Chadema yapingana rasmi na CCM kuhamishia makao makuu Dodoma


Kama hutatoa sababu za kuonyesha ni kwa nini unafikiri hivi basi utathibitisha kwamba hujajipa jina lako kwa ajali.
 

Salamu mkuu. Mia kwa 100%.
Ume click vyema
 


The alternative ni utaahira Why? bila sababu wewe ndiye utaonekana taahira
 

Bado tunahamisha makao makuu ya nchi kwa miaka 37! (1973-2010) na haijulikani hili zoezi litaisha lini. Only in Bongo! 😕
 
Mambo mengine ni kupotezeana muda tuu,nchi haina umeme na rushwa kila kona wao wanatuletea debate za ofisi za mafisadi zijengwe wapi...wanyamaze tuu!
 

Hata Babaako Makamba mwenyewe haamini kama Dodoma ni Makao Makuu na hawezi kutoka Hadharani kupingana na CHADEMA katika hili maana hata watu wasio na Akili watamuuliza kwa kumuumbua kwamba mbona mmeshindwa kufanya hivyo for more than 30 years
 
watahama mwaka ujao wa fedha!!
Mbona tulishaanza kuhama siku nyingi tu. Baadhi ya wizara watumishi wake walilipwa gharama zote za kuhama. Wizara ya Maji waliondoka pale Sokoine Drive kuelekea Dodoma wakaishia Ubungo enzi za EL akiwa waziri. TAMISEMI wao walitangulia siku nyingi ingawa bado hawajafika huko Dodoma.
Maofisa wa wizara hizi "zilizohama" wakienda Dodoma wanalipwa tena posho! Hivyo ndivyo tunavyoendesha nchi bila utashi na nia ya kweli kutekeleza yale tunayoyaamua.
 

Kwanza napenda kumwomba J.Mnyika atudhihirishie hiyo kampeni yake yakupinga kuhamishwa makao makuu ya mji wa kiserikali na kibiashara toka Dar to Dom?

.....Alisema mbali na azma yao ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia Makao Makuu kwenda Dodoma majengo yote ya serikali Dodoma yatageuzwa kuwa vyuo vikuu vya elimu na vyuo vya ufundi ili jiji hilo liwe kitovu cha elimu nchini......

Actually i dont get him, wataka kuniambia kuwa majengo mengi ya Dom mjini ni mali ya CCM? au wao wanaajenda fulani yakutaka kubakia Dar,


Wao chadema wataka hayo makao makuu yahamishiwe wapi Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza? hii topic ya kuhamia DOM ilikuwepo to 1980's kwa kukufahamisha, Hapo nikuwauliza hao viongozi wa CCM since that time wao walikuwa wanafanya nini mpaka miaka ina kwenda hawajahamia DOM?

J.Mnyika labda uni convince kwa kujenga hoja ya majimbo hapo natkuelewa ati DAR imeitangulia mikoa mingine mbali sana kiasi kwamba kila kitu its in DAR hata kampeni ya Malaria tu ati itafanyikia Dar what is this? check occasion nyingi tu ni Dar.

To be Honestly Wana JF me ni wakwanza na kukubaliana DODOMA iwe makao makuu ya kiserikali. ndio tuta expand kimaendeleo.



 
- Bravo Chadema, huwezi kuwa unahamia Dodoma, wakati kila siku unachota hela za kodi yetu wananchi na kukarabati Ikulu na Ofisi za serikali Dar kila siku, huwezi kuwa unahamia Dodoma wakati unajenga nyumba mpya za mawaziri Dar, I mean sasa unataka zijengwe Flyovers Dar, now this is insane kama sio insanity!

- CCM wafike mahali wawekwe kiti moto na waamue moja, kama wanataka kuhamia Dodoma au waache mara moja kuharibu hela za wananchi, kwa hili Chadema wako right on the money ni nothing but uwajibikaji, kwanza Chadema wamechelewa sana na hii ishu!

- I mean talking about kero kwa wananchi! kuhamia Dodoma should have been number one ishu on the table!

Respect


FMEs!
 


Ha ha haaa eti waliishia ubungo mataa umenifurahisha kweli Tamisemi walipeleka wafagiaji na watunza bustani wakadai wameshahamia Dodoma hii bongo bwana kaazi kweli
 

Na kwa taarifa yetu maafisa na wahandisi kutoka Serikali ya Nigeria miaka hiyo ya nyuma walikuja kujifunza kutoka Tanzania mbinu za kuhamisha Makao Makuu toka Lagos kwenda Abuja. Labda tuwaulize waliokuwa CDA ilikuwaje Nigeria wakatu-overtake baada ya kujifunza kutoka kwetu? Tanzania itajengwa na wenye Moyo!
 


Hakuna haja ya kutafuta mchawi wakati anajulikana tusiwasingizie CDA wao wanapokea amri kutoka serikali kuu Tanzania haitajengwa na wenye moyo pekee bali wenye moyo safi na wazalendo halisi wa Tanzania.
 
Hakuna haja ya kutafuta mchawi wakati anajulikana tusiwasingizie CDA wao wanapokea amri kutoka serikali kuu Tanzania haitajengwa na wenye moyo pekee bali wenye moyo safi na wazalendo halisi wa Tanzania.
I salute you sir and I totally agree with you that Tanzania itajengwa na wenye moyo safi na wazalendo halisi. But all in all CDA was the "authority" ndio waliokuwa wamepewa jukumu la usimamizi na utekelezaji kwa hiyo wao wako kwenye position nzuri ya kutuelewesha vizuri zaidi ni wapi tulipokwama na kwa nini tulikwama katika azma ya Serikali kuhamia Dodoma maana. Perdiem is such a flimsy excuse!
 
Sasa mkuu huoni kuwa pia wanafunzi wanahitaji huduma muhimu ambazo hazitapatikana huko mapolini nafikiri labda Chadema imeona kuhamia Dodoma italigharimu taifa mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kusaidia secta zingine
nikweli chadema wanahuruma na fedha zitakazo tumika wakati huwo ni bora sekta muhimu ziboreshwe
 
hivi serikali ya tanzania wanatuona kuwa watanzania niwajinga sana na hatutaki kufahamu yaliyo ndani ya seikali yetu? kwakuwa kunashutuma za kweli za chenge mbina mapaka sasa hawajibishwi wakati imegundulika kulikuwana hujuma tena mpaka washikaji wanatulipa chenge awajibishwe huyu simtu wa kumchekea ni hatari kwa taifa mjadala uendelee mpaka kieleweke
 
YOU KNOW WHAT.....!
WANA UCHAGUZI AMBAO TAYARI ULISHAKUMBWA NA KASHFA YA RUSHWA UCHAGUZI CHADEMA
SASA WANATAFUTA HOJA MBADALA KUEPUKANA NA HILI.....!WAMEKURUPUKIA HOJA DHAIFU AMBAYO KWAYO HAWATOKI......!
Dodoma utabaki kama ilivyopangwa....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…