CHADEMA Wamkanya Mwakyembe!

CHADEMA Wamkanya Mwakyembe!

.

Wewe ndiye Umefulia na Upeo wako mdogo.
Kama unaona Halmshauri za wilaya zinafanya kazi za mbunge,basi hakuna haja ya kuwa na mbunge.

Mwakyembe anatakiwa kuwa mbunge wa Kawe kwani muda wote yuko Dar kwake kunduchi.

Na Mwakalinga anatakiwa kuwa mbunge wa wapi - Poraandi?
 
Sikilizeni, Hakuna kosa kumsaidia Mwakyembe kuhusu udhaifu wake.

Hawa ndugu ni watu wema sana kwa Dr.

Ni kweli kuwa hakuna haja ya yeye kuwa na malumbano ya mara kwa mara na akina nani sijui. Yeye ni mbunge wa sasa na anatakiwa afanye kile aliahidi kuwafanyia wana Kyela.

Kama alifanya usanii kama wa mwenyekiti wake JK kwa kuahidi hewa, atayalishe uongo mwingine mkali zaidi maana wadanganyika wewe njoo na uongo mpya kila election watakubali tu, tena hata ukiwadanganya kuwa nimeshafanya niliyoahidi hata kama ujafanya watakenua meno kidogo na kisha watakupa kura tena.

Lakini hii ya kulumbana kwenye vyombo vya habari na akina Mtanzania na Engineer ni ku expose udhaifu alio nao, na hii inaweza kuja mgharimu sana next year.
 
Engineer alipowaambieni juu ya habari hii mkadai majungu, sasa wameandika Tanzania Daima labda ndio mtaamini.

Mkuu Engineer, lete zingine za huku Konyumba!

Vijana wa Ipinda nasikia wanamwambia mbunge kafulia?

Bambumbile,

Achana na hawa vijana wa Dar ambao hata hawaijui Kyela. Mimi nitaendelea kuwahabarisha tu. Mwanakatwe na NIPASHE mbona hajaandika? Au hawakujua CHADEMA watakuwa Kyela?

Dr. Mwakyembe sasa anaongoza kufungua matawi ya CCM. Toka mwaka huu uanze kafungua zaidi ya kumi wakati huko nyuma hakufungua hata moja.

Huu muda si angetumia kukaa na watu kujenga shule? Kuimarisha huduma ya afya?

Juzi kafungua tawi la mbugani na hakukuwa na watu kabisa. Mimi siamini huyu jamaa hata ana washauri, labda ni hawa wa JF.

Huku umeme unasumbua sana.
 
.

Wewe ndiye Umefulia na Upeo wako mdogo.
Kama unaona Halmshauri za wilaya zinafanya kazi za mbunge,basi hakuna haja ya kuwa na mbunge.

Mwakyembe anatakiwa kuwa mbunge wa Kawe kwani muda wote yuko Dar kwake kunduchi.
lete hoja, hapa hapana hoja yoyote. jaribu tena. labda unatoa mapendekezo. bado hujatushawishi kuwa mwakyembe hafai kuwa mbunge kyela.
 
Back
Top Bottom