CHADEMA wa Mtandaoni watamwelewa lini Dr. Lwaitama?

CHADEMA wa Mtandaoni watamwelewa lini Dr. Lwaitama?

Hayupo asiyependa hoja, wote tunapenda kusikiliza na kuchangia hoja, akiwemo Dr. Lwaitama, pamoja na mimi nawe.

Lakini wakati ambao bado unaikumbuka hoja ya mwenzio ya jana, ghafla leo unaona anageuka, anaanza kuzungumza vitu tofauti na jana, hapo lazima uwe makini..

Mfano, ACT msimamo wao ulikuwa Tume Huru kwanza, sijui ni lini walibadilika kwa pamoja wakaanza kusema Katiba Mpya kwanza, sasa unapoamua kumfuata mtu wa aina hii, umakini unahitajika, anaweza kukuacha solemba muda usiotarajia..

Jambo muhimu katika siasa zenye tija yaani za kisayansi ni kutenganisha baina ya watu na hoja.

Tupende hoja za watu si watu. Vivyo hivyo tuchukue hoja zao Lakini si wao.

Tukiwa na musimamo hii hatuwezi kukwazika na watu. Kwa maana kuwa hoja fyongo tutazitupa kule Lakini si watu. Hoja kuntu tutazikumbatia Lakini si watu.

Kwa mtaji huu hoja ya mtu na mtu juzi inahusika vipi wapi?

Kwanini isiwe ruksa mtu kukengeuka ila sisi tunaangalia hoja zake zenye nashiko peke?
 
Uwepo wa mtu kwenye siasa kwa upande wangu hauna shida, tatizo langu ni kinywa kimoja na cha mtu mmoja, kuwa na ndimi mbili, hapo ndipo kuchanganyana kunapoanzia.
 
Uwepo wa mtu kwenye siasa kwa upande wangu hauna shida, tatizo langu ni kinywa kimoja na cha mtu mmoja, kuwa na ndimi mbili, hapo ndipo kuchanganyana kunapoanzia.

Kwa nini pamoja na hIzo ndimi mbili tusichague kujikita na ulimi mmoja unaotupendeza au tunaokubaliana nao?

Kwani:

1. Zitto au ACT hawana haja na katiba mpya?
2. Zitto au ACT hawamwoni CCM kama dhulumati?
3. Zitto au ACT hawatambui au kuona kuwa nchi inahitaji utawala au uongozi mbadala?
4. Zitto au ACT hawataki uwapo wa utawala wa haki?
5. Nk, nk.

Hebu jaribu kutafakari ni wapi hasa CDM na ACT wanapotofautiana?

Tofauti hIzo zinaweza kuhalalisha kutupiana mawe huku tunakokuona?

Zingatia si Zitto tu bali wote kina Slaa, Mkumbo, Kina, Ndugai, pole pole, Mpina, nk Kila tuliye wahi kutofautiana naye mahali. Asithubutu kuwa na hoja?!

Mabadiliko hayataletwa na CDM peke yake.

Prof. Lwaitama ana hoja.

Asikilizwe!
 
Si kutokea Jun tu hadi leo. Zingatia clip hii ya Dr. Lwaitama. CDM wa mitandaoni waliokaza bongo zao ni mzigo kwa chama:

View attachment 2710472

Kwa ujumla wanarudisha nyuma jitihada za ukombozi.

Lini watambue Umoja ni nguvu ndugu hao?
Hivi kushirikiana na Mnafiki kuna faida gani? ACT haipiti siku 2 bila kiongozi wake wa ngazi ya juu kuisema vibaya CHADEMA. Imefikia hatua Juma Duni anailaumu CCM kwamba wao ACT wanamtetea Mwenyekiti wa CCM kuliko CCM wenyewe. Kwamba miongoni mwa kazi halali za ACT ni kuitetea CCM na viongozi wake. Wewe uliona wapi Aina hiyo ya upinzani wa kupinga wapinzani?
 
Wenye busara wana dhihaka hii..."never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable"!!!!

Hata kukosoa kuna adabu zake....

Wengi wetu vijana tumekuwa msambweni katika hili.....

Ni kama hatujui tunapigania nini katika "mvurugiko" wa dunia ya sasa na changamoto zake.....

Safari ni ndefu sana na tunaweza KUIPUNGUZA ikiwa tutataka na kubadilika......

#SiempreJMT[emoji120]
Handsome boy CBE unamrithi Faizafoxy
 
Hivi kushirikiana na Mnafiki kuna faida gani? ACT haipiti siku 2 bila kiongozi wake wa ngazi ya juu kuisema vibaya CHADEMA. Imefikia hatua Juma Duni anailaumu CCM kwamba wao ACT wanamtetea Mwenyekiti wa CCM kuliko CCM wenyewe. Kwamba miongoni mwa kazi halali za ACT ni kuitetea CCM na viongozi wake. Wewe uliona wapi Aina hiyo ya upinzani wa kupinga wapinzani?

Kwa mawazo yako unadhani Lwaitama kapotoka kwenye kauli yake?

Unatambua kauli ya Lwaitama ni zaidi sana ya Zitto au ACT?

Nani aliyewahi kutofautiana na CDM anavumiliwa tena?

Ni Kitila Mkumbo, Slaa, Makene, Ndugai, Mpina, Pole pole, Bashiru, nk?

Kila mtu mbaya malaika watoke wapi kumbe?

Waliopotoka huwa hawarudi?
 
Back
Top Bottom