CHADEMA yataka maelezo juu ya zuio la Zanzibar la kutouza nje Sukari na Mchele

Kalime acha kulialia. Unataka ushibe kwa hasara ya mkulima?
Kunywa chochote kwa bili yangu kaka. Yaani wakati mkulima anataabika wao nashabikia siasa alafu leo wanataka serikali impangie mkulima pa kuuza kwa manufaa yao
 
Rais wa huko hana akili na akiua Kilimo na Biashara ndio atatia akili,Tanzania Kuna mfumuko wa bei? Kuweni serious basi

Unawezaje kuzuia kuuza nje kitu ambacho huzalishi? Ni sawa leo hii tusikie kuwa Serikali ya JMT imezuia uuzwaji wa matrekta nje ya nchi. Au alimaanisha wafanyabishara wa Zanzibar wanaoagiza mchele toka bara, wakiufikisha mchele Zanzibar, ni marufuku kuutoa nje ya Zanzibar?
 
Hoja ya Mwalimu wa CDM Zanzibar sijaielewa Hadi sasa.
 
Ni maandalizi ya mwezi wa Ramadhan... ! Ukipita ama soon baada ya Sikukuu zuio litaondolewa..
 
Wewe ndo nmekuelewa,

Maana walizuia exportation, bt importation Iko pale pale.

Imelenga kupunguza inflation Kwa manufaa ya raia.

Hivi vyama vya upinzani, tuwe makini navyo sana sometimes, hutoa matamko kupata political advantage in case malengo ya Watawala yakifail bila kujali yalikuwa mema au mabaya.
 
Zanzibar wamestuka

Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikitangaza zuio la uuzaji nje ya nchi bidhaa ya sukari na mchele, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kimeitaka itoe maelezo ya kina juu ya marufuku hiyo.
Kimesema uamuzi huo umefanyika wakati ambao, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijaweka mikakati ya kutosha kuhusu kilimo cha mazao hayo.

Kauli hiyo ya Chadema inakuja wiki moja baada ya Serikali ya Zanzibar kupitia Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban izuie uuzaji wa bidhaa hizo nje ya nchi.

"Kwa kutekeleza mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 35(1) cha Sheria ya Biashara ya Zanzibar, namba 14 ya mwaka 2013, mimi Omar Said Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

"Naagiza katazo la kusafirisha mchele na sukari nje ya Zanzibar kwenda nchi yoyote, kuanzia tarehe 30 Januari, 2023," imeeleza katika taarifa hiyo ya Omar.

Leo, Februari 10, 2023 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amewaaeleza waandishi wa habari kuwa kilichofanywa na Serikali hiyo ni sawa na kujifungia.

"Hakijatosha kutoa tu tamko hilo ipo haja ya Serikali (Zanzibar) kutoa maelezo ya kwanini imefikia uamuzi huo na mikakati yao ya kuhakikisha hilo linalotokea halitajirudia," alisema.

Alisema wakati Watanzania wanahangaika kutafuta chakula kufungiana kunahatarisha uzalishaji wa changamoto nyingine.

Kama sababu ya uamuzi huo ni kuviwezesha visiwa hivyo kujitosheleza kwa chakula, alisema nyema Serikali ingekuja na mkakati wa uzalishaji katika kilimo.

Kwa mujibu wa Mwalimu, Zanzibar ina maeneo mazuri yanayowezesha uzalishaji wa bidhaa hizo kiasi cha kutosheleza mahitaji ya wananchi na hata kuuza nje ya nchi.

"Uko wapi mkakati mahususi wa Serikali katika kilimo, naamini kama utawekwa mkazo visiwa hivyo vinaweza kupata chakula cha kutosheleza na kuuza nje," alisema.

Hata hivyo, alisema visiwa hivyo ni kitovu cha biashara kulingana na historia yake, kitendo cha kuweka marufuku kunafifisha fursa hiyo.

"Zanzibar ni kitovu cha biashara na hiyo ni asili na ndiyo heshima ya Zanzibar, biashara lazima itazamwe kuwa fursa pana na siyo changamoto bila kuathiri ustawi na usalama wa wananchi," alisema.

Tatizo lilipo alisema: "Ni ama juhudi za Serikali ndogo au hazipo kabisa katika baadhi ya maeneo na hatimaye tunajikuta katika kufunga, tutajifungia hadi lini."

Chanzo: Mwananchi
Haaaaa haaaaa. Chadema bwaaana, mmmmmmh
 
Kwa hili Chadema wako sahihi kabisa ,
Tena wamechelewa sana kupinga sera hii ya kufungia mazao na bidhaa za wakulima na kuwanyima soko la uhakika mwisho kuwafanya maskini
Hongera Makamu mkit Cdm Zb ,
Natamani Cdm bara nayo iamke ichukue agenda hii ya kutetea wakulima

Serikali itengeneze mazingira ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula sio kufungia masoko ya wakulima maskini na kuua mitaji yao
 
Hivi mlishawahi kuwaona Msikitini hata siku moja? Ni kawaida kwa Tanzania tangia Nyerere, alikuwa anasali St.Peters, Mzee Mwinyi alikuwa anaswali Kisutu na kwingineko, Mzee Mkapa (RIP) alisali na Magufuli naye alikuwa anasali, wote walikuwa God fearing.

Hamjajua tu bado, wanatengeneza starvation kwa makusudi ipo kwenye globalist agenda 2030 wanayofwata to depopulate Afrika, ni satanic!
Inatengenezwaa Tanzania? Make kuna Baadhi ya nchi za Africa wana jitosheleza kabisa kwa chakula,
 
Hawana akili Hawa wajinga, wanataka mkulima spare hasara ili wao washibe kwa Bei rahisi na wafanye maendeleo mengine kwa fedha inayobak utadhan mkulima yeye hataki hayo maendeleo mengine

Kwani wamezuia kwenda shambani?
Nyie mmelewa maada? Nchi ina vihiyo wengi sana Mungu tusaidie
 
Wewe ni mpambavu kweli, kwa hiyo mkulima ndo akuuzia kwa bei ya hasara mtaji wake ukate , ninyi ndo mmefanya wakulima kuwa maskini kwa miaka 60 ya uhuru

Kama unafikiri kulima ni rahisi nendeni mkalima mje muuze kwa bei mnayotaka ,tumechoka kuwaelimisha
Mpambavu kabisa
Umeelewa andiko linataka nini? Au ni Maada ngumu? Nchi ina vihiyo wasio kuwa na idadi
 
Kunywa chochote kwa bili yangu kaka. Yaani wakati mkulima anataabika wao nashabikia siasa alafu leo wanataka serikali impangie mkulima pa kuuza kwa manufaa yao
Vihiyo mnapongezana, Andiko lina husu kufunga mipaka Je vipi na wengine wakafunga? kwamba Zanzibar wanasema Chakula kisitoke hata kuja Bara na Vipi Bara na wao wakasema kisiende Zanzibar? Shida yenu mnakuwa vihiyo sana
 
Unawezaje kuzuia kuuza nje kitu ambacho huzalishi? Ni sawa leo hii tusikie kuwa Serikali ya JMT imezuia uuzwaji wa matrekta nje ya nchi. Au alimaanisha wafanyabishara wa Zanzibar wanaoagiza mchele toka bara, wakiufikisha mchele Zanzibar, ni marufuku kuutoa nje ya Zanzibar?
Zanzibar inanunua mchele na Sukari kutoka nje kabisa, sasa kuzuia usiingia Bara ni hatari na vipi Bara wakaja kuzuoa na wao?
 
Hoja ya Mwalimu wa CDM Zanzibar sijaielewa Hadi sasa.
mwalimu anasema kama Zanzibar wanazuia Mchele na Sukari visitoke nje ya Zanzibar hata kuja Bara vipi siku na Bara wakaja kuzuia vyakule visiende Zanzibar? Kilichopo ni kuzalisha kwa winhi au badi kufidia na sio kufunga mipaka, vipi Bara wakaja kufunga na wao?
 
Back
Top Bottom