Chinga:
Nimekusoma mara nyingi ukinisingizia mimi kuwa ni Asha Abdala na kuniporomoshea matusi. Una haki kabisa ya kunichukia na hata kunitukana kwa sababu zozote zile ulizo nazo, lakini kwa kweli huna haki ya kunizushia mambo. Niliamua ku-ignore posts zako za kunisingizia mimi kuwa ni Asha Abdala. Lakini naona unaendelea na uongo ukiendelea kusemwa na kurudiwa mara kwa mara hujenga taswira ya ukweli. Sasa natamka hapa kwa nia ya kuweka record kuwa mimi sio Asha Abdala. Asha pia ameshajibu mara kadhaa hapa kuwa yeye sio Kitila Mkumbo, lakini kwa sababu unazozijua wewe unaendelea.
Kwa vyovyote vile, sina uwezo wa kukufanya uache kufikiri na kuamini kile ambacho wewe umeamua kufikiri na kuamini. Lakini kwa watu wanaofuatilia maandishi ya watu hapa wanajua tofauti ya wazi iliyopo kati ya maandishi yangu na ya Asha.
Siwezi kumaliza post hii bila kutoa malalamiko yangu ya dhati kabisa kwa administrator na moderators wa JF. Naamini kazi za administrator na moderators ni pamoja na kulinda haki na hadhi ya members hapa. Ninasikitishwa sana na kitendo chenu cha kukaa kimya huku mkiona baadhi ya members wenu wakishushiwa hadhi na kuchafuliwa utu wao kwa kila aina ya matusi na kusingiziwa mambo ambayo nyie kama watunza kumbukumbu zetu mnajua kabisa kwamba sio kweli. Nyie mnajua kabisa ukweli wote kwamba mimi sio Asha Abdala na ninaamini pia Mwanakijiji sio Mwafrika wa Kike wala Bi Senti, lakini, kwa sababu mnazozijua nyie, mmekaa kimya huku Chinga akiendelea na uongo na matusi yake kama vile yeye yupo juu ya taratibu tulizoziwekea hapa na tukakubaliana wote kama members. Ninaamini hii si sawa.
KM
Chinga aliwahi kusema kuwa wewe ni mwanasiasa na unasoma mji wa UK, ulikatusha sana kipindi hicho unatumia Mwanasiasa na ukasema kuwa nani kasema unasoma UK, lakini baadaye imejulikana ni kweli.
Senti50 kasema mimi na maslahi binafsi toka kwa JK na kuna sehemu kasema kuwa Mswahili ni godoro la JK na jana kasema mimi ni Chinga, Mtalii na Mswahili,nilitegemea na hili uwafahamishe Ma moderators au kwa vile sisi wengine hatuchangii Chadema?
mie sijaona tusi ulilotukanwa na Chinga labda umetumwa na Mwanakijiji ili umlinde na tabia yake ya kutumia majina mengi kama yalivyotajwa humu.
Asha Abdallah kasema Kubwajinga ni Chinga na Mugongo hilo hujalitolea maelekezo.
Nashindwa kukusoma unaposema kuwa Mwanakijiji sio Mwafrika wa kike jee wewe ni moderator humu? au kwa vile ni mwanachadema unamsaidia.
wiki iliyopita kulikuja na habari ya wewe kukamatwa ililetwa na Brazameni akaja ES akasema kuwa huyo jamaa ni member mkubwa JF na anatumia jina maarufu sana, bwana Kitila hukujibu hoja hiyo lakini hili la Mwanakijiji limekuuma sana.
mimi nilifungiwa for the whole week last week kwa kujibizana na senti 50 lakini moderator hawakumfungia senti 50 na wewe hukuja kunitetea. leo hii Chinga kusema maneno kwa mwanakijiji ambayo si matusi kama anayotoa Senti 50 kwa rais wetu na RO na members wengine humu na kuna dada yuko Foreign anamtukana sana wewe umekaa kimya tena tunakutegemea kama Msomi na mwanaharakati.
Kwako wewe Mwanakijiji ni bora kuliko rais wetu.
Asante bwana mkubwa tumekusoma. umgekuwa na maana japo kumtetea Brazameni kwa kuonesha mapenzi kwako. kumbe kwako kuwa Mwanachadema ni bora zaidi.