MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Siasa zina mbinu nyingi katika ushindi. Moja ya mbinu ni kujua adui wako ana silaha za aina gani kabla haujaingia kwenye mapambano!
Kwa mfano, Miaka ya nyuma, wapinzani walikuwa wanasubiri kwanza CCM iteuwe wagombea wake ili waliokatwa wajiunge kwenye vyama vyao. Kwa kutumia mbinu hii, vyama vya upinzani vilikuwa vinanufaika na kuongeza ruzuku.
Mwaka huu, CCM waliamua kutangaza wagombea wao siku nne kabla ya zoezi la kuchukua fomu na kurudisha halijafungwa. Mbinu hii kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kwa sababu hata wale waliojiunga upinzani baada ya kukatwa wamejikuta katika wakati mgumu kutimiza malengo yao. Mfano mmojawapo ni aliyekuwa Mbunge wa CCM katika Jimbo la Nachingwea, Hassan Masala ambaye alijiunga ACT-Wazalendo baada ya jina lake kukatwa, jana ameamua tena kurudi CCM.
Inasemekana CHADEMA kwa sasa wanasubiri kwanza CCM watoe Ilani yao ya Uchaguzi 2020-2025 ili waisome na baadaye warekebishe Ilani yao katika maeneo ambayo wanadhani CCM hawakuyagusa au wameyagusa lakini sio kwa undani zaidi. CHADEMA wanachofanya ni kutengeneza mazingira ya kujibu mapigo ya Ilani ya CCM. Hii ni mbinu nzuri ya kivita pamoja na kwamba ina matatizo yake ambayo kwangu nayaona hayana athari ukilinganisha na faida zake.
Je, CCM watazindua Ilani yao ya Uchaguzi kesho au nao watasubiri/kuahilisha kama ambavyo CHADEMA wanafanya?.
Tusubiri Kesho katika Uzinduzi wa kampeni za CCM kupata jibu sahihi!