PostGE2025 CHADEMA walitoa sadaka ya kujimaliza Oktoba 29, hawainuki tena

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Chadema walipanga mauaji ya vijana, hata Lissu alisema hivyo wakati anatangaza kukinunisha siku ya uchaguzi. Au nikuwekee clip yake kuthibitisha hilo?
Kwa hiyo mpaka hayo maandamano na vurugu zilipotokea, huyo Lissu alikuwa wapi?

Inakuwaje watu wazima mnaongea hadharani mambo ya kitoto na yasiyo na ushahidi usio na shaka? Hizo hela hao vijana walipewa mikononi, waliingiziwa kwenye akaunti, au walizipata kwa utaratibu upi?

Halafu hizi porojo hata yule bosi wako muuaji aliwahi kuzitoa hadharani, na watu wenye akili timamu tulibakia tu kumshangaa.
 
Bado unawaza zile hekaya za Abunuas. Lissu aliposema watakinukisha sana wewe ulikuwa unadhani watajamba sana hadi nchi yote inuke ushuzi? acha utoto kaka. Jamaa walikuwa na mipango mikubwa lakini ya kitoto/miscalculated. Yaani mipango ime backfire. Mipango sio matumizi, wakapange upya.
 
Unadhani no reforms no election ilishiishia wapi na iliisha vipi? Tunza heshima yako kaka.
 
Inasikitisha sana watu wamepigwa risasi hadi majumbani halafu linakuja zezeta moja kusema CHADEMA ndio waliua watu .
Kwani ile mitungi ya gesi waliyobeba waandamaji hawakuipeleka majumbani kwao kupikia? Kwahiyo kama ukichoma kituo cha polisi na kukimbilia getoni kwako basi umesalimika, hawakufuate tena. Una maana hiyo? Hebu wewe taja idadi ya vituo vya polisi, vituo vya mwendokasi, ATM na ofisi za serikali zilizochomwa moto na wahuni hawa.

Hata NUTA Jazz band chini ya Muhidini Gurumo waliwahi kuimba wimbo wa Mwana acha wizi. "........uliiba duka la ushirikaa bunduki ikalia shaba ikaingia mwilini mwako mwangu umefungwa, hospitali umelazwa na pingu zako........." Hapo aliimba wimbo huo miaka ya 1970s. Ukiiba na kuharibu mali ya umma shaba itakuhusu. A rule of thumb.
 
Wiki tatu kabla ya uchafuzi na hadaa yenu, mlihakikisha mmewakamata viongozi wote waandamizi wa Chadema mkawaweka ndani,

Lissu hadi leo anaozea jela tangu April mwaka jana 2025.

Mahakama imepiga marufuku mikutano yao.

Halafu Chadema ipi iliyoandaa hayo maandamano.

Ona aibu hata kama ni mijnga usikubali kuwa mpumbavu.
 
Wewe mjinga, adhabu ya mtu anayeiba mitungi ya gesi au kuvamia na kuharibu ATM ni kupigwa risasi hadi kuuwawa?

Upo uthibitisho wa watu kupigwa risasi wakiwa nyumbani kama Sheikh Sharif Majini , Master Tindwa,yule mama wa Arusha na wale waliokuwa wanaangalia ligi ya Uingereza kwenye kumbi, je hao na wengine wengi walikua wameiba mitungi ya gesi au kwenye ATM?

Ujinga ni mzigo.
Wewe mjinga nakuuliza tena , kazi ya risasi za mpira huijui?

Hujui kuna tofauti ya rubber bullet na live bullet na zote zina kazi zake?

Kama mmepitisha adhabu ya wezi wote ni kuuwawa kwa kupigwa risasi tupeni ratiba ya kupiga risasi majizi yaliyotajwa kwenye kashfa kama EPA, ESCROW, Meremeta, Richmond, Kagoda na huu ubadhrifu kwenye mradi wa treni ya umeme.
 
Ndugu sisi ni watanzania na tanzania ni yakwetu sote. Lissu alishirikiana na watu wenye maslahi binafsi kumuondoa Mama ambae hana hatia. Alipeperushwa tu na upepo wa Katiba yetu ya 1977 kuwa Rais wa nchi baada ya Rais wetu JPM kufa. Wanaompinga Samia walimpinga hata kabla ya kuapishwa kuwa Rais. Hawampingi kwasababu anaongoza vibaya bali hawamtaki tu kwakuwa maslahi yao hayatatimia kama Rais atakuwa ni Samia au Mbowe. Lazima Rais angekuwa mtu kama Lissu.
 
Yaani wewe hamnazo kabisa, yaani mhalifu anatumia risasi za moto kuua polisi halafu unataka polisi wao watumie risasi za mipira, kwenda zako. Nguvu sahihi ilitumika sehemu sahihi.
 
Yaani wewe hamnazo kabisa, yaani mhalifu anatumia risasi za moto kuua polisi halafu unataka polisi wao watumie risasi za mipira, kwenda zako. Nguvu sahihi ilitumika sehemu sahihi.
Wewe zezeta ,hivi polisi si wana kauli yao kwamba watu wasichukue sheria mkononi?

Niambie wapi katika sheria imeruhusiwa polisi kuua mwizi?

Nakuuliza tena Master Tindwa na Sheikh Sharif Majini waliopigwa risasi waliiba mitungi ya gesi?

Juzi nilikuwekea hapa picha ya maiti za watu Mwananyamala ukasema kule ni Darfur, nikaweka na video ya maiti kule Arusha kuna shuka za MSD je wale wote waliopigwa risasi ni wezi?

Sheria ipi inasema wezi adhabu yao ni kupigwa risasi?

Kama ipo basi na majizi na mafisadi yaliyopo CCM huko mseme lini yanapigwa risasi .

Yale majizi ya policcm yaliyoiba muda kanisa la Gwajima limefungwa yanapigwa risasi lini?

Yale majizi ya policcm yaliyoiba safe za pesa walipomteka Polepole yanapigwa risasi lini?

Hawa watu wanavyopigwa hapa na polisi muda mmezima internet ulifikiri hamtokuja kujulikana?

Yaani mtu hana silaha mmemvunja miguu bado mmampiga watu zaidi ya watano.

Your browser is not able to display this video.

 
Risasi za mpira zinatumika kuzuia maandamano ya wanafunzi wanaopinga kula ugali maharage shuleni kila siku, sio kwa wanaotaka kuipindua serikali; umerogwa nini wewe?

Hali ya hewa inaveza kuruga miundombinu na makazi kwenye taifa lolote lile duniani. Moto na vimbunga viliweza kuunguza miundombinu na makazi kule Los Angles na California, Japan, Ufaransa sembuse Tanzania. Wewe unaposikia watu wakisema juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani unadhani wanaongelea kuhusu babu na bibi yako walioana lini?

Hata hivyo maneno yenu yanaisaidia kuifanya serikali isilale katika kutimiza majukumu yake kwa wananchi. Hata Nyerere alipigania kuwepo kwa vyama vingi nchini kwaajili ya kukipasha joto CCM isigande.
 
Kupitia mitandao ya kijamii leo tarehe 8 Januari 2026, Mbowe amesema anatambua kuwa hatua yake imewaumiza wengi, hasa waliomlea kisiasa ndani ya Chadema, na hivyo kutumia nafasi hiyo kuomba radhi hadharani.

Mbowe amesema kuwa Chadema ni chama chenye nafasi ya kipekee katika maisha yake ya kisiasa na kwamba anaendelea kukiheshimu licha ya kuondoka kwake.
 
Risasi za mpira zinatumika kuzuia maandamano ya wanafunzi wanaopinga kula ugali maharage shuleni kila siku, sio kwa wanaotaka kuipindua serikali; umerogwa nini wewe?
Kwahiyo wale walioandamana walikuwa na silaha za moto hadi polisi warushe live bullets?

Nijibu swali langu usitake kuhamisha mada, nipe kifungu cha sheria kinachosema adhabu ya mwizi ni kupigwa risasi.
Wewe tangu mwanzo nimesema ni zezeta na unathibitisha hili , hapa masuala ya hali ya hewa yanahusiana vipi na hii mada?

Mimi sizungumzii hali ya hewa kuharibu miundombinu ya reli kutokana na mvua , bali ubadhirifu wa kifedha na kujenga mradi chini ya kiwango ambao ni hatarishi kwa wasafiri mvua imekuja tu kuwaumbua mlichokijenga chini ya viwango.

Ulivyo zezeta na picha nimeweka hasara ya matrilioni ya pesa ila wewe umechagua kichaka cha mvua kujificha.

Halafu utetezi wako kwenye mambo ya hali hewa unataja ulaya na marekani mbona katika demokrasia huwa hamtolei mifano huko?
Hata hivyo maneno yenu yanaisaidia kuifanya serikali isilale katika kutimiza majukumu yake kwa wananchi. Hata Nyerere alipigania kuwepo kwa vyama vingi nchini kwaajili ya kukipasha joto CCM isigande.
Nieleze lini mafisadi na majizi ya EPA,ESCROW, Kagoda, Meremeta, Richmond, na majuzi hapa mradi wa reli ya umeme yatapigwa risasi kutokana na wizi.

Na majizi ya policcm yaliyoiba kwenye kanisa la Gwajima yalipokua yanalinda miezi 6 lini ni tarehe yao ya kupigwa risasi kwa wizi walioutekeleza.
 
Wewe kwa akili yako chadema iko hai?
Kapa ilikufa mliogopa kunini kuweka reforms mkaona cha moto?

Mbona mlikimbilia Mahakamani kumfunga Lissu?

Mbona mlikimbilia Mahakamani kukataa mikutano ya Chadema kipindi cha no reforms no election campaign?
 
Kwani Chadema ndo walipanga maandamano au Gen Z?

Mbona mlikimbilia kuweka Jwtz Barbarani ?Msingefunga Barbara Kwa mitutu mkaona
 
Acha ife inakuhusu nini, mtego wenu wa kutaka Chadema kishiriki kwenye dhambi , chadema ikwa mbele ya mda ,sasa roho zawauma , mmezibeba wenyewe
 
Acha porojo! Wataje hao wahusika wa CHADEMA waljishiriki kwenye kuandaa hayo maandamano ya tarehe 29 Oktoba. Porojo za kusema "Lissu alisema" sijui nini! Haina mashiko. Kwa sababu tangu April mlikuwa mnamshikilia kwa kesi yenu ya mchongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…