ya Taifa itakuwa na vikao vifuatavyo:-
(a) Mkutano mkuu wa Taifa
(b) Baraza Kuu
(c) Kamati Kuu
(d) Sekretarieti ya Kamati Kuu
7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama

7.7.12 Baraza Kuu la Taifa litakutana angalau mara moja kila mwaka. Vikao maalum/dharura vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.

7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.
(b) Kumchagua Katibu Mkuu miongoni mwa majina mawili yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(c) Kuwachagua manaibu katibu wakuu miongoni mwa majina mawili mawili kwa kila naibu yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(d) Kuchagua wajumbe wa nane kuingia kwenye Kamati Kuu. Kwa uwiano ufuatao:-

(i) Wanaume watatu na wanawake watatu kutoka Tanzania Bara na angalau mmoja awe mlemavu
(ii) Mwanaume na Mwanamke mmoja kutoka Tanzania Zanzibar
(e) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kutoka ngazi za chini.
(f) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya mkutano mkuu na mkuu mkutano na kuifanyia maamuzi panapostahili.
(g) Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za serikali hususani uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
(h) Kuandaa ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama .
(i) Kutunga na kuzifanyia marekebisho kanuni za kuendesha shughuli za Chama.
(j) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu.
(l) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko yake.
(m) Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa mkutano Mkuu kwa maamuzi.
(n) Kusimamia chaguzi za Chama ngazi za Jimbo/Wilaya.
(o) Kuteua wadhamini wa Chama.
(p) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
(q) Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(r) Kumwachisha ujumbe wa Baraza Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, kanuni na maadili ya Chama ama hatakidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(s) Kuthibitisha wa majimbo ya chama
 
Ninachojua mimi ni kwamba mahakama imemsaidia shinikizo lake la kutaka kamati kuu isikilize rufaa yake. Bila shaka viongozi wa chadema watakutana ili kuisikiliza rufaa yake kabla hawajafikia hatua ya kumwondoa. Kwa uhakika nilionao ni kwamba chadema watakaa na kuipitia kiaina na kuja na maamuzi yaleyale ya kumvua uanachama but be aaured kwamba zzk ataibuka na kesi nyingine. This man has a very great & intelligent mission
 
Naona maluweluwe tu hapa!
Swali langu la msingi:
1. Je zitto bado na vile vyeo alivyovuliwa?
 
Tafsiri ya hukumu kwa Lugha nyepesi ni kuwa:

Huwezi kuendelea kutoa hukumu zaidi kwa Mtuhumiwa kwa kesi ambayo ameikatia Rufaa mpaka pale utaposikiliza Rufaa yake.

Chadema wanapaswa kuitisha Baraza kuu la Chama chao ili kujadili Rufaa ya Zitto Kabwe na Pia Dkt Slaa anapaswa kumpa Nakala ya hukumu hiyo ZITTO ILI AANDAE UTETEZI WAKE.

Angalizo. Kuchelewa au kuwahi kuitishwa kwa Baraza hilo kunaweza kuathiri Pande mojawapo kulingana na Mazingira ya Sasa.
Wakichelewa kuitisha Baraza kuu ina maanisha wanatengeneza Mazingira ya kila kambi kujipanga ili kuimaliza kambi Pinzani na Matokeo yake ni Hasi kwa Chama kwani Mnyukano huo utakwenda mpaka Ngazi ya Chini kabisa ya Chama.

Wakiwahi kuitisha Haraka Baraza kuu la Chama bila ya kujua Nguvu ya Mpinzani wako inaweza ukawa ndio Mwisho wa Kambi mojawapo maana kwa hali ilivo sasa ni Ama Zitto arudi Mbowe akae Pembeni au Mbowe abaki Zitto atoke.
 
Wana-JF,
Naomba ufafanuzi au tafsiri wa kisheria kuhusiana na na hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu kuhusu kesi ya uanachama wa Zitto Chadema.

Mahakama imetoa amri ya pingamizi

Kamati kuu ya chadema haitajadili uanachama wake au chombo chochote hadi kesi ya msingi isikilizwe
.

Naomba ufafanuzi hasa kuhusu hiyo kesi ya msingi.

Mods, tafadhali hii post iachwe isimame bila kuunganishwa na zingine kwani maudhui yake ni tofauti. Imelenga zaidi katika kupata tafsiri za kisheria kutokana na hukumu ya leo na si mwenendo wa kesi.

Ahsanteni.

kesi ya msingi ilifunguliwa na zitto kwamba cc ya chadema isijadili uanachama wake hadi baraza kuu litakaposikiliza rufaa yao.

chadema kwa kuongozwa na ushauri wa tundu lissu wakapinga hiyo kesi, wakitaka mahakama iitupilie mbali.

Mahakama wanasema wanaona hoja kwenye kesi ya zitto na kwa hiyo pingamizi na tundu lissu limetupiliwa mbali na sasa mahakama itaisikiliza kesi iliyofunguliwa na zitto
 
Wana-JF,
Naomba ufafanuzi au tafsiri wa kisheria kuhusiana na na hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu kuhusu kesi ya uanachama wa Zitto Chadema.

Mahakama imetoa amri ya pingamizi

Kamati kuu ya chadema haitajadili uanachama wake au chombo chochote hadi kesi ya msingi isikilizwe
.

Naomba ufafanuzi hasa kuhusu hiyo kesi ya msingi.
Mods, tafadhali hii post iachwe isimame bila kuunganishwa na zingine kwani maudhui yake ni tofauti. Imelenga zaidi katika kupata tafsiri za kisheria kutokana na hukumu ya leo na si mwenendo wa kesi.
Ahsanteni.

BY Yericko Nyerere
Mahakama imetoa amri ya pingamizi
Kamati kuu ya chadema haitajadili uanachama wake au chombo chochote hadi kesi ya msingi isikilizwe,
KESI YA MSINGI ni kuwa rufaa yake ikasikilizwe na baraza kuu la chama
EPUKENI UPOTOSHAJI: Zitto ameshinda pingamizi lake la uanachama tu, Suala lakuvuliwa VYEO vyake vyote LIPO PALEPALE.
 
Naona maluweluwe tu hapa!
Swali langu la msingi:
1. Je zitto bado na vile vyeo alivyovuliwa?

Japo mimi si mwanasheria, Zitto ni mwanachama wa kawaida! Na si mahakama au chombo chochote nje ya chama kinachoweza kumrudishia nafasi za uongozi alizokuwa nazo! Habari ndiyo hiyo!
 
Zito Kabwe ni kirusi cha kisiasa amabye pamoja na mambo mengine kapandikiza kuzorotesha na hatimaye kumaliza upinzani nchini...stay tune!
 
Japo mimi si mwanasheria, Zitto ni mwanachama wa kawaida! Na si mahakama au chombo chochote nje ya chama kinachoweza kumrudishia nafasi za uongozi alizokuwa nazo! Habari ndiyo hiyo!

Zitto anataka Baraza kuu la Chadema kusikiliza Rufaa yake je Baraza kuu ni Chombo nje ya Chama? Jiulize Slaa na Mbowe wanaogopa nini kumpa Nakala ya hukumu na Mashtaka waliyomtuhumu ili akate Rufaa kama tARATIBU ZA cHAMA ZINAVOTAKA?
 
Mambo sasa na huku
.7 NGAZI YA TAIFA
7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
7.7.7 Ngazi ya Taifa itakuwa na vikao vifuatavyo:-
(a) Mkutano mkuu wa Taifa
(b) Baraza Kuu
(c) Kamati Kuu
(d) Sekretarieti ya Kamati Kuu
7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama

7.7.12 Baraza Kuu la Taifa litakutana angalau mara moja kila mwaka. Vikao maalum/dharura vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.

7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.
(b) Kumchagua Katibu Mkuu miongoni mwa majina mawili yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(c) Kuwachagua manaibu katibu wakuu miongoni mwa majina mawili mawili kwa kila naibu yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(d) Kuchagua wajumbe wa nane kuingia kwenye Kamati Kuu. Kwa uwiano ufuatao:-

(i) Wanaume watatu na wanawake watatu kutoka Tanzania Bara na angalau mmoja awe mlemavu
(ii) Mwanaume na Mwanamke mmoja kutoka Tanzania Zanzibar
(e) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kutoka ngazi za chini.
(f) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya mkutano mkuu na mkuu mkutano na kuifanyia maamuzi panapostahili.
(g) Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za serikali hususani uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
(h) Kuandaa ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama .
(i) Kutunga na kuzifanyia marekebisho kanuni za kuendesha shughuli za Chama.
(j) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu.
(l) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko yake.
(m) Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa mkutano Mkuu kwa maamuzi.
(n) Kusimamia chaguzi za Chama ngazi za Jimbo/Wilaya.
(o) Kuteua wadhamini wa Chama.
(p) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
(q) Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(r) Kumwachisha ujumbe wa Baraza Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, kanuni na maadili ya Chama ama hatakidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(s) Kuthibitisha wa majimbo ya chama

Ahsante sana kwa maelezo ya Katiba ya Chadema.
 
Back
Top Bottom