PreGE2025 CHADEMA yaitisha Kikao cha Kamati Kuu Mei 21, Baraza Kuu lanukia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam Jumatano Mei 21, 2025.

Kikao hicho kimeitishwa kipindi ambacho chama hicho kinapitia misukosuko ikiwemo ya mwenyekiti wake, Tundu Lissu kuwa gerezani akikabiliwa na kesi mbili ya uhaini na ya kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Pia, makada na viongozi wake kuanzia ngazi ya kamati kuu, kanda, mikoa, wilaya, majimbo hadi kata wakitangaza kukihama kwa madai kimepoteza mwelekeo.

Aidha, kamati kuu hiyo imeitishwa kipindi ambacho Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imeiandikia barua Chadema ya kuwaeleza kutokuwatambua viongozi wanane wa kamati kuu na sekretarieti.

Hiyo inatokana na kudai akidi ya Baraza Kuu la Januari 22, 2025 haikutimia na kuwataka kuitisha upya baraza hilo. Miongoni mwa viongozi hao ni Katibu Mkuu, John Mnyika na naibu wake wawili Bara na Zanzibar.

Aidha, kikao hicho kimeitishwa Makamu Mwenyekiti wake Bara, John Heche kipindi ambacho makada na viongozi wake wanaokikimbia wakieleza Heche ameshindwa kukiongoza vyema kwa vikao badala yake kimekuwa cha matamko.

Siku moja kupita yaani jana Ijumaa, Mei 16, 2025, Heche akizungumza na wanachama wa Chadema Famili Kijiji cha Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika kikao cha ndani alitangaza uwepo wa kikao hicho.

Amesema kikao hicho kitajadili mambo kadhaa ya ustawi na mikakati ya chama ikiwemo muendelezo wa kampeni ya No reforms, no election 'bila mabadiliko hakuna uchaguzi' ambayo imefanyika kanda mbalimbali za chama hicho.

"Kuna watu eti wanadai Chadema inakufa...Chadema hii hii tunayoitisha mkutano wa hadhara saa 2:00 asubuhi na watu wanajitokeza hadi mtu unakosa pa kukanya ndio inakufa? Wanajidanganya sana," amesema Heche

Bila kutaja ajenda za kikao hicho, Heche amesema: Mei 19, 2025 tunaenda Mahakama ya Kisutu kwenye kesi ya Mwenyekiti wetu Tundu Lissu na Mei 21 tutafanya kikao cha Kamati Kuu. Baada ya hapo tutaueleza umma nini kinafuata. Chadema siyo tu ni chama cha siasa, Chadema ni imani katika mioyo ya Watanzania wapenda haki na demokrasia."

Chanzo: Mwananchi
 
Baada ya kushutumiwa na mmoja wawajumbe ex. CDM kuwa hakijawahi kufanyika!

Amandla...
 
Wajumbe wa hiyo kamati kuu watakuwa nani? Akidi itaenea? Sababu kuna wale nane wameenguliwa na msajili kuwa hawatambui.

Kuna wanaojitoa CHADEMA. Awe makini asizalishe tatizo juu ya tatizo
 
Sidhani kama unajielewa.
 
Heche ni bingwa wa mihemko sijui hicho kikao kitajadili nini zaidi ya tone tone.
 
Back
Top Bottom