CHADEMA yajibu hatua ya Mbunge Cecil Mwambe, kusoma Ilani ya CCM Bungeni

CHADEMA yajibu hatua ya Mbunge Cecil Mwambe, kusoma Ilani ya CCM Bungeni

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetetea hatua ya Mbunge wake jimbo la Ndanda Cecil Mwambe kuingia na ilani Ya Chama cha Mapinduzi bungeni kwa kile ilichokisema ni jambo la kawaida.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema amewataka watu wasishangae kwani Chama hicho kinawahamasisha wabunge wake kusoma ilani ya (CCM) ili kujua namna gani ambavyo Chama hicho tawala kinatekeleza ilani ahadi.

"Ni jambo la kawaida sana, sisi kama chama tunawahamasisha wabunge wetu kusoma, ndio maana huyo huyo Mwambe wiki iliyopita ulimuona akimpa sera Mbadala za Chama moja ya mawaziri Bungeni", amesema Mrema.

Aidha, amesema "kuingia na ilani ya Chama cha Mapinduzi si tatizo kwa sababu hata ukija ofisini kwetu utakutana na ilani ya CCM kwa hiyo kama angekuwa na nia ya kuhama chama, angehama kimya kimya kama wanavyofanya wengine".

Leo Novemba 14, 2018 akiongoza vikao vya bunge, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, amesema mheshimiwa Cecil Mwambe anasoma sana ilani ya Chama cha Mapinduzi, siku hizi baada ya kugundua ina mambo mazuri sana.View attachment 933813
sawa huko nako ni kuongeza madini kichwani
 
Huyo Mrema anajua nini kipo moyoni kwa Mwambe?

Ni maelezo dhaifu sana. Kwa nn asiseme Mwambe mwenyewe?
 
Mbona ikulu ilipotembelewa na Rostam, kurugenzi kuu ikaitaarifu nchi? Wacha uwendawazimu.
Ha haaaaa..... Rostam mlisema ni rafiki wa lowassa, leo mtasema nini? Kwa kahama chama cha lowassa nini jamani.
 
Back
Top Bottom