Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Hii safu mpya iliyoingia CcM inachokosa ni Agenda. Haiwezekani mkutano wa kwanza kwa umma usiwe na issue za nini watafanya kwa wananchi katika kuzisimamia serikali.
Unapokuwa na kikao cha kwanza na wananchi au adhira yoyote agenda kubwa baada ya utambulisho ni maono ya pamoja. Hotuba au mazungumzo ya kwanza na vyombo vya habari yanapaswa kuwafahamisha umma ni kipi na kwa mbinu zipi utafanya kutatua changamoto za wananchi?
Leo nimemsikiliza Joketi hakuna alichoonyesha anakwenda kukifanya badala yake anahubiri kuaminiwa. Je kwa mtizamo wake kuaminiwa kunapunguza mfumuko wa bei? Kama alifanya vizuri kwanini ameshushwa? Haya yalipaswa kuwa maswali na alipaswa kuwaelekeza vijana wafanye nini?
Ally Hapi nadhani yeye kilichokuwa moyoni mwake toka ametenguliwa ni kuwaza lini atarudi kwenye siasa. Hakutumia muda wake kuwaza siku akirudi ataboresha wapi. Matokeo yake day one tu ya kazi tayari ameonyesha kukosa vision. Tukumbuke huyu ni katibu mkuu wa idara ya wazee. Alipaswa kuwaambia wazee nini anategemea kuja nacho kwa umri wake kama vijana ili wazee wote nchini wanapokaa na jamii waweze kuyadodosa na kuyaweka kwenye matendo maono ya mtendaji wao mkuu.
Ndugu Amos Makala yeye kwa fikra zake anaamini uenezi ni propaganda. Anaamini alizaliwa Kariakoo basi anaweza kuwa kiongozi. Anashindwa kuelewa kwamba kwa kauli yake ameonyesha wazi kwamba waliozaliwa nje ya Kariakoo siyo watu na siyo viongozi. Lakini kwa tafakuri nyingine Kariakoo ni sehemu ya wezi na wavunjaji wa sheria; means Makala anavyoamini yeye siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi ni wizi wa kura. Na ndiyo maana anatamka bila kuonyesha mikakati yoyote kwamba atashindaje uchaguzi?
Tunapoteua timu kama hii ikaingia mtaani kukutana na timu ya chadema inayoongoza maandamano kwa kueleza ugumu wa maisha, mfumuko wa bei na rushwa iliyokithiri ni wazi kwamba Mhe. Mwenyekiti wa Chama anayo kazi yakurudi tena kwenye vyanzo vya taarifa na kuteua watu wenye kupambana kwa hoja.
Hawa viongozi wakiingia kwenye mdahalo na vichwa kama Mnyika tutarudi kwenye historia ya Tido mhando kwenye MCHAKATO MAJIMBONI. Leo hii siku Makala kwa uwezo wake ulivyo akisema aende kwenye mdahalo hata na John Pambalu chama kutavuliwa nguo. Hawa viongozi wanakosa utafiti na walishaacha kusoma na kuiona dunia katika angle za wapinzani
Narudia tena MKUTANO WA KWANZA WA MWANASIASA NA MWANANCHI NDIO UTOA MWANGA WA WAPI KIONGOZI HUYO WA KISIASA ANATAKA KWENDA. SAFU YA NCHIMBI IMEKOSEA SIDHANI KAMA ITAWEZA KUJIREKEBISHA.