Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 ikiwa na malengo mawili.
Kwanza CHADEMA walikusudia kuonesha kwamba kwa kutumia mfumo huu wa uchaguzi unaopendelewa na CCM, uchaguzi hautakuwa huru wala wa haki.
Jambo la pili ambalo CHADEMA walikusudia kuonesha ni kwamba CHADEMA Ina ushawishi mkubwa sana kwa wananchi kuliko CCM.
Kwenye mambo yote mawili CHADEMA wamefanikiwa.
Kitendo cha wagombea wao kuenguliwa kinyume cha kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024,zilizotungwa na CCM wenyewe, kinaonesha kuwa hoja ya CHADEMA kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri za miji hawafai kusimamia uchaguzi huo na mwigine wowote ule, hoja yao hiyo kuwa ina mashiko.
Kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA bila ya sababu za msingi, kunaimarisha hoja ya CHADEMA kuwa CCM inategemea nguvu ya vyombo vya dola kuendesha siasa zake.
Lakini ukiangalia nguvu wanayotumia CCM kufanya Kampeni zao, unagundua kuwa hawakubaliki kwa wananchi ila wanalazimisha kukubalika.
Lakini kwa upande wa pili CHADEMA Kampeni zao zina muamko mkubwa sana na hoja zao zinaonekana kuvutia hisia za watanzania wengi.
Bahati mbaya sana CCM watafanya kile walichofanya mwaka 2019, watajitangaza washindi.
Kiujumla CHADEMA imepata ushindi mkubwa sana kwenye huu uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.