Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
na Asha Bani, Same
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliongoza Operesheni Sangara katika Jimbo la Same Mashariki kwa kumrushia makombora mazito mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela (CCM).
Wakizungumza kwa zamu katika Kijiji cha Usambara ilipo nyumba ya Kilango kwenye Kata ya Kihurio, viongozi hao wa CHADEMA walieleza kusikitishwa na hatua ya mbunge huyo aliye katika kundi la wabunge wa chama tawala waliojipambanua kupambana na ufisadi, kusafiri hadi Moshi Mjini na kumshambulia mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA).
Akihitimisha hotuba katika eneo hilo la nyumbani kwa Kilango baada ya viongozi wengine kuzungumza, Mbowe aliwataka wananchi wa Same Mashariki kutambua kuwa tatizo la ufisadi ndani ya CCM limeathiri mfumo mzima wa utawala.
Kutokana na hali hiyo, Mbowe alisema matokeo ya hali hiyo yameifanya CCM kuongozwa na mafisadi ambao wamekuwa wakitumia kila aina ya hila kushinda wakati wa uchaguzi unapofika.
Akimgeukia Kilango, Mbowe alisema, mbunge huyo wa CCM amekuwa akijinadi kupambana na ufisadi huku akijua fika kwamba waasisi halisi wa vita hiyo ni CHADEMA ambao Septemba 15, mwaka 2007 walitaja orodha ya watuhumiwa wakubwa 11 wa ufisadi nchini.
Kutokana na ukweli huo, Mbowe alisema hatua ya Kilango kumshambulia Ndesamburo katika jimbo lake, inaweza kuifanya CHADEMA ikalazimika kumfungia kazi mama huyo kwa kumuangusha katika kinyanganyiro cha ubunge mwakani na kumfanya alazimike kwenda likizo kuishi na mumewe huko Mtera mkoani Dodoma.
Akizungumza katika Kijiji cha Bendera, Kata ya Bendera wilayani hapa, Mbowe alisema hakuna sababu ya Kilango kupiga kelele bungeni kuwa anapambana na mafisaidi huku wakazi wa jimboni kwake wakiwa wanakunywa maji yanayotiririka mtaroni na kunywa pamoja na wanyama.
Sina ugomvi na Mama Kilango, nilikuwa naye bungeni, ni rafiki yangu, lakini ugomvi wangu unaanzia pale ninapomuona akiwa anapiga kelele bungeni za kudai ufisadi huku wakazi wa jimboni kwake wakiwa hawana huduma za afya, maji safi na salama, na hata barabara kupita ni shida, hii ni hatari sana, lazima wakazi wa Same muache kuwakumbatia wabunge wa namna hii, kelele zote anazopiga zilitakiwa kupambana na serikali ili wakazi wa Same wapate huduma bora na zinazostahili, alisema Mbowe.
Kijiji cha Bendera kwa sasa kinakabiliwa na njaa kali, jambo lililosababisha mwenyekiti huyo kumtaka Kilango kutumia muda wake mwingi katika kuwatafutia njia mbadala, hata kuwaombea chakula cha msaada na kusimamia, ili kiweze kufika kwa wakati.
Kutokana na matatizo hayo, aliwalaumu wakazi wa Bendera kwa kutokuwa na maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi wao kana kwamba wamefunga ndoa na wabunge wa CCM.
Alisema Kilango hawezi kuwatetea wakazi wa Same wakati yeye mwenyewe anaishi mjini Dodoma na mumewe John Samuel Malecela aliyewahi kuwa waziri na ambaye pia ni mbunge kwa kipindi cha miaka mingi.
Mwanasiasa huyo alisema hata siku moja mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi hawezi kukaa mbali kwa kipindi kirefu na wapiga kura wake na kuonekana katika kipindi cha uchaguzi kwa ajili ya kuwatumia katika kampeni na kupata ushindi.
Awali akihutubia mkutano huo wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika, alisema historia inaonyesha wazi kwamba wakati Ndesamburo alianza kupambana na ufisadi wa CCM tangu mwaka 2000 ndani na nje ya Bunge, Kilango ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa viti maalum, alikuwa kimya akitetea chama chake.
Alisema uamuzi wa Kilango kujivua gamba la CCM na kuanza kujitanabahisha kupiga vita ufisadi, ulikuja baada ya viongozi wa CHADEMA kutangaza rasmi kupambana na ufisadi ndani ya serikali ya chama hicho tawala.
Kama kweli Kilango ni mpambanaji wa kweli wa ufisadi, anapaswa kumuunga mkono mbunge mwenzake wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Ndesamburo na CHADEMA ambao tunafanya mapambano ya kweli ya ufisadi, alisema Mnyika na kusababisha umati wa watu kumshangilia.
Wakizungumza kabla na baada ya mikutano hiyo ya hadhara, wananchi wa kata anayotoka Kilango walieleza kusikitishwa na hatua ya mbunge wao kupata muda wa kuitisha mikutano ya hadhara nje ya eneo lao wakati hajapata kufanya hivyo kwao.
Walisema badala yake mbunge wao huyo amekuwa na desturi ya kuitisha mikutano ya ndani na wana CCM wenzake ambayo pamoja na kuzungumzia masuala yanayohusu jimbo lao, ameshindwa kupambana na mtandao wa udikteta na ufisadi unaoongozwa na viongozi wa kata yao.
Wakitoa mfano wananchi hao waliwaeleza akina Mbowe kuwa, uamuzi wa kijiji kujenga lambo la kuhifadhi maji kwa lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji uliofanikisha kupatikana kwa sh milioni 28 umebatilishwa na kikundi cha wana CCM wachache na badala yake fedha hizo zimeamriwa zitumike kujengea maghala ya kuhifadhia chakula.
Katika malalamiko yao, wananchi hao walisema, uamuzi wa kujenga maghala badala ya lambo la maji wanalolihitaji kwa kiasi kikubwa hivi sasa, umewasononesha ikizingatiwa kuwa, hadi hivi sasa kuna maghala mawili zaidi ya kuhifadhia chakula ambayo hayana hifadhi yoyote ya chakula kutokana na ukame ulioharibu mazao.
Mbali ya hayo wananchi hao, waliwalaumu viongozi wa CCM na mbunge wao kwa kukaa kimya wakati wakazi wa Kata ya Kihurio anakotoka Kilango wakiporwa ardhi yao kwa kisingizio kuwa ni eneo la misitu.
Walisema hatua ya ardhi yao hiyo kuporwa, imesababisha akina mama wengi kulazimika kwenda maeneo ya mbali kuchota maji na hivyo kuwaongezea matatizo mengi.
Naye Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo Taifa wa CHADEMA, Benson Kigaila, alisema kuwa mbunge huyo hana hoja kutokana na kupiga kelele anapambana na ufisadi huku akishindwa kuwataja mafisadi wanaotuhumiwa.
Alisema kuwa kama Kilango ni mpambanaji wa kweli wa ufisaidi, anatakiwa kutoka katika chama hicho na kutafuta chama mbadala kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya CCM wanaoongoza katika ufisadi nchini.