Chadema yalaani Kuzuiliwa kwa Gobless Lema mpakani Namanga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Ikumbukwe kwamba kuna amri ya Haramu iliyotolewa na viongozi wa Tanzania ya kuzuia Viongozi wa Chadema kusafiri Nje ya Nchi.

Nabii huyo wa Mungu amenyang'anywa Passport yake na kutakiwa kuripoti Uhamiaji Makao Makuu Dodoma ikiwa ana Malalamiko yoyote.

Taarifa ya Chama hicho iliyosambazwa kote Duniani hii hapa
============
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga vikali kitendo kisicho halali na chenye msukumo wa kisiasa cha kumkamata Mheshimiwa Godbless Lema, mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, ambaye leo amezuiwa kwa njia isiyo ya haki na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania katika mpaka wa Namanga akiwa safarini binafsi kuelekea Nairobi, Kenya.

Maafisa wa uhamiaji waliomzuia walimueleza kuwa walikuwa wakitekeleza “maelekezo kutoka juu” kuzuia viongozi wa CHADEMA kusafiri nje ya mipaka ya Tanzania—kauli inayotia hofu kubwa inayoashiria matumizi mabaya ya mamlaka ya dola kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kisiasa. Pasipoti yake ilichukuliwa na kwa sasa anazuiliwa katika Ofisi ya Uhamiaji Namanga bila kufuata taratibu za kisheria.

Tunasema wazi: hakuna msingi wowote wa kisheria wa kumzuia Mh. Lema au kumzuia kutoka nje ya nchi. Uhuru wa kusafiri ni haki ya msingi inayotambuliwa na sheria za Tanzania na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.

Soma Pia: Godless Lema: Nimekwama kwenda Nairobi kutokana na zuio la Viongozi wa CHADEMA kusafiri nje ya nchi

Tunamtaka Mheshimiwa Godbless Lema aachiwe mara moja bila masharti yoyote, arejeshewe pasipoti yake, na kukomezwa kwa aina zote za unyanyasaji na ufuatiliaji dhidi ya viongozi wa upinzani. Hili si suala la Godbless Lema pekee, bali ni suala la kulinda heshima, utu na haki za kikatiba za Watanzania wote. Tunatoa wito kwa wananchi, asasi za kiraia, na washirika wa kimataifa kusimama kidete dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka kama haya.

Screenshot_2025-06-06-17-05-43-1.png
 
Ikumbukwe kwamba kuna amri ya Haramu iliyotolewa na viongozi wa Tanzania ya kuzuia Viongozi wa Chadema kusafiri Nje ya Nchi.

Taarifa ya Chama hicho iliyosambazwa kote Duniani hii hapa

View attachment 3358159
vibaka na matapeli wa kisiasa nchini wanatafuta kiki za kilofa kwa udi na uvumba na wanasiasa waliopoteza uelekeo nchini 🐒
 
Ikumbukwe kwamba kuna amri ya Haramu iliyotolewa na viongozi wa Tanzania ya kuzuia Viongozi wa Chadema kusafiri Nje ya Nchi.

Nabii huyo wa Mungu amenyang'anywa Passport yake na kutakiwa kuripoti Uhamiaji Makao Makuu Dodoma ikiwa ana Malalamiko yoyote.

Taarifa ya Chama hicho iliyosambazwa kote Duniani hii hapa

View attachment 3358159
Samia The Killer angekuwa Hawa (mwanamke wa kwanza duniani) pengine Mungu angeamua kuifuta dunia na kuanza upya tu badala ya kumpa mwanadamu a second chance!
 
Adui wa CCM sio Chadema, adui wa CCM ni mafisadi walio ndani ya CCM na serikali wanaojificha kwa kivuli cha uchawa.
Sana sana CCM wanajitahidi kuitangaza na kuipa umaarufu Chadema.
Kama kuna mtu anakusema na kukutoa makosa, ukimjibu ujue atapaza sauti zaidi ila ukinyamaza ataacha.
 
Tunachojua ni kwamba Chadema imekufa,sasa kufanya vituko vya namna hiyo mnaongeza chadema kupendwa na kuonewa huruma na wananchi.
 
Ikumbukwe kwamba kuna amri ya Haramu iliyotolewa na viongozi wa Tanzania ya kuzuia Viongozi wa Chadema kusafiri Nje ya Nchi.

Nabii huyo wa Mungu amenyang'anywa Passport yake na kutakiwa kuripoti Uhamiaji Makao Makuu Dodoma ikiwa ana Malalamiko yoyote.

Taarifa ya Chama hicho iliyosambazwa kote Duniani hii hapa
============
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga vikali kitendo kisicho halali na chenye msukumo wa kisiasa cha kumkamata Mheshimiwa Godbless Lema, mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, ambaye leo amezuiwa kwa njia isiyo ya haki na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania katika mpaka wa Namanga akiwa safarini binafsi kuelekea Nairobi, Kenya.

Maafisa wa uhamiaji waliomzuia walimueleza kuwa walikuwa wakitekeleza “maelekezo kutoka juu” kuzuia viongozi wa CHADEMA kusafiri nje ya mipaka ya Tanzania—kauli inayotia hofu kubwa inayoashiria matumizi mabaya ya mamlaka ya dola kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kisiasa. Pasipoti yake ilichukuliwa na kwa sasa anazuiliwa katika Ofisi ya Uhamiaji Namanga bila kufuata taratibu za kisheria.

Tunasema wazi: hakuna msingi wowote wa kisheria wa kumzuia Mh. Lema au kumzuia kutoka nje ya nchi. Uhuru wa kusafiri ni haki ya msingi inayotambuliwa na sheria za Tanzania na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.

Soma Pia: Godless Lema: Nimekwama kwenda Nairobi kutokana na zuio la Viongozi wa CHADEMA kusafiri nje ya nchi

Tunamtaka Mheshimiwa Godbless Lema aachiwe mara moja bila masharti yoyote, arejeshewe pasipoti yake, na kukomezwa kwa aina zote za unyanyasaji na ufuatiliaji dhidi ya viongozi wa upinzani. Hili si suala la Godbless Lema pekee, bali ni suala la kulinda heshima, utu na haki za kikatiba za Watanzania wote. Tunatoa wito kwa wananchi, asasi za kiraia, na washirika wa kimataifa kusimama kidete dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka kama haya.

View attachment 3358159
Alitaka kutoroka kwenda Canada atuachie msala. Tumelikoroga tulinywe sote hapahapa.
 
Kuna watu wamepewa madaraka kimakosa sana. Na ushahidi ndiyo huu. Yaani mtu anasafiri kwa nauli yake, halafu unamzuia huku ukiwa huna sababu za msingi.

Haya mambo ya kitoto sijui yataisha lini!
 
Back
Top Bottom