Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kimetishia kuandaa maandamano ya nchi nzima yenye lengo la kushinikiza serikali kufufua mchakato wa Katiba Mpya na kuachiliwa huru kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche ndiye ambaye ametangaza azma hiyo ya Chadema ya kuitisha maandamano nchi nzima, wakati akihutumia maelfu ya wananchi katika kituo cha mabasi cha Kabwe jijini Mbeya.