carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka Serikali kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa na wa kitaifa ufanyike kufuatia matukio ya mauaji ya Oktoba 29, 2025, huku akisisitiza kuwa familia za wahanga wa mauaji hayo pamoja na majeruhi wanapaswa kulipwa fidia.
Mnyika ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa mauaji ya Oktoba 29, 2025, yaliyoandaliwa na CHADEMA
“Tumeendelea kusisitiza wakati wote katika mambo haya ya mauaji ya Oktoba 29 na siku zilizofuatia tunataka ufanyike uchunguzi huru wenye kuhusisha vyombo huru vya kimataifa na wadau huru wa kitaifa ili ukweli ukijulikana na haki itendeke, na tumetaka wakati wote wahanga wa mauaji, familia zao zilipwe fidia na wale waliojeuriwa waweze vilevile kulipwa fidia”, ameeleza Mnyika.
Aidha, Mnyika ametoa rai kwa wanachama wa CHADEMA wa Dar es Salaam na nchi nzima kujitokeza kwa wingi mahakamani tarehe 6 Novemba, 2026 kusikiliza na kumuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, ambapo uamuzi wa shitaka lake la uhaini utafanyika siku hiyo.