Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimetoa rasmi tamko mara baada ya baadhi ya viongozi wake kukamatwa na Jeshi La Polisi wakati wakiwa wanaandamana.
Tamko la CHADEMA linakuja saa chache tangu viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Godbless Lema kutiwa mbaroni na Jeshi La Polisi katika nyakati tofauti tofauti jijini Dar Es Salaam.
Kwenye tamko lao lililochapishwa kupitia mtandao wa X, CHADEMA walidokeza kuwa polisi walitumia nguvu nyingi sana kudhibiti maandamano hayo yalikuwa na lengo la kupaza sauti kuhusu uchunguzi wa baadhi ya watu waliotekwa na kuuwawa.
READ ALSO: Maandamano Ya CHADEMA: Jeshi La Polisi lathibitisha kukamata waandamanaji 14 ikiwemo viongozi wa CHADEMA
Aidha CHADEMA, imelitaka Jeshi la Polisi kuheshimu haki zote za waliokamatwa na kuwatendea kama watu ambao sio wahalifu kwa wakati wote wa kushikiliwa kwao.