Uchaguzi 2020 CHADEMA wanajipa matumaini hewa

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Kwanza kabisa me sio mpenzi wa vyama vya Siasa ila nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania. Nimefatilia mchakato mzima wa chama Cha Chadema na wote tumejua wagombea wa uraisi watakao chuana na Dr. John Magufuli niwe mkweli katika hai wagombea wote sijaona hata mmoja atakayepata kura kuanzia 40% kuendelea dhidi ya Magufuli, keep it in your mind.

Nimeona humu jamvini wapenzi wa Chadema wakiaminishana watashinda uchaguzi mkuu. Niwaambie kitu: Hakuna Jambo zuri kama kukubali hali halisi kuliko kujipa matumaini hewa.

Kuwa rais wa nchi sio jambo jepesi kama wanavyoaminishana wanaChadema. Kuna vitu vingi vinavyo determine mtu kuwa raisi Kama ifuatavyo:

1. Financial capability
Uwezo wa mgombea kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha au Chama kinachomsimamisha wa kufanya kampeni kwenye maeneo mengi ya Tanzania.Ukiangalia wagombea wa chadema hawana uwezo mkubwa wa kifedha. Lowassa aliweza kupata kura around 6 million; haikuja kwa urahisi ali-invest sana hela. Kwanza alinunua baadhi ya vipindi vya television ikiwemo ITV kuwafikia Watanzania wengi, ndio mgombea pekee aliyewahi kutokea wa upinzani ambaye aliyofanya kampeni maeneo mengi ya Tanzania n.k

2. Strong group support
Hapa tuna angalia makundi yenye nguvu Magufuli ana support kubwa ya viongozi wa dini zote na amecheza karata zake vizuri amejenga misikiti na amekuwa karibu Sana na viongozi wa kiislamu karibia shughuli zote pia ana support ya viongozi wa kikristo hata wale waliokuwa wanampinga sasa wapo upande wake kama mchungaji wangu Maksai wa kanisa la Korogwe huyu alikuwa ni Team Lowassa na alimpigia sana kampeni kanisani ila nowdays ni Team Magufuli na amekuwa anampaisha sana kanisani. Kuna Lusekelo, kuna Gwajima n.k Kuna magroup mengine ila naomba niishie hapo wakati Chadema haina mahusiano mazuri na viongozi wa dini.

3. 99.9% of artists support CCM
Wasanii wote wenye influence kubwa kwenye Jamii wanaisapoti CCM Kama vile Diamond and WCB in general ambao Wana wafuasi wengi sana kwa jina la "Team WCB" Kuna Alikiba, Harmonize, Mwana fa n.k

4. Kuwekeza kwenye majimbo aliyokosa kura
Hii Ni sababu itakayompa ushindi mnono Magufuli mf. Jimbo la Arumeru Arusha lilikuwa na tatizo sugu Sana la ukosefu wa Maji ila chini ya Magufuli ameleta mradi mkubwa wa Maji lakini pia walikuwa wanasumbuliwa na tatizo la Umeme tangu aingia Magufuli ameweza kupunguza tatizo la Umeme kwa kiasi kikubwa Sana. Kuimarisha usafiri wa treni Moshi, la tatu ni kuweka Dar kajenga flyover na miundombinu ya Barabara lakini uko kwetu kimara kulikuwa na tatizo maji kwa kiasi kikubwa na nikilio kikubwa kwa wakazi wa Ubongo, Kimara na Mbezi Magufuli amelitatua kwanza kwa kuaweka mabomba maeneo yote bure na wanatoa maji karibia wiki nzima. Suala mgao wa Umeme ulikuwa unaboa Sana na ilikuwa Ni tatizo kuu sana kwa dar ila now day inaweza kuchukua miezi hata 6 Umeme usikatike na hata ukikatika unarudi mapema tofauti na kipindi Cha nyuma.

NB: Kama nilivyotoa analysis yangu kwa kifupi Chadema hata kupata Asimilia 40 ya kura itakuwa ngumu kupata huo ndio ukweli wenyewe.Na bahati nzuri nyuzi zinabaki humu Kama kumbukumbu tutajionea.
 
Hata aslimia kumi hawapati,arobaini umadiria kubwa sana.
 
Duh aiseee ukiwa WCB basi unaamini kila music mzuri ni mali ya WCB na kila uongozi mzuri ni mali ya CCM

Yaani ukaona uzi bila kuiweka timu doma haujakamilika. Domo anajipendekeza CCM ili mambo yake yakae sawa ila CCM kamwe haijawahi jipendekeza kwake zaidi ya kumtambua harmo(inauma hapa)
 
Sasa kama siyo mwanasiasa umeleta thread ya siasa kwa sababu gani.

Ungetaja sababu za chadema kushindwa kama;

Miaka 5 bunge haikuwa live na bungeni spika alikuwa mwonevu kwa vyama upinzani

Miaka 5 wabunge wa chadema walibambikiwa kesi na mda mwingi kupoteza huko,

Jeshi la polisi kuivuruga chadema kulinda maslahi ya CCM ,

CCM ndani ya miaka 5 inafanya kampeni huku vyama vya upinzani vikiwekewa marufuku
,
hakuna tume huru ya uchaguzi.

CCM kununua watu wa kuiunga mkono hasa wabunge na madiwani wa upinzani,wenye msimamo kuwatisha,kuwatesa na kuwaweka ndani.

Siyo unakuja hapa kukata mauno na bangi zako.

Halafu si alisema urais ni kazi nzito na unamwumiza kichwa mbona leo ndo wa kwanza kuchukua fomu ya urais?



Mzee jikite kwenye hoja me sio mwanasiasa au mshabiki wa chama Kama wewe
 
😁😁😁
 
Iwapo ni sahihi yote uliyosema hivyo CCM na Magufuli waache kutumia mabavu na sapoti kutoka vyombo vya dola iwe ni free and fair elections
Hawatathubutu,wanafahamu kitakachotokea.Wanakumbu kumbu za 2015,Mh.hajazoea vya kuchinja maana vinamkawiza.
CCM ya Mwl.Nyerere kuogopa demokrasia,haya ni maajabu.Chama cha gwiji wa siasa safi,Fundi Wa kujenga hoja na midahalo.Sasa hivi viongozi wa CCM hawawezi aina yoyote ya Free Style debate katika ngazi yoyote. Siyo madiwani,wabunge ama Mzee mwenyewe.
 
Tatizo nyumbu hupenda kusikia sifa tuu na matumaini hewa. Wanafanya vitu vya hovyo halafu wabunge,madiwani wakiwakimbia wanadanganywa kwamba wamenunuliwa.
Kama kuna kitu kitawaangamiza cdm kwenye uchaguzi huu ni ubinafsi wao wakujiona wajuaji na kung'ang'ania lockdown kinyume na watanzania wengi. Hiyo imedhihirisha kwamba cdm wanajijali wao na sio wapiga kura.

Pia suala la mlevi wa taifa kuteguka mguu akitoka kwenye uzinzi na kujaribu kuisingizia serekali. Hili limewaumbua. Wamepuuzwa na watapuuzwa kwa kila watakacho dai. Kama walidhani wamepata kiki,basi walichanga karata zao hovyo
 
Huyo Mgombea wako umempitisha kashindana na kina nani?au hamna uchaguzi sisiem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…