Kuna mikataba tumeingina kama Taifa ya kuheshimu haki za binadamu na utawala bora. Ndiyo maana Mwalimu alikubali kubadilisha katiba na sheria ili kuruhusu mambo haya kufanyika, alitaka twende sambamba na matakwa na kiulimwengu maana alielewa fika kwamba hutuwezi kujitenga na mataifa kwa namna yoyote ile.
Sasa kuna kikundi cha watu kinaona alichofanya mwalimu ilikuwa ni Ujinga na usaliti, sasa kimeamua kufanya kinyume chake, yaani kuturudisha nyuma kabisa wakati tulikuwa tuna sauti moja tu - ya Kiongozi wa chama akishatamka basi kauli yake ni sheria tayari..(zidumu fikra za Mwenyekiti.....)
Majority ya ulimwengu wote wanafuata mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi, ni mfumo mzuri maana kila raia wa nchi husika anapata nafasi na sehemu ya kusema dukuduku lake liwe ama kukosoa au kuishauri Serikali iliyoko madarakani.
Sasa mataifa yameamua kututenga endapo hatutaheshimu MIKATABA YA KIMATAIFA tuliyo sign kwa hiari yetu sisi wenyewe, kututenga ni pamoja na kutunyima misaada na zaidi tunaweza kushitakiwa katika mahakama hizo za kimataifa.
Sasa sidhani CDM wanahusika kwenye hili, wanaohusika hapa ni CCM ambao wamegoma kabisa kuheshimu haki za binadamu na utawala bora, wamegoma kabisa kuruhusu shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani nchini ingawa Katiba na Sheria inaruhusu, na kwa makusudi kabisa wamefanya udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huu uliopita.
Sasa adhabu itatuangukia sisi sote ingawa ni kosa la mmoja yaani CCM. Maana tunavyojua Tanzania hii bado haina uwezo wa kujitegemea kwa asilimia mia. tunakwenda kupata shida ambayo ni afadhali ya ile shida tulipata baada ya vita ya Kagera kwa wale wakongwe wenzangu mtakumbuka namna tulivyofunga mikanda.