Pre GE2025 CHADEMA yadai kuzuiwa kufanya Mkutano katika kumbi za Hoteli ya Sea Cliff, uliopangwa kufanyika leo, Februari 27, 2025 Dar

Pre GE2025 CHADEMA yadai kuzuiwa kufanya Mkutano katika kumbi za Hoteli ya Sea Cliff, uliopangwa kufanyika leo, Februari 27, 2025 Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mara Chadema haina hela,mara ina hela inachezea ,bado hamjasema,ndio kwanza kazi inaanza leo,No reform no election
Aliyesema Chadema haina hela ni mwenyekiti wenu wa Taifa Tundu Lisu sio CCM

Sasa hizo pesa za kwenda kufanya kikao hotel ya mamilioni pesa mumetoa wapi?
Tunaomba jibu je Chadema ina hela au haina? Jibuni

Tqking into consideration hicho kikao kufanyika hotel kubwa la mamilioni la kitalii
 
Chai na vitumbua asubuhi katika Ikulu Ndogo Tanga, kabla ya kuanza kazi kuelekea Muheza na kisha Mkinga kuzungumza na wananchi na kuhusu kazi, na namna zaidi ya Shilingi Trilioni 3.1 toka serikalini kuja Mkoa wa Tanga zilivyobadili maisha yao kupitia miradi mbalimbali katika kipindi cha miaka minne.
 
Aliyesema Chadema haina hela ni mwenyekiti wenu wa Taifa Tundu Lisu sio CCM

Sasa hizo pesa za kwenda kufanya kikao hotel ya mamilioni pesa mumetoa wapi?
Tunaomba jibu je Chadema ina hela au haina? Jibuni
Unatuhoji wewe kama nani?
 
Unajua anayeungana adui yako sio rafiki yako Bali adui?
Ni kweli lakini kwa mazingira ya Tanzania ukisema ufanye hivyo utakuwa unakosea maana sheria zetu hazipo huru na bado haki haijapata sauti. Vyema sana kuweka nguvu kwa adui sahihi
 
"Nilimwambia dr slaa atulie abaki CHADEMA kwa sababu hata LOWASA angeshinda 2015 asingetangazwa "( Prof. Safar)
Tatitizo ni mfumo mbaya wa uchaguzi
Wanawalazimisha watu kuwaza kulishawishi Jeshi lichukue nchi.
 
Huu ni uonevu wa wazi kabisa unaofanywa na watu wanaojitapa na kuwadanganya Watanzania kuwa mwaka jana wamerekebisha Sheria za Uchaguzi na Demokrasia.

Huu ni uthibitisho kuwa Tanzania hakuna demokrasia na siasa zinafanywa kuwapendelea CCM tu.

Huu ni uthibitisho kuwa CCM wanafanya uonevu wa wazi hivyo mwaka huu vyovyote vile tuwaombe wenye akili na wanaoguswa na haya kwenye vyombo vya ulinzi wa Usalama watusaidie kweli kuwaambia CCM kuwa There Should be No Election this Year Without Reforms.
View attachment 3251842
Gentleman,
kwa mujibu wa katiba ya nchi,
uchaguzi mkuu huru, wa wazi na wa haki zaidi utafanyika October mwaka huu 2025 bila mbambamba, kelele au mdomo wa kibaka au tapeli yeyote wa kisiasa nchini 🐒
 
Halafu kuna mtu anakaza magego tushiriki uchaguzi
Mimi tangu uchaguzi wa 2015 upite na matokeo kugeuzwa juu chini, chini juu! Niliapa sitokuja tena kupoteza muda wangu. Siku tukifanikiwa kuwa na Katiba ya wananchi pamoja na tume huru ya uchaguzi (achana na hii takataka iliyobadilishwa tu jina) ndipo nitarudi tena kushiriki.
 
Wanawalazimisha watu kuwaza kulishawishi Jeshi lichukue nchi.
Mkuu watu wenyewe sasa? Sasa hivi wameletewa kubet, mziki na mpira mchana kutwa watu wana jadili haya mambo. Watajadili changamoto zao lini??
 
Gentleman,
kwa mujibu wa katiba ya nchi,
uchaguzi mkuu huru, wa wazi na wa haki zaidi utafanyika October mwaka huu 2025 bila mbambamba, kelele au mdomo wa kibaka au tapeli yeyote wa kisiasa nchini 🐒
Endeleeni tu kuchezea kodi za wananchi walalahoi wa nchi hii. Ipo siku mtazitapika.
 
Back
Top Bottom