CHADEMA waendelea na ajenda yao ya maandamano ya amani. Wapeleka barua Polisi kuomba ulinzi

CHADEMA waendelea na ajenda yao ya maandamano ya amani. Wapeleka barua Polisi kuomba ulinzi

Asante sana, kwa taarifa ni muhimu sana, inaonyesha Chadema sasa ni chama makini kinachofuata katiba, sheria taratibu na kanuni.

This is very good news and a good move, ombi kwa uongozi wa Chadema, uwe tayari kupokea majibu yao kesho, wakikataliwa wasiandamane.

P
Hakuna cha kukataliwa ni taarifa inatolewa tu. 😁😁😁 mwanasheria afu vifungu vimekupiga chenga
 
Maandamano yenu yalishapigwa Marufuku kitambo tu

Sasa barua ya nini tena?
Ni kufuata taratibu zinazo hitajika kisheria kufuatwa. Hakuna sheria inayo zuia maandamano ya amani. Sasa unataka tu kunipotezea muda kueleza kinacho eleweka na kila mtu mwenye akili timamu.
 
Familia ya Mbowe nayo itaandamana au?
Ina maana hajawahi kumuona Mbowe kwenye maandamano na mtoto wake? Usiwadanganye wananchi kuwa maandamano ni uasi wala uvunjifu wa amani na Sheria. Chadema wameandamana mara ngapi na ulishawahi kuona vurugu? Wameandamana mikoa 5. Dar, Mbeya, Arusha, Mwanza na, nimesahau mkoa mmoja
 
Ina maana hajawahi kumuona Mbowe kwenye maandamano na mtoto wake? Usiwadanganye wananchi kuwa maandamano ni uasi wala uvunjifu wa amani na Sheria. Chadema wameandamana mara ngapi na ulishawahi kuona vurugu? Wameandamana mikoa 5. Dar, Mbeya, Arusha, Mwanza na, nimesahau mkoa mmoja
Haya ya sasa ya Samia must go yamevuka red line
 
Nani ana mamlaka ya mwisho kuruhusu maandamano?

Mwenye kuomba kibali au mwenye kutoa kibali baada ya kupokea maombi.?

Mwenye mamlaka ya kutoa kibali, keshasema hayo maandamano hakuna. Na ana mamlaka ya kisheria.

Halafu kuna watu wanajifanya wao wanajua zaidi, kwa taratibu za sheria zilizo kwenye vichwa vyao.

Cheka na nyani, uvune mabua.

CDM ni chama cha fujo tu.
 
Katibu John Mnyika kaja na ujumbe huu leo jumapili, kuelekea hitima ya kesho..
FB_IMG_17269902020846250.jpg
 
Ha ha ha , wewe ulifaa kuwa waziri wa kazi na vijana maana unajua kudeal na vijana .

Ni wakati sasa Paskali uingie kwenye Serikali kuu au chukua form ya ubunge .

Haiwezekan bunge limejaza watu kama kina tale tale huku watu critical kama nyie hampo sehemu kama hiyo kutoa michango thabiti….. badala yake vijana wamegeuka kuwa machawa as a year means ya kuishi

Nataman siku moja Upate hata ubunge wa viti malum … TZ inahitaji kuwa na watu critical kama nyie kwenye sehemu nyeti
Wewe humtakii mema, mwenzako alichukuwa fomu akagombea kuteuliwa kuwa mgombeabwa ccm jimbo la kawe akaambulia kura moja, akagombea ubunge wa bunge la EA akaliwa kichwa, maccm ni mashetani.
 
Hofu yangu je wakikataliwa katiba inataka waandamane hivyo hivyo ?

Ama katiba inasema mkikataliwa muisfanye ?

Au katika inasema mkikataliwa fanyeni hivyo hivyo ?

Isijekuwa kuna gap la kisheria ambalo litaupa kila upande hoja za kuhalaljsha watakachofanya siku hiyo
Sheria inakitaka chama cha siasa kutoa taarifa angalau saa 48 kabla ya siku ya maandamano hii ni kwa mujibu wa K/F 43 (1)cha CAP 322. Kifungu 43(2) kinaruhusu kuendelea na maandalizi ya maandamano hadi utakapopata zuio la maandamano. Lakini kifungu cha 43(3) kinampa mamlaka Polisi ofisa aliyepelekewa taarifa, akifanya tathmini kuwa maandamano yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani, atajibu barua kukataza maandalizi na ufanyikaji wa maandamano.

Sasa akili ya kawaida tu, Rais ameyakataa na kuahidi taarifa, IGP amekataa na kusema yanaashiria uvunjifu wa amani kumbuka kuna kauli mbiu SAMIA MUST GO, mkuu gani wa Polisi wilaya atajichanganya kutoa baraka ya maandamano kufanyika?

K/F cha 43(6) kinamtaka mtu aliyeitisha mkutano iwapo ataona katazo la polisi hakulipenda, akate rufaa kwa waziri. Sasa CHADEMA wanataka SAMIA aondoke, MASAUNI aondoke na WAMBURA aondoke, sasa nani atakubali maandamano hayo? si kujitafutia matatizo?
 
1. Kwanza you are right
Ukitaka kuandamana toa taarifa ya maandishi polisi, sio kuomba ruhusa!.
2. Baada ya kutoa taarifa lazima usubirie kibali cha maandishi kuruhusu, kuandamana.
3. Serikali inaposhindwa kuchunguza tukio, Scotland Yard huwa wanaitwa, hivyo Chadema are right.
P
Paskal- polisi hawajashindwa kufanya uchuguzi- tumeamua tu kutowapa mda na tumewanyima ushirikiano.
Nina swali- kwa utaratibu uliopo, nani anapaswa kuwaalika Scotland Yard?

 
Back
Top Bottom