Uchaguzi 2020 CHADEMA wana faida kubwa mbili

Uchaguzi 2020 CHADEMA wana faida kubwa mbili

Malcom XX

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2020
Posts
470
Reaction score
949
1: Mikoa ya kanda ya kati ni base ya Lissu kwa maana ni mtu wao wa nyumbani kisaikolojia ni ngumu kwa watu wa nyumbani kwako kukuacha kukuunga mkono, kanda hii inatarajiwa kuwa na wapiga kura milioni tatu.

2: Mikoa ya kanda ya kasikazini ni ngome ya chadema kwa maana kuwa ni makao makuu ya Mwenyekiti Mbowe na Chadema imejengwa kupitia kanda hii, Arusha ndio mother and father of revolution in Tanzania, Kanda hii inatarajiwa kuwa na wapiga kura kama milioni tatu na nusu.

AKILI YA LISSU NI KUBWA, HAJAHANGAIKA NA KANDA YA KASIKAZINI AKIFAHAMU KUWA ENEO HILI HALINA SHIDA HIVYO KAJARIBU KUFRUSTARATE KAMBI YA JIWE HUKO KANDA YA ZIWA, JAPO KUWA JIWE ATAONGOZA KANDA YA ZIWA BUT SIYO KWA KIWANGO KIKUBWA hivyo inampa fursa Lissu kumpiku Magufuli kwa kura za Kusini ambazo kwa kiwango kikubwa Magufuli atazikosa kwa sababu ya korosho.

Dar es Salaam ni ngoma droo,
 
Lissu anafanya kampeni kwa akili sana na kila anakopita watu wanampokea vizuri, mm niko mwanza naona kabisa lissu atapata kura nyingi sana
Yani magufuli hadi kwao chato hali ni mbaya, kweli MUNGU ni mkuu na amepandikiza chuki ndani ya mioyo ya watu dhidi ya magufuli kila mtu anamsema vibaya
 
Mkuu una mawasiliano mazuri na hizo kanda kwa uhakika? Mwaka huu ungekuwa mzuri sana lakini hatukujipanga . .. ... .. .

Hakuna kanda tutatoka salama.

Fanya mawasiliano vizuri usijiaminishe hali inaweza kuja tofauti, kiushabiki tutakuunga mkono uzi wako. Siasa ni maisha sipendi nifanye ushabiki maandazi, naandika kama kilivyo japo nitakosana na wengi. . . .ambao mashabiki.
 
Kanda ya ziwa haijawahi kuwa ngome ya CCM, 2015 karata ilichangwa vizuri kuongeza kura na hata hivyo hazikutosha kwa kiasi kilichofikiriwa, mwaka huu zitapungua zaidi.

Tulipata wabunge wangapi wa majimbo kanda ya ziwa 2015?
 
Mkuu una mawasiliano mazuri na hizo kanda kwa uhakika? Mwaka huu ungekuwa mzuri sana lakini hatukujipanga . .. ... .. .

Hakuna kanda tutatoka salama.

Fanya mawasiliano vizuri usijiaminishe hali inaweza kuja tofauti, kiushabiki tutakuunga mkono uzi wako. Siasa ni maisha sipendi nifanye ushabiki maandazi, naandika kama kilivyo japo nitakosana na wengi. . . .ambao mashabiki.
Hapa umejitafsiri jinsi ulivyo shabiki maandazi!
 
Ni tahadhari Boss

Chadema isibweteke, ijipange na uzembe wa 2015 usijirudie

Hata Ezekiel wenje alipitezaje ubunge?

Tushangilie tu nyomi na Kimbunga
CDM safari hii 2020 wapo very organized.

Narudia tena , 20015 si 2020.
 
CCM wamepoteana kila mahali. Chama Cha Lisu kikipanga safu ya mawakala vizuri na usimamizi wa kura za rais ukawa mzuri Lisu ataibuka mshindi mapema Sana.

Kuna tabia ya wagombea ubunge kukomaa kulinda kura zao na kusahau zile za rais. Hapoo ndipo huwa wizi unafanyjika.
 
Stronghold za Chadema kwa hisia zao ni mikoa ya kaskazini {Arusha , Kilimanjaro na Mara)

Na kwa nyanda za juu kusini ni Mbeya pekee, ambako kote huko tayari wameshatepeta.

Mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi, Ruvuma) Chadema hana influence kabisa.

Singida labda kule kwao Kijiji Cha mahambe ila kwa Dodoma inafahamika kabisa mshindi ni CCM.

Huko kanda ya Ziwa unakosema amevuruga, hana impact yeyote.

Kwa ufupi ni kuwa Lisu atapata kura zisizozidi elfu mbili, akijitahidi sana atafikia elfu 5, ila hawezi fikia kura laki sita za Mbowe.
 
Chadema jamani msisitizo mawakala wapewe barua na mafunzo . Njama za CCM Ni kubwa sana .
Screenshot_20201015-115322.png
Screenshot_20201015-115258.png
 
1: Mikoa ya kanda ya kati ni base ya Lissu kwa maana ni mtu wao wa nyumbani kisaikolojia ni ngumu kwa watu wa nyumbani kwako kukuacha kukuunga mkono, kanda hii inatarajiwa kuwa na wapiga kura milioni tatu.

2: Mikoa ya kanda ya kasikazini ni ngome ya chadema kwa maana kuwa ni makao makuu ya Mwenyekiti Mbowe na Chadema imejengwa kupitia kanda hii, Arusha ndio mother and father of revolution in Tanzania, Kanda hii inatarajiwa kuwa na wapiga kura kama milioni tatu na nusu.

AKILI YA LISSU NI KUBWA, HAJAHANGAIKA NA KANDA YA KASIKAZINI AKIFAHAMU KUWA ENEO HILI HALINA SHIDA HIVYO KAJARIBU KUFRUSTARATE KAMBI YA JIWE HUKO KANDA YA ZIWA, JAPO KUWA JIWE ATAONGOZA KANDA YA ZIWA BUT SIYO KWA KIWANGO KIKUBWA hivyo inampa fursa Lissu kumpiku Magufuli kwa kura za Kusini ambazo kwa kiwango kikubwa Magufuli atazikosa kwa sababu ya korosho.

Dar es Salaam ni ngoma droo,
Kura zimeamuliwa kanda ya ziwa...
 
Back
Top Bottom