PostGE2025 CHADEMA yatangaza siku saba za maombolezo kuwaenzi waliofariki wakati wa uchaguzi mkuu 2025

PostGE2025 CHADEMA yatangaza siku saba za maombolezo kuwaenzi waliofariki wakati wa uchaguzi mkuu 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza siku saba za maombolezo kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2026, kwa ajili ya kuwaenzi na kuwakumbuka watu waliopoteza maisha Oktoba 29, 2025, wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Tangazo hilo limetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa, katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.

Golugwa amewaomba Watanzania kuvaa nguo nyeusi au kufunga kitambaa cheusi kwenye mkono wa kushoto katika kipindi chote cha maombolezo, ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka marehemu.

"Tunawaomba Watanzania wote tuvae nguo nyeusi kuanzia tarehe ya leo tarehe 29 mpaka tarehe 4 mwezi wa 11 tuvae nguo nyeusi au iwapo umevaa nguo ya rangi nyingine ufunge kitambaa cheusi katika mkono wako wa kushoto kama ishara ya majonzi na kumbukumbu na mshikamano..

"Leo tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka 2026 mwaka mmoja tangu lilipotokea tukio ambalo limeacha simanzi katika mioyo na maisha ya watanzania walio wengi Tanzania na Afrika na dunia nzima kwa ujumla tulishuhudia vifo vya mamia kwa maelfu ya watanzania majeruhi wengi walioachwa na ulemavu wa kudumu."
 
Wacenge hao yaani wanaharakati na TEC wana Nguvu kuliko CHADEMA, CHADEMA siku hizi Mapunga tuu
 
Nini siku Saba, watangaze hata miezi mitano. Samia atatoka ikulu muda wake wa haki utakapopita.
 
Back
Top Bottom