CHADEMA wanafanya Janja Janja kumtangaza Mgombea Urais

CHADEMA wanafanya Janja Janja kumtangaza Mgombea Urais

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
450
Reaction score
423
Tundu Lissu anatarajiwa kuingia nchini siku ya Jumatatu tarehe 27/07/2020 akitokea Ubelgiji.

Taarifa kutoka chanzo kilicho ndani ya chama hicho, ambacho kimsingi hakikubaliani na namna mipango inavyofanywa, zinasema kuwa initially, CHADEMA ilipanga Lissu ashukie katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta huko Nairobi kwa kile walichosema kuwa ni kutokana usalama wake, lakini recently wameamua ashukie JNIA wakisema kuwa hilo litampa political mileage kutokana na sababu tatu ambazo wao wanaziona:
  1. Wanaamini kuwa Lissu amekuwa akitafutwa na Mahakama kwa muda mrefu ili aweze kujibu kesi zinazo mkabili. Mara kadhaa wadhamini wake wameshindwa kujitoa kwenye kesi hizo kwa kuwa mtuhumiwa wanayemdhamini hajaonekana mahakamani kwa muda mrefu bila taarifa yoyote. Hivyo CHADEMA wanaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Lissu atakamatwa na kuwekwa mahabusu. Kitendo hicho kitafanya waanze kulalamika kuwa Lissu amewekwa ndani kwa kuwa ameonyesha nia ya kugombea Urais wa JMT kwenye uchaguzi Mkuu ujao na hivyo kupata sympathy toka kwa watu mbalimbali. Baada ya hapo mawakala wake wataizungusha fomu yake nchini kumuombea wadhamini wa ndani ya chama chao, na kufanya hilo kama sehemu ya kampeni za kumnadi.​
  2. Wamefanya mabadiliko hayo baada ya kujua kuwa muda ambao Lissu atakuwa akiwasili nchini, Tanzania itakuwa kwenye maombolezo ya Kitaifa ya msiba wa Marehemu Benjamin William Mkapa. CHADEMA wamekuwa wakihamasisha wanachama wao kujitokeza Uwanja wa Ndege wa JNIA kumpokea Lissu, licha ya Kesho la oPolisi kuzuia mikusanyiko yoyote ya kisiasa kwa kipindi hiki cha maombolezo, na pia kutokana na sababu kuwa Uwanja wa JNIA utakuwa busy kupokea wageni wa Kitaifa na Kimataifa wanaokuja kuhudhuria Mazishi ya Marehemu Mkapa. Chadema wanaamini kuwa Polisi watatumia nguvu kuwatawanya wafuasi wao katika Uwanja huo wa ndege, na hivyo kutumia kitendo hicho kama sehemu ya kujitangaza kisiasa na hivyo kujiongezea umaarufu.
  3. Aidha CHADEMA wamesema kuwa siku ya Jumanne, Lissu atatakiwa kwenda Uwanja wa Uhuru kwenye tukio la kumuaga Marehemu Mkapa kitaifa. Wanasema kuwa uwepo wa Lissu katika tukio hilo inabidi ufahamike na watu wote watakaokuwepo katika eneo hilo. Moja ya njia watakayotumia ni kufanya mpango ili Lissu atoe salamu kwa niaba ya vyama vya upinzani, ijapokuwa ACT nao wanaitaka nafasi hiyo ili Mgombea wao Membe apate nafasi ya kuzungumza.
Chanzo hicho cha habari kinasema kuwa CHADEMA iliamua kutengeneza migogoro feki ndani ya chama ili tu kuwapumbaza washindani wao. Walimtaka Mbowe achukue fomu ya kugombea Urais ili watu waone kuwa hiyo nafasi Mwenyekiti anaitaka, lakini ukweli ni kuwa Mbowe anataka kugombea Ubunge Jimbo na Hai. Aidha kitendo cha Godbless Lema hivi karibuni kusikika akimnanga Lissu kilikuwa ni danganya toto, ilikuwa ni sehemu ya migogoro hiyo feki.

Chanzo hicho cha ndani kinasema kuwa wanachama wengi hawafurahishwi na namna CHADEMA inavyopanga kujipatia umaarufu kwa njia ambazo ni haramu. Kimesema wao hawakubaliani na namna yoyote ile inayohamasisha maandamano haramu, kwani yanaweza kuwa na maafa makubwa kwa raia wanyonge wakati Viongozi wakijijenga kisiasa.

Mchezo huo mchafu umefahamika, CHADEMA wanataka kujijenga kupitia migogoro wanayosababisha nchini ambayo mara nyingi imekuwa ikisababisha madhara kwa Watanzania.
 
Benmpo,

Ivi Tarehe ya Ujio wa TL na Kufa kwa BM nikipi kilianza?

Nani hapo alitakiwa kufix ratiba yake kwanza kwaajili ya mwenzake?

Bila kujalisha Nin na nani, kafanya nn. Imekuaje, Ratiba ya Lissu kurudi ni kesho na wote lazima muiheshimu ivoivo.. MNAMPANGIA?

Alafu unakuta mtoa mada ni Mwakyembe Madegree alopigwa KO na Wajumbe[emoji23].
 
Ratiba ya wajumbe iko ivi

Baada ya kesho kumpokea ,

Wajumbe /Watanzania woteee wenye mapenzi na T.Lissu, vyama vyotee .

Tuhakikishe Tunakuwepo sanaaaaa siku T.Lissu atakapoenda Msibani.

Akifika tuu, tunampokea kwa Shangwe, vifijo, nderemo, makofi, nyimbo na ngojera.

Nani kasema, nguvu ya Umma imewahi kushindwa?
 
Tulieni hivo hivo dawa iwaingie nyie si mlisema Chadema haina mgombea urais hahaha
 
Hahaha! Natabiri kuanzia kesho thread zote humu jukwaa la siasa zitahusiana na Lissu.

Lakini pia naamini kuna watu wako kwenye hali ngumu sana! Matumbo yananguruma! Usiku wa leo ni wa taabu sana!
Wanateseka sana kisaikolojia.
 
Sana! Haswa kwenye uamuzi wa kumkamata.

Pamoja na huu msiba, kunawafanya wazidi kutaabika kwenye maamuzi.

Ngoja tuone.
Kama wanaongozwa na busara, watamuacha, ila kama sivyo, tutarajie kuona wakiharibu hali ya hewa hiyo kesho
 
Mtoa mada kajaza kinyesi cha mbwa kichwani badala ya ubongo. Matokeo yake anaongea pumba na udaku.
 
Kwa nini watu wanateseka kwa ujio wa Lissu? Na mara nyingine ni hao hao waliokuwa wanasema kwa nini harudi nyumbani. Dhamira zinawasuta
 
Kusoma tu, munasikitisha shana.. kuona chadrama.. bado hawafahamu.. kuwa wapinzani. Poleni sana wapiga mbizi.. mitandaoni.. vizuri munafahamu CCM bapo dakika tano mbele yenu.. na pia wananchi wengi bamewachoka na drama za kupenda kukamatwa.. kwa makisudi.. siasa za futi sita..

2020 ni Magufuli
 
Benmpo,

Ivi Tarehe ya Ujio wa TL na Kufa kwa BM nikipi kilianza?

Nani hapo alitakiwa kufix ratiba yake kwanza kwaajili ya mwenzake?

Bila kujalisha Nin na nani, kafanya nn. Imekuaje, Ratiba ya Lissu kurudi ni kesho na wote lazima muiheshimu ivoivo.. MNAMPANGIA?

Alafu unakuta mtoa mada ni Mwakyembe Madegree alopigwa KO na Wajumbe[emoji23].

Ni wapi umeambiwa amepanga jana kurudi. Tumia akili wewe Mbweha Mweupe
 
Back
Top Bottom