Uchaguzi 2020 CHADEMA wanajipa matumaini hewa

Kwa maoni yako haya hukutaka uchaguzi ufanyike ?!. Au lengo ni nini, Magufuli asipingwe ?!.

Nikukumbushe kitu kimoja . Wakati Magufuli anachukuwa fomu za kuomba kazi aliyonayo Leo, hakuwa na nguvu kama kina Lowassa, Membe na hata Sitta. Lakini leo ni Rais na si hao waliokuwa ma giants.

Kitu muhimu ungesema tume tulionayo si tume huru ya uchaguzi . Lakini ukisema swala la kukubalika, huwezi kujiamini mambo ya kura za siri.
 
Nimewauliza wanaccm wengi swali hili; kwanini mnaichagua ccm? majibu yake ni yale yale kama yakwako; Hakuna sababu ya msingi...ni hatari.
 
Magufuli alipata nguvu kwa sababu ya ndio alikuwa mgombea mkuu wa CCM pili baada ya makosa mengi aliyofanya Lowassa baada ya kuwa akipiga kampeni dakika 5 karibia maeneo mengi pia kuchafuliwa kwa kashifa ya ufisadi.
 
Nimewauliza wanaccm wengi swali hili; kwanini mnaichagua ccm? majibu yake ni yale yale kama yakwako; Hakuna sababu ya msingi...ni hatari.
Sitakuja kupenda chama chochote Cha siasa Cha Tanzania by any means atanikikuuliza wewe kwanini unakipenda chama Cha Chadema wewe ujanijibu Nini?
 
Sitakuja kupenda chama chochote Cha siasa Cha Tanzania by any means atanikikuuliza wewe kwanini unakipenda chama Cha Chadema wewe ujanijibu Nini?
Nataka madiliko baada ya miaka 60 ya ccm. Nchi zilizoendelea zote ambazo tunawapigia magoti kuomba hela wanabadilisha chama kila baada ya miaka 4 au 8. Na sisi tunashangaa kwanini tunawakimbilia kuomba hela; tunapenda hela yao lakini hatupendi wanachofanya kupata hela hiyo.
 
Magufuli alipata nguvu kwa sababu ya ndio alikuwa mgombea mkuu wa CCM pili baada ya makosa mengi aliyofanya Lowassa baada ya kuwa akipiga kampeni dakika 5 karibia maeneo mengi pia kuchafuliwa kwa kashifa ya ufisadi.
Nimekuuliza sasa lengo lako ni nini ?! Hutaki apingwe kwenye uchaguzi ?!. Au ulitaka chama gani kimuwekee mgombea wa kumpinga !!
 
Nimekuuliza sasa lengo lako ni nini ?! Hutaki apingwe kwenye uchaguzi ?!. Au ulitaka chama gani kimuwekee mgombea wa kumpinga !!
Nashangaa unaniuliza swali la kipuuzi Kama Hili au kichwa nikigumu kuelewa kusoma kote thread yangu na umeshindwa kujua Nini nimelenga any way nilichoandika hapo Ni mtazamo au maono yangu ya uchaguzi wa mwaka Huu.
 
Je unavyoona wewe Chadema ndio itaisaidia hii iwe Tajiri?
 
Niambie Ni kwanini?
Mfumo wa ccm ni wa zamani tangu mwaka 1954. Watu wengi waliokulia kwenye mfumo huu walikuwa na lengo la kupigania uhuru wa nchi miaka ya 1960. Wengi chini ya Nyerere walikuja kuwa wajamaa. Huu ni mfumo maskini sana na mataifa waliyochukua mfumo huu walijikuta wakiwa maskini wakubwa e.g. Msumbiji, na nchi kadhaa za America ya Kusini.

Watu hawa kwenye mfumo wa ccm wamejenga himaya au genge lenye lengo la kujilinda wao wenyewe. Ukiwaunga mkono wanakupa nafasi kwenye genge lao. Wamezoea kutawala na kupata fedha kirahisi kwa njia ya madili ya serikalini. Hawajui biashara wala hawana ujuzi wa mikakati mbalimbali. Hawajui namna ya kujituma na kufanya kazi kwa maarifa, wamezoea kufanya mambo ili mradi wao wanafaidika haijalishi.

Ona jinsi viwanda vyote walivyoacha wakoloni vilivyokufa chini ya Mwalimu. Ona mashirika mbalimbali yaliyokuwepo, ni mengi sana siyataji hapa yalivyokufa, shirika la ndege, shirika la meli, mashamba ya mkonge, kahawa, hata korosho ona zinavyokosa soko, tumbaku, n.k. Watu kama akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, hawajawahi kufanya biashara na hawajui biashara, unafikiri mtu kama huyu atasimamia mgawanyo mzuri wa dili au mkataba wa madini? Kenya marais waliopita walikuwa watu wenye mashamba makubwa, mahoteli n.k, wanajua uchumi ni nini.

Chadema ina watu wanaojua uchumi na wao wenyewe wamewahi kufanya kazi nje ya siasa sio kama wana ccm ambao ni watu wa mtandao wa ccm tangu kuzaliwa wanapiga siasa tu. Usitegemee mtu huyo aweze kuleta mabadiliko na kunyanyua kilimo na biashara nchini, atakuwa mtu wa kukwapua tu vilivyo tayari mezani. Ndivyo walivyo ccm na hivyo tunahitaji akili mpya.
 
Umeandika vitu vya ukweli kabisa
Zile kura million 6 za lowasa sio za Chadema ni za ukawa
Ukitaka upate uhalisia subiri October CDM wakipata kura mil 3 wafanye sherehe kabisa

2015 vijana wengi walikuwa na hamasa ya kufanya mageuzi bila kujali mgombea ni nani?
Yule mkwele alifanya makosa mengi na ya wazi kabisa
Hadithi za EPA, KAGODA, RICHMOND, ESCROW, GES YA MTWARA,
mikataba ya IPTL, AGRECO,
KUKATIKA UMEME OVYO OVYO
MAJI HAKUNA
MAWAZIRI WAPIGAJI
RAIS MKWELE KUWA KAMA VASCO DAGAMA
BUNGE LA 2010 / 2015 Kutawaliwa na hoja za nguvu za upinzani
Haya yote yaliwatia hasira wananchi wakataka kufanya mageuzi
Mbowe akaja kuhalibu kabisa mageuzi
Tulipata kura mil 6 za hasira
Lakini uchaguzi huu 2020
Kwanza Rais ameshajulikana iwe isiwe
Pili upinzani umepararaizi
Vijana awana tena ile hamasa
Msije kushangaa kusikia wapiga kula wa 2020 awazidi mil 10


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umemezeeshwa propaganda Sana unaweza ukawa ukipendi Chams Cha CCM ila chadema ni kibovu kuliko hata CCM yenyewe tangu lini chadema wanajua uchumi? Lakini pia akina demokrasia Kama Ccm hiv umewahi kuona hata ilani ya CHADEMA? Ebu kuwa serious.
 
Kwanza kabisa me sio mpenzi wa vyama vya Siasa ila nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania.
Wewe ni m CCM kindakindaki. mnafahamika kwa kujivunia na kuusifu u dictator wa Jiwe, badala ya kuuonea haya.
Miaka minne bila ya chembe ya aibu, wengine mmewazuiwa kufanya siasa, lakini bado mnawaogopa.
Mnajijua pamoja na makelele na vitisho vyote, hamjaweza kugusa nyoyo za waTZ, 90% ya mnayofanya sio mahitaji yao ni yenu na mikogo yenu.
Kiburi chenu chatokana na tegemeo la kubebwa na walofaidika na teuzi na matumizi ovu ya vyombo vya dola.
Kama mwana ambae amekuwa akiandamwa na kuonewa na wazazi wake,mwaka huu HATUOGOPI tena.
 
Mzee una ushabiki maandazi
 
Umeandika mambo mengi wakati huwa mnapata msaada toka kwa Tume feki ya uchaguzi, na jeshi la polisi; hayo yote uliyoandika hayana maana.
40% ni mbali sana... 17%watajikamua sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…