CHADEMA wajitokeza UDOM kuwasaidia wanafunzi wasio na mkopo mpaka sasa

CHADEMA wajitokeza UDOM kuwasaidia wanafunzi wasio na mkopo mpaka sasa

Kama kweli CDM wameamua kuwasaidia wanachuo wa UDOM, Wasiingiliwe na Magambazi.

Kuna taarifa kwamba walioandikishwa majina wanatafutwa watimuliwe chuo. HII NI HAKI?
 
Wanabodi ni juzi tu CDM imetangaza kutaka kuwasaidia wanachuo wote wa UDOM ambao tangu chuo kifunguliwe october hawajapata fedha zao.

Kuonyesha kwamba Menejimenti ya Udom kuna ubabaishaji, leo wamebandika zaidi ya majina 50, miongoni mwa ambao hawakupata Mkopo kwamba wasaini leo na kuingziwa fedha zao haraka.

SWALI: Walikuwa wapi kuwapa fedha zao kabla ya CDM?

Hao wengne hatima yao nini?

Au ni Maagizo kutoka white house/NEC?

Udom ni aibu kubwa kwa Jk na wenzake, ambao badala ya kufika kujionea adha na uodho wa Udom, wameishia kupigiana simu na akina Kikula na Mlacha na kuelekezwa Udom kukoshwali wakati hali siyo hivyo.
 
Wanabodi wa jf

Katika hali ambayo CHADEMA wamefanya la maana Mpango wao wa kutaka kubeba zigo la serikali kuwapatia wanafunzi pesa ya kujikimu.

Kiongozi mmoja ambaye pia ni Mbunge wa CHADEMA jana alisema anaenda Dsm na watahakikisha wanaanda mpango wa haraka kuwaokoa Wanachuo hao ambao serikali ya CCM Imewakacha.

Amesema wanachuo ambao mpaka sasa hawajapata fedha zao wanaishi maisha ya dhiki na anasa.

Hata hivyo taarifa za ndani za wanafunzi chuoni hapo zinasema hata baadhi ya Makada hawajapa mkopo, Waliotajwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Chunya Sauli Mwaisenye na Katibu wa CCM UDOM NA MJUMBE WA UVCCM TAIFA, Elius Ndabila.

Hata hivyo walivyopigiwa simu Kuulizwa suala hilo Ndabila alisema nenda bodi utapata taarifa.

Mpango huo wa CHADEMA Unaratibiwa na Wabunge wake na wamesema watawasaidia wanafunzi bila kujali rangi, dini wala itikadi. Wamesema hawana uwezo wa kuwapa fedha ya kuwaridhisha kama Bodi badala yake kuwapunguzia ukali wa maisha.

NAWASILISHA.

Watu wa UDOM ni kweli hizi pesa zilitolewa na CDM?
 
hizi ni kelele za kisiasa tu kaka window7 tuwasubiri waje watoe ukweli.
 
Siasa na elimu wapi na wapi?tutafute njia za kuwasaidia waliokosa mkopo na si kuhusisha siasa,tuwe great thinkers,tujaribu kufahamu kuwa siasa ni propaganda,zenye ukweli %15,uchochezi %25 na uongo %60,kamwe tusiwape wanasiasa nafasi ya kuwatumia wasomi wetu,ya serikali iachiwe serkali
 
umeona sasa hii wenje anawakataa wapiga kura wake ili hali wana CCM wanaamini ngome kubwa ya upinzani wao ipo nyegezi na ndiyo ilimfanya mr masha kuachia kiti na hasa SAUT leo hii anawakana kusemea tu kuwa jamani vip katika jamii wahusika wakasikia

kwani ni chuo cha wenje
 
hizi ni kelele za kisiasa tu kaka window7 tuwasubiri waje watoe ukweli.

Ndio maana Tunataka uthibitisho wanasiasa wanatudanganya sana nchi hii. Hasa kwenye matatizo wao huyatumia kushawishi watu kuwachagua badala yakutatua
 
Wanabodi wa jf

Katika hali ambayo CHADEMA wamefanya la maana Mpango wao wa kutaka kubeba zigo la serikali kuwapatia wanafunzi pesa ya kujikimu.

Kiongozi mmoja ambaye pia ni Mbunge wa CHADEMA jana alisema anaenda Dsm na watahakikisha wanaanda mpango wa haraka kuwaokoa Wanachuo hao ambao serikali ya CCM Imewakacha.

Amesema wanachuo ambao mpaka sasa hawajapata fedha zao wanaishi maisha ya dhiki na anasa.

Hata hivyo taarifa za ndani za wanafunzi chuoni hapo zinasema hata baadhi ya Makada hawajapa mkopo, Waliotajwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Chunya Sauli Mwaisenye na Katibu wa CCM UDOM NA MJUMBE WA UVCCM TAIFA, Elius Ndabila.

Hata hivyo walivyopigiwa simu Kuulizwa suala hilo Ndabila alisema nenda bodi utapata taarifa.

Mpango huo wa CHADEMA Unaratibiwa na Wabunge wake na wamesema watawasaidia wanafunzi bila kujali rangi, dini wala itikadi. Wamesema hawana uwezo wa kuwapa fedha ya kuwaridhisha kama Bodi badala yake kuwapunguzia ukali wa maisha.

NAWASILISHA.
sasa mtu anaishi vipi maisha ya dhiki na anasa kwa wakati mmoja?
 
Back
Top Bottom