CHADEMA wanakosea kwenye mpangilio wa kuomba Katiba Mpya

CHADEMA wanakosea kwenye mpangilio wa kuomba Katiba Mpya

Tindo endelea kuukimbiza UPEPO....

Suala la KATIBA mpya SI JIPYA....

Mbona hamkuvuruga baada ya mchakato ule kujifia mikononi mwa hayati mzee SITA?!!!

Hamkuwepo?!!!!

Mkuu endelea kuota njozi.....

Uchaguzi uliopita mliutengenezea "movies" za kura FEKI na ikathibitika JANJA YENU....

Hizo kura fake niliziona kwa macho yangu wala sihadithiwi. Tufanye kura ni fake, na ile kuengua wagombea wa upinzani kwa kiwango kile na zile sababu dhaifu nayo ilikuwa ni fake pia? Hata Afrika kusini makaburu walikuwa wanawadhihaki weusi kuwa kudai usawa ilikuwa ni kawaida yao, leo yako wapi? Soma alama za nyakati, Maguvu ya dola yana mwisho wake.
 
Mama pia ni binadamu mwenye madhaifu yake, naye anaweza kuchukia kama ambavyo mtu yeyote humu anaweza kuchukia. Lakini yeye akichukia tusisahau kuwa ndiye mwenye amri ya mwisho kuhusu vyombo vyetu vyenye silaha za moto (kwa mujibu wa katiba ya JMT)


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Nataka nijibu kipengere hiki tu


Ukiwa kiongozi wa watu hususani ktk ngazi ya Urais wa nchi, itakupasa kushughulika na mambo mengi sana, mojawapo ni dai la katiba mpya...

Watu na serikali wanadhani kwamba dai la Katiba mpya ya wananchi ni la CHADEMA lakini hii siyo kweli. Makundi mbalimbali ya kijamii yanadai hii kitu....

Ila CHADEMA sauti yao ndiyo inayosikika kwa mbali na ukali zaidi na kuwakera wenye mamlaka ya kiserikali na kuanza kutafuta njia mbalimbali kuzuia au kujaribu kukataa hili...

Anyway. Point yangu ni hii:

Mwitikio (reaction) ya serikali chini Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hili ni jambo muhimu sana...

Kuwa na mamlaka ya kiserikali, kuwa na nguvu za kijeshi na kuwa na bunduki, siyo ishu hata kidogo. Na ni KOSA KUBWA LA KIUFUNDI iwapo serikali itatumia nguvu yake hii kupambana na wananchi wake wasio na silaha kwa ishu ndogo ya "dai la katiba mpya" ambayo kimsingi ni ya kwao wananchi wala siyo ya watawala...

Nakuhakikishia jambo moja akitumia mamlaka yake vibaya kama unavyoshauri hapa (kuwa awe na hasira kama binadamu), ita backfire na moto huo utamla mwenyewe na wenzake na chama chake cha CCM....!

Anapaswa ajifunze kwa mtangulizi wake Mwendazake John P. Magufuli. Yeye kila dai toka kwa watu wake alilokuwa halipendi, approach yake ilikuwa ni lugha kwa lugha kali ya matusi, ubabe, violence, yaani piga, umiza, poteza, ua nk nk. Kilichomkuta, wote tunajua...

Hii haifai, tusimshauri Rais kuwa na hasira maana hasira ni hasara...
 
Saccos ya CHADEMA ni sikio la kufa.....

Hiki chama cha VICOBA kinamlazimishaje Rais wa Kiafrika?!!!

Tanzania si nchi ya KILIBERALI....

#KaziIendelee
"Atake asitake mi5 tena" mlivyokuwa mnatamka haya maneno mlidhani hii ni nchi ya kiliberali? Kwa nini asilazimishwe wakati sisi ndio tumemuweka hapo alipo? Ndio maana tunasema katiba mpya haiepukiki kwa vile Rais amekuwa na mamlaka makubwa kama Mungu
 
Katiba mpya ndio mwisho wa CCM, hilo mnalijua na ndio sababu mnaogopa!
 
Mimi ni mdau ambaye naunga mkono sana mabadiliko ya Katiba lakini mpangilio wa sasa ambao unaongozwa na CHADEMA sijaupenda na hautasaidia mafanikio haya kwasababu zifuatazo

1. Rais mpya Samia hawezi kukubali kufanya katiba wakati mapema kwa kuzingatia ameingia majuzi tu na kachukuwa madaraka kwenye wakati mgumu kwa mtangulizi wake kupoteza maisha. Hii kwa nchi nyingine ambazo hazina usalama wangeweka " state of emergency" ingawa hatukufika huko Rais anahitaji muda kwanza kupata nguvu na kuungwa mkono kabla ya kudandia suala nyeti na lenye kugawanya watu kama katiba mpya.

2. Corona ni ugojwa ni sio kitu cha kisiasa. Huu ni ugojwa na kuna Watanzania wengi wamepoteza ndugu wengi kuanzia mwaka 2019. Tuliulize ni kitu gani kimetokea kusababisha haya? jibu ni Corona. Corona imeondoa watu wengine ambao hata familia hazijui wamekufa kwanini. Kuna watu wawili ambao nina mfano mmoja ni rafiki yangu wa Ilboru ambaye alikuwa anamiliki mgodi kule Mererani kwenye wimbi la pili alikufa ghafla wakidai alikosa pumzi na kafariki wa kisukari. Familia ikadai apimwe Corona maana alikuwa na miaka 44 tu na sukari yake haikuwa mbaya hivyo! Walivyopima zaidi ya mara moja wakakuta ana Corona.

Juzi pia mzazi wa rafiki yangu naye sukari imepanda akafariki Musoma baada ya familia kulazimisha apimwe wamekuta naye alikufa kwa Corona ingawa kabla ya kupima walisema sukari imepanda. Kwa ufupi huu sio wakati mzuri wa kufanya makusanyiko yoyote yasiyo ya lazima. Kwa msingi huu naunga mkono Rais Samia kwamba huu sio wakati mzuri wa kuanzisha mikutano ambayo inaweza kuongeza na sio kuzuia Corona.

3. Mkutano na Rais: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Rais Samia unamfanya Rais aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua. Chadema kwa faida za nchi na kisiasa wanatakiwa kuweka urafiki na Rais na sio kufanya mkutano kama unaenda kukutana na watekaji wako.

Mama anapenda sana umoja, yeye pekee ndiye alienda kumwangalia Lissu Kenya makusudi bila hata kumwambia kiongozi wake Magu. Hata safari ya Kenya inawezekana alilazimisha kwenda Kenya ili akamuone Lissu bila kuwaambia nia yake Chama.

Haya yote kafanya ili Chadema wajue na yeye binafsi aweke rekodi kwamba yeye kama Samia hajahusika kwenye njama zozote za kumuumiza Lissu. Cha ajabu chadema pamoja na kuwa na mtu ambaye ataweza kufanya nao kazi wanataka wampime kijinga kwa kuweka maandamano ambayo yatawasaidia wale ndani ya CCM wanaotafuta sababu za kuwapiga upinzani kwa faida zao.

Chadema ni lazima wajue kule CCM kuna wengi walikuwa wananufaika na biashara za upinzani ilikwa ni pamoja na kutumia pesa za kununua wapinzani nje ya utaratibu, kuunda vikundi vya ajabu, kuomba pesa za teknologia za kurekodi watu, hizo zote ni biashara za mabilioni ambazo Chadema kwa kuleta mikutano ya ajabu itawapa sababu hawa walaji kwenda kwenye chama na kuanza tena kuchukua pesa baada ya kumuogopesha Rais
Naunga mkono hoja
 
Mimi nashauri namna ya kudai katiba , sijasema ssh hana makosa.
Angalau anaachia mwanya watu wapumue. Ni muhimu kutumia huu mwanya kwa hesabu makini la sivyo kuna uwezekano tukapata kiongozi wa kwanza wa kiislam katili(Mwinyi na Kikwete walikuwa waungwana sana) . Na sababu zipo wazi - amefanya kazi bega kwa bega na dikteta hivyo kumuiga ni swala la kubonyeza batan tu. Si umeona ameanza hotuba za kwenye magari! Kinachofata ataanza kugawa hela barabarani kwani nyuma yake kuna nguvu kubwa ya genge linalofurahia udikteta.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

..Asante.

..mimi ninachopendekeza ni kwamba tuwe balanced.

..raisi akikosea akosolewe, na wapinzani vilevile.
 
Fk u ,mnaiba na kuua shnz type ....Safari hii hamna k2
Uchaguzi wa kishenzi kwako....si kwangu....

Tindo utaendelea kulalamika mpaka uzee wako.....

CCM ni chama cha KIJAMAA....na wajamaa tunaposhika hatamu basi "tutalaumiwa nanyi kila uchao".....

#KaziIendelee
#KatibaYetuNiBofk u
 
Back
Top Bottom