PostGE2025 CHADEMA yatangaza kutoitambua Serikali ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kusema si halali, au ni haramu haitasaidia chochote ! Kaeni yafanyike maridhiano tuone tunafanya Nini kuepusha migogogoro iso ya lazima!
Lasivyo mkitakacho hasa kwa vurugu hakitafanikiwa asilani
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Desemba 11, 2025, CHADEMA imetaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyosimamia uchaguzi huo ikisema tume hiyo “haina uhuru, haina uaminifu na haiwezi kusimamia uchaguzi wa haki.”

Katika maelezo yao, chama kimeorodhesha matukio kadhaa ya kile walichokiita ukandamizaji ikiwamo kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa, kufungiwa akaunti za chama, kukamatwa kwa viongozi, kuzimwa kwa mitandao, kutekwa na kupotezwa kwa raia, pamoja na kupigwa risasi kwa wananchi wakati wa uchaguzi, huku ikitaka miili ya watu waliouawa kukabidhiwa kwa familia zao ili “izikwe kwa heshima za Kitanzania.”

Kutokana na matukio hayo CHADEMA imetaka kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayowekwa chini ya uangalizi wa taasisi za kimataifa, kurejesha utulivu na kufungua anga la kisiasa.

Chama hicho kimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwawekea vikwazo wote waliotajwa kuhusika katika uhalifu wa kibinadamu, huku kikipendekeza fedha za misaada zisipelekwe serikalini bali kwa asasi huru.

Chanzo Jambo TV
Kwa wanaofuatilia siasa hakuna jipya. Hawakuitambua Serikali ya awamu ya 5 hadi walisusia hotuba ya Rais bungeni wakatoka nje. Walisusia uchaguzi wa marudio Zanzibar hadi wakaenda UN.
Wakae wajipange wajenge chama. Karne ya 21 haihitaji harakati za miaka 1960s.
 
Waendelee kutokuitambua cha muhimu wanalipa kodi nyumbu hao.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Desemba 11, 2025, CHADEMA imetaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyosimamia uchaguzi huo ikisema tume hiyo “haina uhuru, haina uaminifu na haiwezi kusimamia uchaguzi wa haki.”

Katika maelezo yao, chama kimeorodhesha matukio kadhaa ya kile walichokiita ukandamizaji ikiwamo kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa, kufungiwa akaunti za chama, kukamatwa kwa viongozi, kuzimwa kwa mitandao, kutekwa na kupotezwa kwa raia, pamoja na kupigwa risasi kwa wananchi wakati wa uchaguzi, huku ikitaka miili ya watu waliouawa kukabidhiwa kwa familia zao ili “izikwe kwa heshima za Kitanzania.”

Kutokana na matukio hayo CHADEMA imetaka kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayowekwa chini ya uangalizi wa taasisi za kimataifa, kurejesha utulivu na kufungua anga la kisiasa.

Chama hicho kimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwawekea vikwazo wote waliotajwa kuhusika katika uhalifu wa kibinadamu, huku kikipendekeza fedha za misaada zisipelekwe serikalini bali kwa asasi huru.

Chanzo Jambo TV
Unajua heche jaribu kujiheshimu mlikataa uchaguzi wenyewe leo unatokea wapi kutaka uchaguzi ufutwe kirahisi tu kama unavyofikiri hebu wacha nchi ikae kama ilivyo mpaka 2030 ndio uje na hoja mpya tumewachoka hata mnachokitaka hakieleweki
 
Chama Cha Vichekesho.. hawaitambui serikali lakini wametoa tamko la kuitaka serikali kulipa fidia ndugu za waliouwawa tarehe 29 Oktoba.Haya ni maajabu
 
Kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kutoitambua hili genge haramu lililotwaa madaraka kwa mtutu wa bunduki October 29.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Desemba 11, 2025, CHADEMA imetaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyosimamia uchaguzi huo ikisema tume hiyo “haina uhuru, haina uaminifu na haiwezi kusimamia uchaguzi wa haki.”

Katika maelezo yao, chama kimeorodhesha matukio kadhaa ya kile walichokiita ukandamizaji ikiwamo kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa, kufungiwa akaunti za chama, kukamatwa kwa viongozi, kuzimwa kwa mitandao, kutekwa na kupotezwa kwa raia, pamoja na kupigwa risasi kwa wananchi wakati wa uchaguzi, huku ikitaka miili ya watu waliouawa kukabidhiwa kwa familia zao ili “izikwe kwa heshima za Kitanzania.”

Kutokana na matukio hayo CHADEMA imetaka kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayowekwa chini ya uangalizi wa taasisi za kimataifa, kurejesha utulivu na kufungua anga la kisiasa.

Chama hicho kimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwawekea vikwazo wote waliotajwa kuhusika katika uhalifu wa kibinadamu, huku kikipendekeza fedha za misaada zisipelekwe serikalini bali kwa asasi huru.

Chanzo Jambo TV
Wakati wanapokea RUZUKU walikuwa wanaotambua!

Wakati WANAPOKEA RUZUKU walikuwa wanaitambua.🤣
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Chanzo Jambo TV
Duh...! Ila kuhusu hili la kutoitambua serikali na kutomtambua rais, nilisha toa ushauri Thread 'Fact: Samia ndiye Rais wa JMT!, Uwe ulimchagua, hukumchagua, hukupiga Kura, uko Tanzania au Ughaibuni, unamtambua, humtambui, SSH ndiye Rais wako!' GE2025 - Fact: Samia ndiye Rais wa JMT!, Uwe ulimchagua, hukumchagua, hukupiga Kura, uko Tanzania au Ughaibuni, unamtambua, humtambui, SSH ndiye Rais wako!
P
 
Unajua heche jaribu kujiheshimu mlikataa uchaguzi wenyewe leo unatokea wapi kutaka uchaguzi ufutwe kirahisi tu kama unavyofikiri hebu wacha nchi ikae kama ilivyo mpaka 2030 ndio uje na hoja mpya tumewachoka hata mnachokitaka hakieleweki
Akili ya mohd kawaida
 
Hawakuitambua ya mshua Magu ila vibaraka wao wakaleta mabalozi nani chizi kati Yao?
Sasa basi Maisha yataendelea na kutoitambua kwao hivyo hivyo!
 
Back
Top Bottom