Uchaguzi 2020 CHADEMA wamedhibitiwa mkoa wa Mbeya

Uchaguzi 2020 CHADEMA wamedhibitiwa mkoa wa Mbeya

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28

Na Elius Ndabila

Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lissu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu.

Kwa ufupi huwezi kuhalalisha uwingi wa watu waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza TUNDU ANTIPAS MUGWHAI LISSU kuwa unampatia uhalali kushinda Mh Sugu. Mkutano wa jana ulikuwa ni mkutano wa Mgombea Urais na si Mgombea Ubunge. Uwingi wa watu waliohudhuria jana tutaushindanisha na Uwingi wa watu watakaohudhuria mkutano wa JPM MBEYA. Hii itatupatia Matokeo ya Jumla kuwa nani ameujaza uwanja wa Ruanda Nzovwe. Hata hivyo historia inaonyesha Mkutano wa Lisu watu walijitokeza wachache ukilinganisha na idadi ya watu ambao waliwahi kukusanyika kipindi cha Mh Slaa na baadaye Mh Lowassa.

Mkutano atakao fanya Mh Sugu huo utakuwa mkutano wa Mbunge na utatupa mizani ya kupima stamina yake na mkutano atakao fanya Dkt Tulia atakapokuwa akizindua kampeni zake tr 12. Mkutano wa jana hauhusiki na kukubalika kwa Sugu Mbeya, bali ni mkutano ulioenda kushuhudia muujiza unaotembea(CHADEMA wanasema hivyo).

Mh Dkt Tulia ambaye anabeba bendera ya CCM, kwanza yeye mwenyewe yupo vizuri kupambana na Sugu, lakini pia CCM imepania kushinda baada ya kubaini mambo kadhaa yaliyosababishwa kushindwa mihura miwili.

Ninauhakika JPM akija Mbeya ataujaza uwanja zaidi ya mara mbili ya wafuasi wa siasa waliompokea Tundu Lisu jana. Uwingi huu utachagizwa na kazi kubwa ambazo JPM amezifanya na ambazo zinampatia uhalali wa kushinda tena OCTOBER 28.
 
Mkuu mbona hata hueleweki Maana kichwa Cha Uzi kipo tofauti na content ya Uzi wako, nilitegemea uanze kushusha madini ya namna gani chadema wamedhibitiwa Jijini Mbeya, wewe unakuja na swaga za kizamani kabisa za kulinganisha idadi ya Watu.

Sasa Basi itoshe tu kusema Uzi wako hauna Maana Tena .
 
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28.

Na Elius Ndabila

Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lisu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu...
At the same time anahalalisha wingi wa watu wanaosombwa na malori kwenda kwenye mikutano ya mgombea wetu kuwa atashinda kwa kishindo.Pathetic
 
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28.

Na Elius Ndabila

Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lisu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu...
Bila bao la mkono ccm haishindi.
 
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28.

Na Elius Ndabila

Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lisu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu..
Mbona sasa hujatoa hizo Hoja zenye utafiti baada ya Introduction uliyoanza? Au tusubiri kidogo mkuu?
 
NGUVU YA CHADEMA HAIPO TENA MBEYA, WATAPIGWA OCTOBER 28.

Na Elius Ndabila

Kuna watu jana baada ya Mh Tundu Lisu kufanya mkutano wake jijini Mbeya wamekuja na kauli kuwa Mbeya mjini ni ya CHADEMA. Bahati mbaya wamefanya utafiti ambao kisiasa ni inlogic. Kabla sijatoa hoja madhubuti ya kupinga tafiti hizi feki, ninaomba niwaeleze kuwa Mbeya mwaka huu CCM itashinda kwa kuwa mipango yao ilianza muda mrefu...
Mama maria jana katuambia kuwa mnalazimisha watu kuja kwenye mikutano yenu ili kujaa uwanja.
 
Kazi mnayo mwaka huu, hao waliohudhuria mkutano wa Lissu ndio wapiga kura wa Sugu, jiandae kuimeza hiyo Chloroquine ni chungu lakini ndio dawa.
 
Na nyie nendeni mkafanye mkutano mbeya bila wasanii muone namna halisi mnavyokubalika, kutumia wasanii ni hadaa tu!.

Bila wasanii ndio itakuwa kipimo cha haki.
 
Mimi nmepita jana pale mikutano yote ya Dr Slaa na Lowassa nilikuwepo lakini jana watu hawakuwepo kama mkutano iliyopita nahisi hata yeye sugu kashtuka Tulia anashinda Mbeya mapema kabisa
 
Kamati ya kampeni za Chadema kama haipo vizuri hivi

1) Tundu Lisu anaendaje kufanya kampeni Mbeya mapema hivi hata wabunge bado hawajazindua kampeni zao

2) Maeneo ambayo ni potential kwa Chadema ili takiwa aende wakati kampeni zimepamba moto yani kati ya mda wa kampeni au mwishoni lakini cha ajabu yeye ndio anapita sasa hivi kama mvua

3) Tundu Lisu anatakiwa atumie gali kuzunguka Tanzania mzima katika kampeni zake sio ndege

Dahhh! Chadema sijui mnakwama wapi
 
Back
Top Bottom