chadema wanahusika??

chadema wanahusika??

Nachaone

Member
Joined
Sep 24, 2018
Posts
67
Reaction score
73
Wiki mbili zilizopita Balozi za Nchi za Magharibi walitoa tuzo ya Ushujaa kwa Wanaharakati wanaotumia social media, ktk tuzo zile hakuwepo mwanachama hata moja wa Chama Cha Mapinduzi karibu watu wote waliyopewa tuzo ni Wanaharakati wenye Malengo ya kupinga serikali iliyopo madarakani.
Wiki mbili baada ya tuzo kutolewa mwanachama wa Chadema Tanzania anadaiwa kutoweka kule Mbozi na Social media inatumika.
Kinachonipa wasiwasi ktk ili upatikanaji wa huyu mwanachama wa chadema, kwanza Naibu waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni anaagiza Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa Mheshimiwa Peter Msigwa asaidie Polisi kuhusu kutoweka kwa mwanachama wake,
Lakini pia Mbunge wa Mbozi anakamatwa bungeni Dodoma siku kadhaa baada ya polisi kuwatia mbaroni Viongozi hao wa chadema mwanachama wao anapatikana huko Mbeya vijijini tena anaokotwa na Diwani wa chadema bora hata wangesema wameokotwa na wananchi wa kawaida kuliko kuokotwa na Diwani wa chadema.
Siku tano wa kutoweka kwa kijana huyo wa chadema mambo Mengi sana yalikuwa yakitolewa ktk Mitandao ya kijamii.
Tulisikia sauti ya Mwanamke akilia kwa uchungu kwamba mheshimiwa Rais wa JMP Dr John Pombe Magufuli ameagiza Mdude Nyagali auwawe na alipigwa vibaya ajitambui.
Sauti Ile ilisikika ikidai alikuwa akipewa Taarifa na mmoja wa Watekaji aliyekuwa akimwita Shemeji ambaye wanafahamiana pia kilikuwa na taarifa zinatembezwa kwenye makundi ya WhatsApp ya chama cha chadema ikionyesha Watekaji walikuwa wanawasiliana na familia ya Mdude Nyagali.
Tukumbuke operation yote hii ilikuwa ikiendeshwa kwenye social media.
Ktk kupotea kwa mwanachama huyu wa chadema niliyoona mpk mabalozi wa nchi za Ulaya Magharibi wakishiriki ktk harakati hizi za social media.
Social media kwa sasa ni sehemu ya Mkakati wa Nchi za Magharibi kuhamasisha vijana wa nchi za ulimwengu wa tatu kuvuruga Amani ktk nchi zao.
Ni Matumaini yangu kuwa Chadema itasaidia Vyombo vya Dola kumpata Yule mtekaji aliyekuwa akiongea na mke wa Marehemu ili kutokomeza kadhia hii mbaya inayochafua taswira ya Taifa letu.

Na: MZAlendo
FB_IMG_1557397133018.jpeg
 
Nyie tengenezeni taifa la kitekaji tu siku na nyie ccm mkianza kutekwa msilielie
 
vp kwa wanachhama wao ambao hawakuonekana tena? vp kwa upande wa media nao wanahusik na wenzao waliopotea?
 
Mwisho mtasema na MO Dewji alitekwa na chadema.
akwilina alipigwa risasi na chadema.
Lisu alipigwa risasi na chadema.
Ben saa nane kapotezwa na chadema.
Kila baya LA chadema.
 
haya mambo enzi za jakaya hayakuwepo, ila na chadema ilikuwepo, ifike hatua hata sisi malofa wasituchukulie kuwa tuna hakiri za limbwata.
 
Back
Top Bottom