LGE2024 CHADEMA yaitisha Kikao cha dharura cha Kamati Kuu kujadili matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika kikao cha dharura kesho, Ijumaa tarehe 29 Novemba 2024. Kikao hicho kitajadili matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024 na kutoa msimamo rasmi wa Chama. Mwenyekiti wa Chama, Mhe. Freeman Mbowe, atakiongoza kikao hicho, na kauli rasmi itatolewa baada ya kikao kumalizika.

 
Tusubirie mapuvu toka kwa Lema na Mzee Mbowe ambao ndio chanzo kikuu kwa hii SACCOS kujifia taratiibu
 
asante kwa taarifa, tutafuatilia怂
P
 
Wamechelewa tuliwaambia humu waachane na huo upuuzi huo haukuwa na dalili ya kuwa uchaguzi hasa kwa hiyo tume iliyojaa makada watiifu wa CCM.
 
Mhuni ni huyo aliyekuzaa , maana like begets like and therefore ulizaliwa na wahuni nawe lazima uwe muhuni, asiye muhuni hawezi kuandika ujinga huu
Mkuu naona umevimba baada ya kusikia wahuni wameguswa
 
Hiki chama bwana kama kikundi fulani hivi cha wahuni waliojichokea maisha kisha kuungana kurudi kwenye Maisha
Ingekua ni hivyo isingetumika nguvu kubwa kukizima , kingepotezewa tu kama chaumašŸ¤”
 
Hakuna jipya
 
Baada ya kikao.

Kama kawaida ni yale yale.

Tumedhulumiwa.

Watu wetu wameumizwa.

Watu wetu wamekufa.

Uchaguzi umebagazwa.

Ule sio uchaguzi ni uchafuzi.

Tumekamata makaratasi ya kura feki.

CCM wanategemea polisi.

Tunataka tume huru.

Tunataka katiba mpya.

Baada ya wiki Mbowe anachukua chake maisha yanaendelea.
 
".....tutakwenda nao(CCM) kimlalo mlalo hadi mwisho...." by Elikaeli Mbowe.

Mbona bado mapema sasa? Hiyo kimlalo mlalo uliyosema mbona bado Sana?
Chadema kuweni makini na Mbowe, bado hamjachelewa Sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…