Uchaguzi 2020 CHADEMA wanaweza wasipate Wabunge

pasi padinde

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
281
Reaction score
299
Upepo unaonesha kwamba chadema wanaweza wasipate hata mbunge lakini watakacho kipanda kwa watanzania kitakuwa kikubwa sana .

Mtu anaekuweka moyoni ni wa maana sana kuliko mnafiki anaekuchekea.

Agenda kubwa ya cdm itakuwa Tume huru na yakiyotokea katika utawala wa awamu ya Tano.

Watakumbushwa watanzania mengi waliyotendewa bila huruma.

Mfano
Bomoabomoa
Tetemeko
Utekaji uuwaji
Vijana kufukuzwa udom na wengine watoto wa wakubwa kuendelea kusoma
Freedom of speach
Fungafunga kwa wapinzani
Kuzimwa kwa Bunge
Matumizi ya kubambikia kesi

Yapo mengi yataelezwa na watanzania watayasikia na yatakaa moyoni. Athari ya kitu kinachokaa moyoni huwa hakitoki kwa haraka na kina kuwa na matokeo mabaya mbeleni.

Tundu lissu anaweza akawa mtego mkubwa sana katika uchaguzi huu ikiwa ccm wataanza kumsumbua. Ombi langu katika jicho la tatu nionalo ni kwamba wamwache aseme tu mwisho atazoeleka na ayasemayo hayatakuwa na athari yeyote kuliko akisumbuliwa.

Ikiwa ccm wataiba kura tujitayarishe kuona tukio baya sana kwasababu cdm wameshajua mipango ya CCM na huwezi jua plan yao kubwa ni ipi. Yaani ukiwa unaelewa kwamba naenda kufanya mtihani alafu mtihani wangu utapokonywa ili apewe asie mwingine na bado pamoja na kujua unaenda tu kufanya mtihani , tegemea huyu anaefanya mtihani ananjia mbadala.

Tatizo la ccm viongozi wanadhani kuwafanyia hofu na vitisho wanaccm wezao kutafanya wawe watiifu. Kwanza sio kila aliehamia ccm ni mwana ccm wengine ni mamluki kwenda kuleta siri kwa upinzani. Pili CCM itaangushwa na wanaccm wenyewe . Mchana ccm lakini usiku upinzani.

Mwisho mkuu wa nchi kaa na viongozi wa upinzani usikatae kuambiwa ukweli hata kama utakuudhi kuliko kupenda kusikia wanaokupigia makofi hata ukinywa maji tu.

Nchi itajengwa na wananchi sio na wazungu.
Tukae tuelewane ili tusiruhusu weupe watugawe.

Nawaza tu
 
Mgombea wenu keshaanza mazoezi?


KONYAGI-FAHARI YA WATANZANIA
 
Title yako haiko vizuri, jaribu kuiweka vizuri iendane na maudhui yaliyomo.

Umeelezea vizuri lakini title inakinzana.
 
Title yako haiko vizuri, jaribu kuiweka vizuri iendane na maudhui yaliyomo.

Umeelezea vizuri lakini title inakinzana.

Ahsante.
Nimefanya hivyo ili iwe chambo machoni pa wasomaji. Uandishi una njia nyingi kuvutia walengwa
 
Mfano
Bomoabomoa
Tetemeko
Utekaji uuwaji
Vijana kufukuzwa udom na wengine watoto wa wakubwa kuendelea kusoma
Freedom of speach
Fungafunga kwa wapinzani
Kuzimwa kwa Bunge
Matumizi ya kubambikia kesi
Hoja nyepesi sana hizi,hazimgusi kabisa mwananchi wa muhambwe au nyakwale
 
Hoja nyepesi sana hizi,hazimgusi kabisa mwananchi wa muhambwe au nyakwale

Inategemea zitaelezwaje. Wepesi wa kusoma sio wepesi wa kuwasilisha kwa wananchi.
Labda hujawahi kutana na mafundi wa majukwaa ikichanganya na emotional behavior
 
_ (Biashara, Elimu, Kilimo, Afya, Miundombinu, Ajira) Hivi ndivyo vitu majority ya watu wanataka wavisikie. Na ndio matatizo halisi(actual) ya wananchi.

_ Mambo ya kufikirika ( kama uliyotaja hapo juu) umuhimu wake utaonekana pale tu ambapo vitu tajwa hapo juu vitakua si tatizo kwa wananchi.
 
Inategemea zitaelezwaje. Wepesi wa kusoma sio wepesi wa kuwasilisha kwa wananchi.
Labda hujawahi kutana na mafundi wa majukwaa ikichanganya na emotional behavior
Labda kama watatumia uongo wa msigwa
Unamueleza mpiga kura kuminywa demokrasia,huku umesimama jukwaani atakuelewa kweli?
 
Tuliona ya uchaguzi wa mitaa😂😂😂 kama mambo ni yale yale basi hata CUF hawatapata mbunge
 
Huku mnasema mnajiamini, huku mnaweweseka CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO (chadema)

Mmekuwaje mbona mmekata tamaa dakika za mwanzo.

Hayo yote uliyotaja kwa ujumla ndio yalikuwa matatizo ya nchi yetu, ukiongeza na hili la wimbi la wanasiasa wapiga deal!

Mnajaribu kuichonganisha serikali ya awamu ya tano, kuanzia watumishi,walimu,mafao nk.

Lakini mmegonga mwamba.

Jiandaeni kisaikolojia kazi kwenu.

VIVA JPM 2020 - 2025[emoji1241]
 
Naskia fomu imetoka moja tu,mmeogopa kutolewa bandama
 
Inashangaza kumwona kijana mwenye akili timamu akishabikia ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…