PreGE2025 CHADEMA waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ila kwa upofu wa Samia na kundi lake wanachekea chooni wakidhani wanasaidiwa, kumbe wanaharibikiwa.
Hawajui wanavyozidi kukiandama Chadema ndo wanavyozidi kukifanyq kizidi kupendwa na Watanzania.

Maana Watanzania wanashangaa inakuwaje nguvu zote zinaelekezwa Chadema kuliko hata kwenye miundombinu mibovu ya barabara na madarasa wanayosoma watoto wao?
 
No reform no election imeingia ndani ya CHADEMA hiyo kesi inata reform huko ndani chamani

Nendeni mkajibu kesi ya kutakiwa kufanya reform ya hayo CHADEMA inashtakiwa na wanachama wake
Reform gani wanataka?

Endeleeni tu kutumia kodi za Watanzania kwa masuala yenu ya kipumbavu. Na mnavyozidi kufanya huu ujinga ndo mnafanya Chadema izidi kuungwa mkono na Watanzania kila kukicha.
 
Maana Watanzania wanashangaa inakuwaje nguvu zote zinaelekezwa Chadema kuliko hata kwenye miundombinu mibovu ya barabara na madarasa wanayosoma watoto wao?
Mnaelekezana nguvu wenyewe kwa wenyewe huko CHADEMA halafu mnasingixia CCM pambaneni wenyewe kwa wenyewe kwenye ulingo wa masumbwi wa chama chenu
 
Endeleeni tu na upuuzi wenu. Kama mnaakili mngezisoma akili za watanzania na maoni yao wanayotoa sasa dhidi yenu CCM mngeachana na Chadema kabisa.

Chadema imeshafanikiwa kuingia mioyoni mwa Watanzania na wamekiona ndo chama kinachopigania mabadiliko yao kwa ukweli. Sasa nyie endeeleni na huo upumbavu wenu. Wakati ni ukuta.
 
Sema baadhi ya watanzania wewe mimi mtanzania mbona hiyo CHADEMA haijaingia moyoni mwangu
 
1: Walianza G55 wamepuuzwa
2: Imefatia kukamatwa Lissu, wanaona kesi itawashinda
3: Sasa wamekuja hawa, nao watapuuzwa

Kinachowashangaza kampeni ya NRNE inaendelea, so hizi mbwembwe zote ni za kujaribu kupunguza makali ya NRNE.

Watu wanasema Lissu ametelekezwa Rumande, (hahaha) Lissu alimwambia Heche, ww endelea na ziara, huku mahakamani hakuna inshu, jamaa limebaki na mawakili, wanachadema wako ziarani, NrNe imekolea
 
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Zanzibar, wamekiburuza mahakamani chama hicho pamoja na mambo mengine wakilalamikia upendeleo katika mgawanyo wa rasilimali za chama pamoja na stahiki nyinginezo.

Kesi hiyo ya madai namba ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, ambaye anajitambulisha kama mwanachama na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu, ambao wanajitambulisha kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.

Wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, ikiwa mdaiwa wa kwanza na Katibu Mkuu wa Chadema ni mdaiwa wa pili.

Katika kesi hiyo, wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa wadaiwa wamekiuka sheria zinazohusiana na vyama vya siasa na Katiba ya chama hicho.

Wamechukua hatua hiyo na kuomba Mahakama iamuru na kutamka hivyo wakidai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.

Pia, wanadai kuwa kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia; pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, walalamikaji hao wanaomba Mahakama hiyo itoe hukumu na amri dhidi ya wadaiwa kwamba wamekiuka kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Pia wanaiomba Mahakama hiyo itamke kwamba ugawaji wa fedha, mali na rasilimali kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kiutawala kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar unaofanywa na wadaiwa ni kinyume cha sheria na ni batili.

Vilevile wanaiomba Mahakama itamke na kuwaelekeza wadaiwa kuzingatia kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Amri nyingine wanazoomba ni kusitishwa kwa muda kwa shughuli zote za kisiasa hadi hapo kutakapokuwepo na utekelezaji wa maagizo ya Mahakama. Na wanaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio la kudumu dhidi ya matumizi ya mali, fedha na rasilimali za chama hadi wajibu maombi watakapotekeleza matakwa ya sheria husika.

Mbali na amri hizo, wanaiomba Mahakama iamuru, wadaiwa walipe gharama za kesi hiyo na itoe nafuu nyingine yoyote ambayo Mahakama itaona inafaa kuzitoa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga, itaanza leo Alhamisi, Aprili 17, 2025.
Tayari Mahakama imeshatoa wito kwa Chadema kupitia Katibu Mkuu kufika mahakamani wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Kwa mujibu wa hati ya wito ambayo Mwananchi imeiona, licha ya kukitaarifu chama hicho kuwa kesi hiyo imepangwa kutajwa leo, pia mahakama hiyo imekitaka kuwasilisha maelezo ya utetezi wake kwa maandishi.

"Pia tambua zaidi kuwa ikiwa utashindwa kuwasilisha maelezo yako ya utetezi wa maandishi kwa muda ulioainishwa, Mahakama itaendelea kesi na kutoa hukumu dhidi yako", inasomeka hati hiyo ya wito iliyosainiwa na kugongwa muhuri wa Naibu Msajili Mwandamizi.

Mwananchi

Ninamashaka Sana na IQ za sisi wabongo kiujumla ...na ndo mana nashabikia uongozi wa nusu dikteta ... Ikiwa mtu mwered atashika madaraka.
 
1: Walianza G55 wamepuuzwa
2: Imefatia kukamatwa Lissu, wanaona kesi itawashinda
3: Sasa wamekuja hawa, nao watapuuzwa

Kinachowashangaza kampeni ya NRNE inaendelea, so hizi mbwembwe zote ni za kujaribu kupunguza makali ya NRNE.

Watu wanasema Lissu ametelekezwa Rumande, (hahaha) Lissu alimwambia Heche, ww endelea na ziara, huku mahakamani hakuna inshu, jamaa limebaki na mawakili, wanachadema wako ziarani, NrNe imekolea
Chadema wako serious sana kwenye agenda yao ya kuwakomboa kweli Watanzania kutoka kwenye ufedhuli wa CCM.

Hawarudi nyuma. kweli hawa jamaa Mungu awabariki sana
 
Kaolewa na mchaga, na mwenyekiti aliyepigwa chini kwenye uchaguzi halali ni mchaga, na majority ya G55 ni watu wa kaskazini. Hapo akili kichwani!
Hiyo kesi kafungua sio yeye tu wako wazanzibari wengine hao nao utasema ni wachaga? Na ni majority
 
Mwenye kesi ni Komu, Zanzibar cdm iko ofisi tu kwa ajili ya takwa la kisheria boss. Cdm imepakwa matope kuwa nk chama cha wachaga na wakristo, hao ni wapi na wapi na wazanzibar? Kawaulize hao cdm Zanzibar wanatoa mchango gani hadi sasa wa kuendesha chama.

Ni hivi, Mbowe na wafaidika wenzake waliokuwa ndani ya cdm hawajiridhika na kupigwa chini, ndio wanaoendesha hizi hujuma dhidi ya chama. Ifahamike Mbowe na genge lake walikuwa wameshajaa kwenye mfumo wa ccm, na walikuwa wanaendesha siasa za ghiliba kuwa ni wapinzani, lakini walikuwa ni matapeli. Na ndio genge hili lililowapeleka covid 19 bunheni nyuma ya pazia. Na sasa wako na G55.
 
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Zanzibar, wamekiburuza mahakamani chama hicho pamoja na mambo mengine wakilalamikia upendeleo katika mgawanyo wa rasilimali za chama pamoja na stahiki nyinginezo.

Kesi hiyo ya madai namba ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, ambaye anajitambulisha kama mwanachama na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu, ambao wanajitambulisha kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.

Wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, ikiwa mdaiwa wa kwanza na Katibu Mkuu wa Chadema ni mdaiwa wa pili.

Katika kesi hiyo, wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa wadaiwa wamekiuka sheria zinazohusiana na vyama vya siasa na Katiba ya chama hicho.

Wamechukua hatua hiyo na kuomba Mahakama iamuru na kutamka hivyo wakidai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.

Pia, wanadai kuwa kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia; pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, walalamikaji hao wanaomba Mahakama hiyo itoe hukumu na amri dhidi ya wadaiwa kwamba wamekiuka kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Pia wanaiomba Mahakama hiyo itamke kwamba ugawaji wa fedha, mali na rasilimali kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kiutawala kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar unaofanywa na wadaiwa ni kinyume cha sheria na ni batili.

Vilevile wanaiomba Mahakama itamke na kuwaelekeza wadaiwa kuzingatia kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Amri nyingine wanazoomba ni kusitishwa kwa muda kwa shughuli zote za kisiasa hadi hapo kutakapokuwepo na utekelezaji wa maagizo ya Mahakama. Na wanaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio la kudumu dhidi ya matumizi ya mali, fedha na rasilimali za chama hadi wajibu maombi watakapotekeleza matakwa ya sheria husika.

Mbali na amri hizo, wanaiomba Mahakama iamuru, wadaiwa walipe gharama za kesi hiyo na itoe nafuu nyingine yoyote ambayo Mahakama itaona inafaa kuzitoa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga, itaanza leo Alhamisi, Aprili 17, 2025.
Tayari Mahakama imeshatoa wito kwa Chadema kupitia Katibu Mkuu kufika mahakamani wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Kwa mujibu wa hati ya wito ambayo Mwananchi imeiona, licha ya kukitaarifu chama hicho kuwa kesi hiyo imepangwa kutajwa leo, pia mahakama hiyo imekitaka kuwasilisha maelezo ya utetezi wake kwa maandishi.

"Pia tambua zaidi kuwa ikiwa utashindwa kuwasilisha maelezo yako ya utetezi wa maandishi kwa muda ulioainishwa, Mahakama itaendelea kesi na kutoa hukumu dhidi yako", inasomeka hati hiyo ya wito iliyosainiwa na kugongwa muhuri wa Naibu Msajili Mwandamizi.

Mwananchi
HUKU ZNZ SITHANI KM HUWA KUNA WENYE AKILI KM NDIO HV
 
Reform gani wanataka?

Endeleeni tu kutumia kodi za Watanzania kwa masuala yenu ya kipumbavu. Na mnavyozidi kufanya huu ujinga ndo mnafanya Chadema izidi kuungwa mkono na Watanzania kila kukicha.
Na wakumbuke watanzania hao wanaozidi kuiunga mkono Chadema ni pamoja na vijana na wazee wa wale wavaa mabaka mabaka (ambao wanaishi Lugalo, Airwing Ukonga na kwingineko) na kwa taarifa yao ccm hawa wa sasa at least wengi ni wasomi na wanaelewa mambo mengi. Hao sio Chadema hivyo wakichoka ujinga hawahutubii bali mtawakuta jumba Jeupe.
 
Back
Top Bottom