Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,078
Kwa maoni yako haya hukutaka uchaguzi ufanyike ?!. Au lengo ni nini, Magufuli asipingwe ?!.Kwanza kabisa me sio mpenzi wa vyama vya Siasa ila nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania. Nimefatilia mchakato mzima wa chama Cha Chadema na wote tumejua wagombea wa uraisi watakao chuana na Dr. John Magufuli niwe mkweli katika hai wagombea wote sijaona hata mmoja atakayepata kura kuanzia 40% kuendelea dhidi ya Magufuli, keep it in your mind.
Nimeona humu jamvini wapenzi wa Chadema wakiaminishana watashinda uchaguzi mkuu. Niwaambie kitu: Hakuna Jambo zuri kama kukubali hali halisi kuliko kujipa matumaini hewa.
Kuwa rais wa nchi sio jambo jepesi kama wanavyoaminishana wanaChadema. Kuna vitu vingi vinavyo determine mtu kuwa raisi Kama ifuatavyo:
1. Financial capability
Uwezo wa mgombea kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha au Chama kinachomsimamisha wa kufanya kampeni kwenye maeneo mengi ya Tanzania.Ukiangalia wagombea wa chadema hawana uwezo mkubwa wa kifedha. Lowassa aliweza kupata kura around 6 million; haikuja kwa urahisi ali-invest sana hela. Kwanza alinunua baadhi ya vipindi vya television ikiwemo ITV kuwafikia Watanzania wengi, ndio mgombea pekee aliyewahi kutokea wa upinzani ambaye aliyofanya kampeni maeneo mengi ya Tanzania n.k
2. Strong group support
Hapa tuna angalia makundi yenye nguvu Magufuli ana support kubwa ya viongozi wa dini zote na amecheza karata zake vizuri amejenga misikiti na amekuwa karibu Sana na viongozi wa kiislamu karibia shughuli zote pia ana support ya viongozi wa kikristo hata wale waliokuwa wanampinga sasa wapo upande wake kama mchungaji wangu Maksai wa kanisa la Korogwe huyu alikuwa ni Team Lowassa na alimpigia sana kampeni kanisani ila nowdays ni Team Magufuli na amekuwa anampaisha sana kanisani. Kuna Lusekelo, kuna Gwajima n.k Kuna magroup mengine ila naomba niishie hapo wakati Chadema haina mahusiano mazuri na viongozi wa dini.
3. 99.9% of artists support CCM
Wasanii wote wenye influence kubwa kwenye Jamii wanaisapoti CCM Kama vile Diamond and WCB in general ambao Wana wafuasi wengi sana kwa jina la "Team WCB" Kuna Alikiba, Harmonize, Mwana fa n.k
4. Kuwekeza kwenye majimbo aliyokosa kura
Hii Ni sababu itakayompa ushindi mnono Magufuli mf. Jimbo la Arumeru Arusha lilikuwa na tatizo sugu Sana la ukosefu wa Maji ila chini ya Magufuli ameleta mradi mkubwa wa Maji lakini pia walikuwa wanasumbuliwa na tatizo la Umeme tangu aingia Magufuli ameweza kupunguza tatizo la Umeme kwa kiasi kikubwa Sana. Kuimarisha usafiri wa treni Moshi, la tatu ni kuweka Dar kajenga flyover na miundombinu ya Barabara lakini uko kwetu kimara kulikuwa na tatizo maji kwa kiasi kikubwa na nikilio kikubwa kwa wakazi wa Ubongo, Kimara na Mbezi Magufuli amelitatua kwanza kwa kuaweka mabomba maeneo yote bure na wanatoa maji karibia wiki nzima. Suala mgao wa Umeme ulikuwa unaboa Sana na ilikuwa Ni tatizo kuu sana kwa dar ila now day inaweza kuchukua miezi hata 6 Umeme usikatike na hata ukikatika unarudi mapema tofauti na kipindi Cha nyuma.
NB: Kama nilivyotoa analysis yangu kwa kifupi Chadema hata kupata Asimilia 40 ya kura itakuwa ngumu kupata huo ndio ukweli wenyewe.Na bahati nzuri nyuzi zinabaki humu Kama kumbukumbu tutajionea.
Nikukumbushe kitu kimoja . Wakati Magufuli anachukuwa fomu za kuomba kazi aliyonayo Leo, hakuwa na nguvu kama kina Lowassa, Membe na hata Sitta. Lakini leo ni Rais na si hao waliokuwa ma giants.
Kitu muhimu ungesema tume tulionayo si tume huru ya uchaguzi . Lakini ukisema swala la kukubalika, huwezi kujiamini mambo ya kura za siri.