CHADEMA waelewe Katiba Mpya ni ya JMT siyo ya Tanganyika hivyo Zanzibar Wana 50% ya Maamuzi

CHADEMA waelewe Katiba Mpya ni ya JMT siyo ya Tanganyika hivyo Zanzibar Wana 50% ya Maamuzi

Sasa mbona mfano wako ni irrelevant? Watu wanazungumzia rais wa znz kuwa na say Tanganyika wewe unatolea mfano wa ruto na m7 wakati si sehemu ya JMT.
Zanzibar na Tanganyika hazijaungana katika kila Kitu ulielewe hilo

Ndio sababu mabalozi wakipokelewa nchini lazima waende kwa Rais wa SMZ kujitambulisha

Kuna maeneo fulani Dr Mwinyi na Dr Ruto wanakuwa Sawa tu!
 
Ndio ujue Rasimu Siyo Katiba

Rasimu ya Warioba ni moja tu

Baada ya hapo tuna Katiba Pendekezwa iliyoandaliwa chini ya Mtemi Chenge
  • inaitwa Rasimu ya Katiba uelewe
  • Rasimu za warioba ipo ya kwanza na ya Pili
  • Katiba pendekezwa hiyo bakini nayo kwenye maktaba zenu huko Lumumba.
 
Ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa JMT
- Wakati Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafsiri yake hadhi yake ni kama wajumbe wengine tu except Mwenyekiti wa baraza, Rais wa Zanzibar hadhi yake imedogoshwa.
 
Yaani watu wapatao 59.2Mn wa Tanzania Bara wawe sawa kimaamuzi na 1.9Mn wa kule Visiwani! Kama serikali tatu hazikubaliki kwa sasa basi ni lazima Zanzibar ikubali uwepo wa serikali moja.

Kama Tanganyika ilipoteza hadhi yake ya kutambulika kama nchi ndani ya JMT toka mwaka 1964, ni vyema sasa nayo Zanzibar ipoteze hadhi yake ya sasa ya kutambulika kama nchi ndani ya JMT, na ianze rasmi kufahamika kama mkoa wa Visiwani. La sivyo tugawane fito, na kila upande uchukue hamsini zake
- Ukiisoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, The constitutional review act imesema kura ya maoni itakuwa ni 50% Kwa Tanganyika, na 50% Kwa Zanzibar
 
Zanzibar na Tanganyika hazijaungana katika kila Kitu ulielewe hilo

Ndio sababu mabalozi wakipokelewa nchini lazima waende kwa Rais wa SMZ kujitambulisha

Kuna maeneo fulani Dr Mwinyi na Dr Ruto wanakuwa Sawa tu!

Yes kila muungano una terms zake bwashee! Kuna JMT,ZNZ na Tanganyika! Sasa Mbona tanganyika imemezwa na JMT? Why hatuna rais wa Tanganyika? Why Tanganyika haitajwi? Katiba Mpya ya Warioba imetatua hiyo mikanganyiko.
 
Yes kila muungano una terms zake bwashee! Kuna JMT,ZNZ na Tanganyika! Sasa Mbona tanganyika imemezwa na JMT? Why hatuna rais wa Tanganyika? Why Tanganyika haitajwi? Katiba Mpya ya Warioba imetatua hiyo mikanganyiko.
Nyerere Sijui hata alifikiriaje kwa niaba ya Watanganyika

Mtego aliowategea Zenji kuwameza na Serikal moja walishaushtukia baada ya ASP kuhamishiwa Ugogoni
 
Tunakumbushana tu kwa sababu Watanzania Siyo Wajinga.

Chadema haina nguvu yoyote Zanzibar na kwa sababu hiyo haina ushawishi.

Kura ya maoni kuamua Katiba Mpya Tanzania na Zanzibar zinasimama Kwenye mzani Sawa kwa asilimia za Maamuzi.

Mbwembwe zote za Tundu Antipas Lisu mwisho wake Nungwi.

Mungu ni Mwema wakati Wote!
Pia ujue ACT wana 50% ya maamuzi Zanzibar kwa hiyo ccm wasijidekeze
 
Kenya ilipata katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi. Leo wangali wanalumbana. Muulize Raila Odinga. Hakunaa uchaguzi huru na wa haki
 
Zanzibar imo kwenye katiba ya Tanzania japo haifuati yote waliyoyapitisha ndani ya katiba ya Tanzania, huu ni ujuha.
Kama Zanzibar imo ndani ya katiba ya tz,kwa nn bc iitwe nchi Hadi ifike kiwango Cha kuwa na rais?kwa kawaida tunaifahamu kwamba mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuiunda tz na sio tanzania Zanzibar!!!!!,means that Zanzibar sio nchi,ni mkoa wa pwani,na Haina hadhi ya kuwa na rais,so katiba ya Sasa inayotambua Zanzibar kama nchi,haiko sahihi hata kidogo!?!!!!! Katiba mpya iundwe ili kama Zanzibar Ina hadhi ya kuitwa nchi bc wapewe hiyo nafasi na tuitambue kama nchi nyingine barani afrika,na kama Haina bc tuitambue kama mkoa na hivyo asiwepo rais yeyote atakayeitwa wa Zanzibar,
 
Back
Top Bottom