Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28
Na Elius Ndabila
Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lissu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu.
Kwa ufupi huwezi kuhalalisha uwingi wa watu waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza TUNDU ANTIPAS MUGWHAI LISSU kuwa unampatia uhalali kushinda Mh Sugu. Mkutano wa jana ulikuwa ni mkutano wa Mgombea Urais na si Mgombea Ubunge. Uwingi wa watu waliohudhuria jana tutaushindanisha na Uwingi wa watu watakaohudhuria mkutano wa JPM MBEYA. Hii itatupatia Matokeo ya Jumla kuwa nani ameujaza uwanja wa Ruanda Nzovwe. Hata hivyo historia inaonyesha Mkutano wa Lisu watu walijitokeza wachache ukilinganisha na idadi ya watu ambao waliwahi kukusanyika kipindi cha Mh Slaa na baadaye Mh Lowassa.
Mkutano atakao fanya Mh Sugu huo utakuwa mkutano wa Mbunge na utatupa mizani ya kupima stamina yake na mkutano atakao fanya Dkt Tulia atakapokuwa akizindua kampeni zake tr 12. Mkutano wa jana hauhusiki na kukubalika kwa Sugu Mbeya, bali ni mkutano ulioenda kushuhudia muujiza unaotembea(CHADEMA wanasema hivyo).
Mh Dkt Tulia ambaye anabeba bendera ya CCM, kwanza yeye mwenyewe yupo vizuri kupambana na Sugu, lakini pia CCM imepania kushinda baada ya kubaini mambo kadhaa yaliyosababishwa kushindwa mihura miwili.
Ninauhakika JPM akija Mbeya ataujaza uwanja zaidi ya mara mbili ya wafuasi wa siasa waliompokea Tundu Lisu jana. Uwingi huu utachagizwa na kazi kubwa ambazo JPM amezifanya na ambazo zinampatia uhalali wa kushinda tena OCTOBER 28.