CHADEMA, Wanaharakati waalikeni waungwana mpatanishwe

Mzee Slaa na Mwabukusi Tajiri Yao mmoja, wanalazimika kuwa pamoja hata kama hawapendani au wanatamani kuwa tofaut

Ni kama Haji Manara na Ally Kamwe hata kama hawapatani lazima washirikiane na mmoja aki post lazima mwingine a like ili kwenda sambamba na masharti na maelekezo ya GSM
 
Mwabukusi siyo mwanaharakani,ni mwanasiasa,mwanachama wa NCCR Mageuzi na moonbeam ubunge Busokelo 2020
Msimfiche kwenye uaharakati na kuisumbua CDM kisa yeye,Ana Chama chake akitumikie na akitumie kufanya mambo yako.

Ungali ukichanganya Mwabukusi na wanaharakati.

Pamoja na kuwa mada ni kuhusu wanaharakati na si Mwabukusi, labda:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Bila shaka Uzi huo utakuonyesha:

1. Kwa nini kusigana kwa Chadema na Wanaharakati.
2. Kusigana kwa Chadema na Slaa na Mwabukusi.

Hata hivyo nikukumbushe kubakia kwenye mada ukizingatia ujumbe ulikuwa;

1. ni ushauri wa bure kwa waheshimiwa kabisa
2. Tena ikiwapendeza. Si lazima.
3. Kwa wanachama wa kawaida ambao utambulisho wao uko hapa:

Watambue Wanachama wa Vyama Mitandaoni

4. Kumbuka hakuna mwenye hati miliki ya uanachama kwenye chama.
5. Hakuna mwanachama anayeweza kujinasibu kuwa mwanachama zaidi kuliko mwingine.



Kwenye huu Uzi:

Tetesi: - Wapo wapi Lema na Sugu?



Fikirieni mara 2 walia machozi ya mamba kina Pohamba ndiyo waunga mkono wenu wakubwa leo kwenye hoja zenu uchwara hizi za kuushadadia utengano.

Muelewe vipi au hadi tukutane ana kwa ana kwenye mikutano ya vyama?
 

Nakusoma hapa:



Kwenye uzi wenu huu:

Mbowe na Tundu Lissu wako kimya sana kuhusu kesi ya Uhaini!

Mkaanga mbuyu, siyo? Kwa hiyo hapa ni machozi ya mamba?

Sherehe kubwa Lumumba, CHADEMA wakiparurana

Utake vipi wewe, kwa wawili hawa kukaribiana, Lumumba pale?
 
Slaa na Mwabukusi ndiyo walianzisha utengano na ndiyo walishadadia utengano,wafanye kazi kwenye vyama walivyoviamini waiache CHADEMA kama ilivyo
 
Slaa na Mwabukusi ndiyo walianzisha utengano na ndiyo walishadadia utengano,wafanye kazi kwenye vyama walivyoviamini waiache CHADEMA kama ilivyo

Uko nje ya mada iliyoelekezwa kwa wadau 2 kama taasisi.

Walengwa kwa upande ni wanaharakati kama wadau katika siasa. Siyo hao ulio wataja.

Kama nia yako ni kuwajadili hao, labda fikiria kuanzisha uzi rasmi kuwahusu.
 
Sijui, ila kam ndio hivyo basi Mwabukusi anajipoteza
 
Hivyo CCM nayo inamalengo tofauti na lile la kuwatumikia wananchi? Au hii ina vihusu vyama visivyo madarakani tu?

Kuwatumikia wananchi maana yake ni kuwasikiliza na kutenda wanayotaka. Kwa maana ya kuwa huwezi kujinasibu kuwatumikia wananchi kama wewe siyo muumini wa demokrasia.

Suala la bandari, Katiba mpya, report za CAG, kadhia lawa Masai na mengi yanaonyesha CCM wanamtumikia nani.

Kwamba nchi Inahitaji ukombozi ni kwa kuwa CCM wanajitumikia wao si wananchi.
 
CCM wantumikia matumbo yao na familia zao. Wanachota mali ya umma kwa maslahi yao binafsi hawautumikii umma.
Kunahaja kuwa na vikundi kama Hamas kwenye vyama ili kukata kiu kama yangu, kuondoa takataka za ccm kwa nguvu maana sasa imekuwa too much.
 
Hayo mawazo yako.

Sasa nitaandika mawazo ya nani ndugu? Au ungependa niandike ya nani? Mawazo yangu yana basis yaani msingi au hoja.

Ndipo yanakuja yale ya hoja kupingwa kwa hoja. Siyo kwa rungu.
 
CCM wantumikia matumbo yao na familia zao. Wanachota mali ya umma kwa maslahi yao binafsi hawautumikii umma.
Kunahaja kuwa na vikundi kama Hamas kwenye vyama ili kukata kiu kama yangu, kuondoa takataka za ccm kwa nguvu maana sasa imekuwa too much.

Haihitaji HAMAS kuwapa CCM nafasi ya kusema ugaidi Ili wapate sababu ya kumshikilia mtu magerezani:

Kujikomboa kutoka CCM, uwe tayari kujitoa ufahamu
 
CDM warudisheni Dr Slaa na wale COVID 19 siasa ni kusoma fursa. CCM sasa hivi inabebwa na makada waliokuwa CDM,imarisheni timu.
 
Kwani akina Mbowe hawana mtu wa kupiga naye dili tena CCM 2025 hadi wahangaike na akina Slaa?
 
Halafu Dr Slaa ni mvurugaji wa madili.
2015 ilikuwa imebaki kidogo tu atuharibie dili letu na Lowasa.
 
Halafu Dr Slaa ni mvurugaji wa madili.
2015 ilikuwa imebaki kidogo tu atuharibie dili letu na Lowasa.
Ana wivu uliopitiliza. Kanisani aliharibu, kwenye siasa anaharibu, sijui hata kama anaelewa anachokitaka. Hta serikali ikitekeleza kila kitu wanachotaka, Dr.Slaa bado hato ridhika.
 
Kwanza ningependa kuwashukuru Mbowe na Lissu kwa kuweza kukaa kimya na kuficha Tofauti zao za Kisiasa chamani. Ni jambo zuri na Tuwaombee waweza kupatana, kwani Tanzania Inahitaji Chama cha Upinzani madhubuti . Pia natoa Shukrani kwa Vyama veginevyo vya Upinzani kama ACT na hata Chama Tawala, kwa kutotumia Fursa hii ya Mgogoro wa Chadema kwa manufaa yao.

Tukumbuke mara nyingi tatizo ndani ya Chadema ni Uongozi, tokea enzi ya Marehemu CHACHA WAngwe, ZITTO na SUMAYE, Lakini safari hii kwa sababu LISSU hakujitokeza waziwazi ila kwa Vitendo ndio maana hatuoni KAMPENI na kelele za nani ashike uongozi wa Chadema.

Tuwaombee kila la kheri
 
Ana wivu uliopitiliza. Kanisani aliharibu, kwenye siasa anaharibu, sijui hata kama anaelewa anachokitaka. Hta serikali ikitekeleza kila kitu wanachotaka, Dr.Slaa bado hato ridhika.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mwanaharajati anayejitambua. Huyu SI mwanasiasa usu wala mwanaharakati usu. hao wote wameelezewa humu:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Ni sahihi kabisa usemavyo:

1. Mwanasiasa mwanaharakati huwa uanaharakati wake haukomi kwani Serikali madarakani haiwezi kufanya yote waystayo wananchi.

2. Mwanasiasa mwanaharakati anayejitambua atashutumiwa wanasiasa usu kwani ni nia yenu kutaka kumtumia kama grader kufikia malengo yenu.

Kumhusu mwanasiasa mwanaharakati ni haya hapa:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.
 

Lissu ni mwanasiasa mwanaharakati mwenye hekima yake. Kumwomba Mungu kwenye hili Ili kupisha shari kutokea kwake ni kumpa kazi si zake. Mungu anazo kazi nyIngi Hadi za migogoro Palestina huko.

Si rahisi Lissu kuingia kwenye mgogoro na chama chake labda kwa hao wengine kutaka mgogoro naye. Hao ndiyo wa kuombea sana. Hawa hapa ni mfano wao:



Kwenye uzi huu:

Tetesi: - Mbowe na Dkt. Slaa wafanya kikao cha siri jijini Dar es salaam

Kuwa mwanaharakati hakukuondoi kwenye chama. Vyama vya siasa ni vya uanaharakati. Vyama vya siasa vinawahitaji sana wanaharakati kuliko wanavyovihitaji vyama.

bIla wanaharakati vyama vya siasa ni kama Simba asiye na meno Wala makucha. Uzi huu hapa chini umejielekeza:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Ndiyo maana hekima ingewaingia mapema wakawahi kwa hii aina ya akina:

"Sheikh Ponda, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi, Prof. Shivji, Askofu Mwamakula (pole zake kwa msiba) nk, nk, kwenye jopo kama hilo kwa upatanisho."

Tatizo si wao ila yale masikio, ya kufa:

imhotep, Retired, Mshana Jr, Tua Ngoma, JokaKuu na wenzenu, mjumbe hauwawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…