Pre GE2025 CHADEMA yalaani kuzuiliwa kwa Tundu Lissu na Viongozi wa Upinzani kuingia Angola

Pre GE2025 CHADEMA yalaani kuzuiliwa kwa Tundu Lissu na Viongozi wa Upinzani kuingia Angola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali kitendo cha kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wake Taifa, Mheshimiwa Tundu Lissu, kuingia nchini Angola, ambako alipaswa kushiriki mkutano muhimu kuhusu masuala ya demokrasia.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo, CHADEMA imesema kuwa mbali na Mheshimiwa Lissu, viongozi wengine wa upinzani kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine pia wamezuiliwa kuingia nchini humo bila maelezo ya msingi.

Soma: Msafara wa ACT, Lissu wazuiliwa airport nchini Angola, kurudishwa nchini, ACT watoa tamko

Chama hicho kimesema kinatafuta maelezo kuhusu sababu za zuio hilo na kusisitiza kuwa haki za kidemokrasia za viongozi wa upinzani zinapaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

"Tunafuatilia kwa karibu ili kubaini sababu za zuio hili na kuhakikisha kuwa haki za kidemokrasia zinalindwa ipasavyo," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

IMG_3495.jpeg
 
Itakuwa CCM wamepandikiza mamuluki Yao huko Angola
 
Back
Top Bottom