SI KWELI CHADEMA wameshindwa kusimamia kikao cha wazee kutokana na ukosefu wa pesa

SI KWELI CHADEMA wameshindwa kusimamia kikao cha wazee kutokana na ukosefu wa pesa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
photo_2025-10-07_16-32-26.jpg
photo_2025-10-07_16-32-33.jpg
photo_2025-10-07_16-32-39.jpg
 
Tunachokijua
Kila Oktoba Mosi ya kila mwaka hufanyika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yakiwa na lengo la kutambua mchango wa wazee, kuhamasisha heshima na huduma bora, huku kaulimbiu ya mwaka 2025 ikiwa ni "Wazee Kuendesha Hatua za Kijamii na za Kimataifa: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu."

Aidha Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kuanzia Septemba 28 kilitoa taarifa ya kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya wazee duniani, kidigitali. Rejea hapa, hapa na hapa.


Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambawa mtandaoni kuwa CHADEMA ilitoa taarifa ya kuaihirisha maadhimisho hayo kwa sababu ya kushindwa kusimamia kikao cha wazee kutokana na ukosefu wa pesa.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani CHADEMA ilifanya maadhimisho hayo kama ilivyotaarifiwa awali.

Aidha taarifa iliyodaiwa kutolewa na chama hicho ni ya kughushi kwani haikuchapishwa katika kurasa rasmi za chama, vilevile inayo mapungufu kama vile fonti isiyotumiwa na chama hicho, makosa katika tarehe kwani mwezi Septemba unaishia tarehe 30.

Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kutengenezwa na wapotoshaji kwani hazijachapishwa na vyombo hivyo (Mwananchi na Jambo TV) kama inavyoonekana. Kadhalika matumizi ya fonti zisizotumiwa na vyombo hivyo ni mapungufu yanayodhihirisha kuwa grafiki hizo ni za kughushi.​
Back
Top Bottom