Mambo sasa na huku
.7 NGAZI YA TAIFA
7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
7.7.7 Ngazi ya Taifa itakuwa na vikao vifuatavyo:-
(a) Mkutano mkuu wa Taifa
(b) Baraza Kuu
(c) Kamati Kuu
(d) Sekretarieti ya Kamati Kuu
7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama
7.7.12 Baraza Kuu la Taifa litakutana angalau mara moja kila mwaka. Vikao maalum/dharura vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.
7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.
(b) Kumchagua Katibu Mkuu miongoni mwa majina mawili yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(c) Kuwachagua manaibu katibu wakuu miongoni mwa majina mawili mawili kwa kila naibu yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(d) Kuchagua wajumbe wa nane kuingia kwenye Kamati Kuu. Kwa uwiano ufuatao:-
(i) Wanaume watatu na wanawake watatu kutoka Tanzania Bara na angalau mmoja awe mlemavu
(ii) Mwanaume na Mwanamke mmoja kutoka Tanzania Zanzibar
(e) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kutoka ngazi za chini.
(f) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya mkutano mkuu na mkuu mkutano na kuifanyia maamuzi panapostahili.
(g) Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za serikali hususani uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
(h) Kuandaa ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama .
(i) Kutunga na kuzifanyia marekebisho kanuni za kuendesha shughuli za Chama.
(j) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu.
(l) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko yake.
(m) Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa mkutano Mkuu kwa maamuzi.
(n) Kusimamia chaguzi za Chama ngazi za Jimbo/Wilaya.
(o) Kuteua wadhamini wa Chama.
(p) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
(q) Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(r) Kumwachisha ujumbe wa Baraza Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, kanuni na maadili ya Chama ama hatakidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(s) Kuthibitisha wa majimbo ya chama