OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Polisi wametoa taarifa leo walizoita za uhakika kwamba wamepata taarifa Viongozi wa CHADEMA wamefanya kikao kwa njia ya zoom na kuhamasisha Wafuasi wetu kwenda Ofisi mbalimbali za Serikali na kuhamasisha Vijana kwenda Vituo vya Polisi na wakasema atakayekwenda kwenye Vituo vya Polisi atashughulikiwa kwa haraka sana”
“Kauli hii ya Polisi tumeichukulia kwa uzito mkubwa sana kwasababu August 09,2024 Polisi walitoa kauli kama hiyo wakati Vijana wakijiandaa kuadhimisha Siku ya Vijana kule Mbeya August 12,2024 na baada ya kauli hiyo Viongozi wetu walianza kukamatwa wakaumizwa vibaya na Vijana wetu wengine wakakamatwa ndio maana tumeona kauli hii tusiiache iendelee kubaki hata kwa dakika moja kwasababu kwanza ni kauli ya uongo lakini pili ni kauli ambayo ni hatari na inahatarisha usalama wa Viongozi na Wanachama wa CHADEMA”
“Tangu hukumu ya Mahakama Kuu tarehe 28 hakuna kikao chochote kilichofanyika kuanzia kwa zoom au cha kawaida, kwahiyo Polisi kutoa kauli kama hii ya kizushi na ambayo inasababisha taharuki kwa Umma, tunalitaka Jeshi la Polisi wathibitishe kauli yao kwasababu ni jaribio lingine la kunyanyapaa Viongozi wa CHADEMA kutufanya Wahalifu wakati CHADEMA sio Chama cha kihalifu, vilevile tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ushahidi hadharani” —— Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo August 30,2024
Soma Pia: Jeshi la Polisi: Tumepata taarifa CHADEMA wanapanga Maandamano na Kuvamia Vituo vya Polisi Dar kwa wakati mmoja
My Take
Imagine nchi inakuwa na chombo muhimu kama hiki halafu ndio kiwanda kikuu cha uongo