CHADEMA ya Lowassa ilikuwa bora kuliko ya Slaa ?

CHADEMA ya Lowassa ilikuwa bora kuliko ya Slaa ?

Watu walikuwa wameichoka CCM ya 2015 ya JPM kuliko CCM ya 2010 ya JK?

Kwa hiyo kama Lowassa angesimamishwa na CCM halafu Slaa angegombea kupitia CHADEMA slaa angeweza hata kushinda?
Wewe unafikiri CCM wenyewe walikuwa wajinga kuntupilia mbali Lowassa wakati alikuwa na wafuasi wengi kuliko wagombea wote waliokuwa wamejitokeza? CCM waliisha fanya tafiti zao na kuonekana wakimleta Lowassa kuwa mgombea wao watapata shida sana kumnadi kwa sababu ya tuhuma zake ambazo Yeye mwenyewe hakuwai kuzikana,na Slaa alikuwa ameisha handaa makombora mazito,hivo Lowassa kumshida Slaa ingelikuwa kipengele.
 
Lowassa alikuwa hawezi kushinda sababu alikuwa na tuhuma nyingi kuliko Magufuli, lakini hata hivyo kipindi hicho ungeliweka mgombea wa CCM na jiwe watu wangelipigia jiwe, CCM ilikuwa imechokwa vibaya mno,Slaa alikuwa ameisuka chadema vibaya mno.
Alikuwa ameisuka chadema vizuri mno, au vibaya mno?!
 
Lowassa alikuta chadema imeisha tengenezwa na Slaa,na kama hisingelikuwa tamaa za Mbowe na Lissu wake kumzunguka Slaa hata kama CCM ingelishinda, chadema ingeliendelea kuwa na nguvu zake kama 2015 hata na kuzidi, Maana kipindi hicho CCM ilikuwa imechokwa vibaya mno hadi kuonekana umevaa nguo za kijani unazomewa, CCM wenyewe walikuwa wanavalia kwenye mikutano yao hikiisha wanavu kuficha aibu.nilivyoona Mbowe na Lissu wamemkubali Lowassa kuwa mgombea wao tokea hapo niliona Mbowe ni mfanyabiashara sio mwanasiasa makini, mpaka Sasahivi siwezi amini chadema ya Mbowe na Lissu ni wanasiasa makanjanja.
UZI UFUNGWE.NO COMMENTS
 
Kwahiyo tunakubaliana na kile ambacho huaga kinatangazwaga na NEC? Bado mimi naamini both Dr. Slaa na Lowasa walishinda but hawakutangazwa
 
Kwa nini Lowassa (mtuhumiwa wa fisadi) alipata kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuliko alizipoata Willibrod Slaa (msafi) mwaka 2010?

Ni mvuto wa kisiasa, pesa, sera, upadri wa Slaa au kitu gani kilicholeta matukio ya kuchanganya hivyo?
CDM ya lowasa ilikuwa si bora kama ya slaa
 
Back
Top Bottom