pasi padinde
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 281
- 299
Upepo unaonesha kwamba chadema wanaweza wasipate hata mbunge lakini watakacho kipanda kwa watanzania kitakuwa kikubwa sana .
Mtu anaekuweka moyoni ni wa maana sana kuliko mnafiki anaekuchekea.
Agenda kubwa ya cdm itakuwa Tume huru na yakiyotokea katika utawala wa awamu ya Tano.
Watakumbushwa watanzania mengi waliyotendewa bila huruma.
Mfano
Bomoabomoa
Tetemeko
Utekaji uuwaji
Vijana kufukuzwa udom na wengine watoto wa wakubwa kuendelea kusoma
Freedom of speach
Fungafunga kwa wapinzani
Kuzimwa kwa Bunge
Matumizi ya kubambikia kesi
Yapo mengi yataelezwa na watanzania watayasikia na yatakaa moyoni. Athari ya kitu kinachokaa moyoni huwa hakitoki kwa haraka na kina kuwa na matokeo mabaya mbeleni.
Tundu lissu anaweza akawa mtego mkubwa sana katika uchaguzi huu ikiwa ccm wataanza kumsumbua. Ombi langu katika jicho la tatu nionalo ni kwamba wamwache aseme tu mwisho atazoeleka na ayasemayo hayatakuwa na athari yeyote kuliko akisumbuliwa.
Ikiwa ccm wataiba kura tujitayarishe kuona tukio baya sana kwasababu cdm wameshajua mipango ya CCM na huwezi jua plan yao kubwa ni ipi. Yaani ukiwa unaelewa kwamba naenda kufanya mtihani alafu mtihani wangu utapokonywa ili apewe asie mwingine na bado pamoja na kujua unaenda tu kufanya mtihani , tegemea huyu anaefanya mtihani ananjia mbadala.
Tatizo la ccm viongozi wanadhani kuwafanyia hofu na vitisho wanaccm wezao kutafanya wawe watiifu. Kwanza sio kila aliehamia ccm ni mwana ccm wengine ni mamluki kwenda kuleta siri kwa upinzani. Pili CCM itaangushwa na wanaccm wenyewe . Mchana ccm lakini usiku upinzani.
Mwisho mkuu wa nchi kaa na viongozi wa upinzani usikatae kuambiwa ukweli hata kama utakuudhi kuliko kupenda kusikia wanaokupigia makofi hata ukinywa maji tu.
Nchi itajengwa na wananchi sio na wazungu.
Tukae tuelewane ili tusiruhusu weupe watugawe.
Nawaza tu