NAPENDA KUTOA RAI
Mnajua wengine tumekimbia vijiwe vya siasa, kukataa mambo kama haya!!!
kwamba mimi ni chadema/ccm/cuf/tlp/ (sijui na vingine vinaitwaje) lolote linaloashiria maslahi kwa chama changu (sometimes hata kama lina athari kwa taifa) basi nami naunga mkono tu. Na kama hoja haiungwi nkono na chama changu au haina maslai kwetu basi huo ni uzushi, fitna, ufisadi, wizi nk nk. Huwa hatusutwi na nafsi zetu na hata bila woga mara nyingi tunatumia uongo, kupandikiza chuki, nk ili muradi kutimiza azma zetu hizo.
Mara nyingi ukisoma mijadala ya kisisasa humu JF unaona kabisa kuwa hata wale ambao wamekuwa msitari wa mbele kuelimisha kwa busara na hekima umuhimu wa uzalendo huwa wananasa katika mtego wa SISI TUKO SAHIHI, WAO LA HASHA!!! Mbaya zaidi mijadala mingi ambayo mingi inahusu mambo nyeti ya taifa huishia ama kwa malumbano ya ushindani wa kivyama au mara nyingine hata mada hubadilika kabisa. Inasikitisha kuwa haya yanafanyika humu humu jamboforum na baadhi yetu bila kutanguliza manufaa kwa taifa kwanza.
Kama Mzee mkjj ni CHADEMA hiyo ni stahili yake, KADA nae kama ni CCM hiyo pia ni stahili yake. Hawa wote nawaheshimu sana, sio kama wao bali kwa mchango wao mkubwa humu Jambo forum. Kitu ambacho nawakumbusha kuwa si stahili yao ni pale watapoweka uchama wao mbele ya Utanzania wao kama (kwa mfano mmoja tu kati ya mingi)vile anavyofanya mwafrika wa kike!! Si dhambi kuwa na chama, si dhambi kutetea chama chako, si dhambi pia kunadi sera za chama chako humu JF. Kosa ni pale unapotumia Bites za JF kupost uovu kwa taifa tu kwakuwa unataka kukiweka chama chako vizuri mbele ya wapiga kura.(pengine hapa mkitaka kunielewa vizuri basi angalia tofauti kati ya Mnyika na M/Kike)
Niliwahi kusema kuwa YAWEZEKANA SIKU MOJA UKAWA SI CCM/CHADEMA TENA ILA HAIWEZEKANI UKAWA SI MTANZANIA. HATA UKIUKANA URAIA, DAMU YAKO SIKU ZOTE ITABAKIA KUWA YA-BONGO TU!
Tuache ushabiki tujadili mambo!!!!!!! Utaifa mbele!!!
NAPENDA KUWAKILISHA RAI