Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Na Dr.Zack
Sababu zilizoletwa na CHADEMA ili kushinikiza kusitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu la chama hicho imeibua maswali mengi kwa Wajumbe kikao hicho wakidai kuwa suala la viongozi kuitwa mahakamani hazionekani uhalisia wa kuhairishwa kwa kikao hicho muhimu cha Kikatiba.
Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Moshi na Tanga walidai kuwa hawaungi mkono kusitishwa kwa kikao hicho kwa kueleza kuwa hoja hiyo ina mapungufu kwa sababu si viongozi wote wakuu walioitwa Mahakamani kutoa ushahidi bali ni wachache tu,ambapo hakumaanishi kwamba shughuli za Baraza Kuu haziwezi kuendelea, hasa pale ambapo viongozi wengine wenye mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya chama bado wapo.
Miongoni mwao viongozi wenye uwezo wa kuendesha vikao hivho ni ni Amani Golugwa, Rugemeleza Nshalla, Godbless Lema na Rose Mayemba, ambao wote ni wajumbe wa Kamati Kuu na wana nafasi katika kuratibu shughuli za chama kwa mujibu wa taratibu zake.
Swali kubwa wanalojiuliza wajumbe hao wa Baraza Kuu ni kwa nini kikao kizima cha Baraza Kuu kisitishwe kwa sababu ya viongozi wachache ambao wanahitajika katika mchakato wa mahakama, wakati viongozi wengine wanaotambuliwa na Katiba bado wapo?
Mwisho : Kutoa ushahidi mahakamani ni wajibu wa mtu binafsi katika mchakato wa kisheria, lakini haimaanishi moja kwa moja kwamba taasisi nzima anayowakilisha haiwezi kuendelea na majukumu yake kupitia viongozi wengine wenye mamlaka.